Yaani acha tu unaweza usitoke kabisa kituo cha polisi ndio maana labda watu wanaogopa atakujitokeza kuwatumbua wauza unga na majambazi yanayojulikana mtaani kwao; leo tena ujifanye unaenda kusema mambo ya ufisadi serikarini kwa utaratibu huu ujitakii mema. Sasa tena ata huku kwenye faragha nako awatakii watu waseme hii ndio polisi yenyewe isiyotaka tips hawa kweli wana nia ya kupambana na wanayosema.KWA MTINDO HUU WA KUANDAMA WHISLE BLOWERS SIDHANI KAMA KUNA RAIA ATAKUWA TAYARI KUSHIRIKIANA NA POLISI KUZUIA UHALIFU. YAANI MTU UNATOA TAARIFA YA KIFISADI BADALA KUPONGEZWA, UNAKANDAMIZWA!
HATA NA MM NATUA NENOTusimame kwa pamoja kuitetea JF bila kujali itikadi zetu.
Natamani kila member atie neno kwenye uzi huu.
Kampuni ya Jamii Media ambayo ndiye wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya JamiiForums na FikraPevu wamewasilisha mashtaka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga ushuruti waliopewa na Polisi kutoa taarifa binafsi za wanachama wake.
Ushuruti unakuja kutokana Sheria ya Uhalifu Mitandaoni (Cyber crime law).
Taarifa ya kilichojiri zitawajia punde.
ile kesi ya msingi kuhusu cybercrime iliyofunguliwa kipind kile imeishia wap?
jitafutie ulinzi haraka, hali si shwariThis one
Kwahiyo mahakama si huru tena ?jitafutie ulinzi haraka, hali si shwari
Kesi kama hizi zinakuwa na nguvu kwenye nchi zinazofuata sheria , nchi zinazosigina katiba ni kazi bure tu , kesi ya msingi haijafika hata nusu , mkuu wa jf kakamatwa !Bongo hii kila kitu kinaenda na kupita kama upepo! Anyway yeyote mwenye taarifa hii !
cc. Invisible
sio mahakama tuKwahiyo mahakama si huru tena ?
Jamani Ben!Kwa Heshima ya kipekee nawapongeza Jamii Media kwa kuamua kulinda Uhuru na faragha ya watumiaji wa Mitandao na pia kwa kupigania haki ya kikatiba ya watanzania na kupingana na masharti kandamizi yasiyo ya kistaarabu katika karne hii ya sayansi na Teknolojia
Nimekua mwanachama wa JamiiForums Tangu Tarehe 18 July,2007 nikiwa Mwaka wa Pili Chuo kikuu na hapo kabla nilikuwa Mwanachama ambaye sikuwa nimesajiliwa
Tumekuwa na WanaJF wengi hapa wenye fani na taaluma mbalimbali.Pia viongozi wa Vyama,Serikalini,Mashirika na hata viongozi wa Dini.Wengine kwa majina yao halisi na wengine ya kificho (Baadhi yao Tunatambuana).
Katika Uanachama wangu JF nimewahi kupata misukosuko mingi na Jeshi la Polisi kutokana na michango yangu humu likiwemo tukio la Kuitwa Polisi asubuhi ya Tarehe 20 December 2013 siku ya Ijumaa na kuhojiwa kisa nilianzisha mjadala dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kipindi Hicho Emmanuel Nchimbi.
Polisi waliniambiwa kuna jalada ambalo liletwa na Dr.Nchimbi.Nikiambatana na Wakili Msomi Peter Kibatala Nilihojiwa kwa masaa kadhaa hadi kufukua thread na kuomba Password zangu za JF na Barua Pepe .Niliwakatalia kwa kuwa hawakua na haki hiyo
Hata hivyo Jioni yake kufika saa 3 Usiku aliyepeleka Jalada Hakuwa Waziri tena(Rejea Operesheni Tokomeza Bungeni).Ilikuwa Coincidence au Mipango ya Mungu?
Ni katika mazingira hayo niliona tishio la haki ya uhuru wa faragha na jinsi ambavyo vyombo vya dola pasipo uhalali wowote wanaweza kuhujumu haki za Raia na pia kukandamiza kabisa uhuru wa habari,haki ya kupewa Taarifa na pia kukandamiza haki za msingi kabisa za binadamu na kutishia misingi ya ukuaji wa utawala bora ambayo inashikiliwa na nguzo kuu mbili za uwazi na uwajibikaji
Ni jambo la ajabu kuwa serikali iliyoahidi kurekebisha sheria ya mitandao inaendelea kutumia dola kukandamiza vyombo vya habari
Kwa uamuzi huu wa JamiiMedia,Nitaungana katika mapambano haya kuilinda sio Jamii Forums Pekee bali haki za watanzania
JF ni nyumbani,Ni Chuo .Tubuni njia ya kuisapoti JF kwa kishindo katika kipindi hiki
Kwahiyo mahakama si huru tena ?