Fomula za Masikini na Tajiri

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,165
10,052
FOMULA ZA MASIKINI NA TAJIRI

Na, Robert Heriel

Asikuambie mtu maisha yana Fomula. Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaofikiri kuwa maisha ni bahati nasibu basi utakuwa umefikiri vibaya. Maisha yanafomula. Sio maisha tuu, kila unachokiona na hata kile usichokiona kina Fomula.

Maisha ni hisabati, ni somo la number. Ndio maana kila kitu kila kitu kinatawaliwa na muda, muda ni namba. Hili peke yake kulifahamu ni sehemu ya mafanikio.

Leo Taikon nataka tujadili fomula za watu masikini kisha fomula za matajiri. Nina sababu za kujadili jambo hili kwa manufaa yangu na watu wengine watakaoona umuhimu wa makala hii.

Katika maisha hakuna jambo gumu kama kuwa masikini. Halikadhalika hakuna jambo gumu kama kuwa tajiri. Ili uwe masikini lazima uwe umeamua kuwa masikini, halikadhalika ili uwe tajiri lazima uwe umeamua kuwa tajiri. Anhaa! Kumbe umasikini na Utajiri ni maamuzi, jibu ni ndio.

Masikini ni shujaa kama alivyo tajiri. Kwani sio kazi rahisi kuwa masikini au kuwa tajiri. Kazi rahisi ni kuwa tabaka la kati. Yaani sio tajiri wala sio masikini.

Kumtabiria mtu utajiri au umasikini ni kazi rahisi mno, hii utazingatia zaidi fomula anazozitumia.

Ukiona mtu anakuambia wewe utakuwa masikini, au utakuwa tajiri basi jua kuna fomula kaziona ambazo unazitumia.

Kuna aina mbili za Fomula zinazowaongoza matajiri na masikini
1. Fomula za Kiroho
2. Fomula za kimwili

Fomula za Kiroho ni zile fomula zinazotokana na msukumo wa ndani ya mtu, na hizi zitajikita katika mambo yafuatayo

1.1. Mtazamo (ATTITUDE)
Mtu anakuwa vile ajionavyo, je anamtazamo gani na maisha, je amejiweka kundi gani katika maisha. Kumbuka kwenye maisha lazima mtu yeyote achague kundi lake. Ikiwa ni tabaka la chini au kati au tabaka la juu. Mtu ataendesha maisha yake kulingana na mtazamo wake.

Katika mtazamo ndio msingi wa maisha ya kiumbe. Mtazamo wa simba mbugani ni tofauti na mtazamo wa nyati. Simba licha ya kuwa ni mdogo kimaumbile lakini anajiona yeye ni mkubwa, mfalme, anayestahili kuheshimiwa, kutiiwa, na kama hutomfanyia hivyo basi atalazimisha ufanye hivyo. Lakini Nyati licha ya ukubwa pengine hata nguvu anazo kumzidi simba lakini kinachomuangusha ni mtizamo wake akutanapo na simba. Yeye anajichukulia ni dhaifu, anastahili kunyenyekea, kutii na hata akiwa mkorofi kujitetea anaona kama anafanya makosa.

Mtazamo wa masikini ni kuwa; anajiona ni duni, hawezi, yeye ni wa kusaidiwa, anaamini bila mtu mwingine yeye hawezi kufanya lolote. Masikini anajiona yeye anapaswa amuheshimu tajiri, amuogope na kumtumikia. Wakati Tajiri mtazamo wake anajiona yeye ni bira, anaweza kila kitu, anastahili kuombwa sio kuomba, anajiona yeye ndiye anaweza kila kitu zaidi ya wengine hivyo haogopi kujaribu, anajiona anastahili kuheshimiwa, kuogopwa na kutiiwa.

1.2. FALSAFA

Falsafa ni kile anachoamini mtu na kinachomuongoza kufanya jambo lolote. Masikini wanafalsafa zao na wana yale yanayowaongoza. Umasikini ni imani halikadhalika na utajiri ni imani. Imani huzaa dini. Dini ni njia ya kumtafuta Mungu au shetani. Unapozungumzia dini lazima uhusishe imani, unapohusisha imani lazima uhusishe shetani na Mungu. Lakini lazima ujiulize Mungu ni nani, na kama hatumjui je anawakilishwa na mambo gani. Ipo hivi. Mungu ni Nguvu, uweza, mamlaka, utawala, utajiri, uzuri na mambo yote yenye kupendeza. Ikiwa Mungu huashiriwa na mambo hayo basi shetani huashiriwa na kinyume cha mambo hayo.

Umasikini ni imani kumfuata shetani, wakati utajiri ni njia kumfuata Mungu. Kumbuka huwezi kuwa masikini bila kuzingatia fomula za kishetani, na huwezi kuwa tajiri bila kufuata fomula za Mungu.

Falsafa ya masikini ni maombi, yaani masikini anaamini kuwa akimuomba Mungu atapewa, wakati falsafa ya Tajiri ni kutafuta, tajiri anaamini akitafuta atapata utajiri. Masikini akishaomba kwa muda akiona hapati wakati huo tajiri keshatafuta akapata, masikini anaamini Mungu amemuumba tajiri ili amsaidie yeye, hivyo anageuka kuomba tena kwa tajiri. Yaani anamuomba Mungu kisha anakuja kuomba kwa tajiri na kote hapati.

Falsafa ya masikini ni kuwa kupata na kukosa ni majaliwa ya Mungu lakini tajiri haamini katika hilo, tajiri anaamini kukosa ni uzembe, na kupata ni kulingana na jitihada zake. Tajiri anaamini amepewa mamlaka ya kutawala dunia na yote yaliyomo, hivyo hana haja ya kumuomba Mungu kwani Mungu alishampa vyote, wakati masikini anaamini kila kitu ni cha Mungu hivyo anapaswa aombe tena kwa kujipendekeza.

Tajiri kwa imani yake anatumia muda mwingi kufanya kazi, wakati masikini anatumia muda mwingi kuomba iwe ni kwa Mungu, shetani au kwa wanadamu

2. FOMULA ZA KIMWILI
Hizi ni fumola za maumbile ya mwili na akili. Fomula hizi huchochewa na fomula za rohoni.

Akili ndio nguzo kuu ya fomula za kimwili. Kila kitu hufanywa kwa akili hapa duniani.

Akili ya masikini ni tofauti na akili ya tajiri.

Akili haionekani lakini inadhihirishwa na mambo yafuatayo;
1. Uvumbuzi wa matatizo na kuvumbua suluhisho
2. Kujithamini na kujipenda
3. Kusoma alama za nyakati
4. Kumbukumbu
5. Ubashiiri na matarajio
6. Utunzaji wa mali na mazingira
7. Mahusiano

2.1. Uvumbuzi wa matatizo na suluhu zake
Akili ya tajiri inauwezo wa kuvumbua tatizo linalomkabli yeye mwenyewe bila msaada wa mtu kisha kulitafutia ufumbuzi. Hii ni tofauti na Akili ya Masikini ambaye kwa kawaida hana uwezo wa kujua tatizo linalomkabili hivyo hutafuta msaada kwa watu wengine, usishangae kuona masikini wengi wakienda kwa waganga wakienyeji ati wakidhani wamelogwa, ndio akili za kimasikini zilivyo, kisha waganga kwa vile nao ni wajanja watakuambia umelogwa na fulani. Au masikini kila mara tunawashuhudia kwenye makanisa ya upako wakidanganywa kila kukicha.

Mtu hafanikiwa kwa sababu labda ni mvivu, au anamatumizi mabaya ya fedha, au hana malengo yoyote alafu anasema amelogwa, ndio akili za kimasikini.

Tajiri yeye atafanya kazi zake, kisha atafanya tathmini kwa wiki, mwezi robo mwaka, nusu mwaka, kisha mwaka mzima alafu atajaribu kuona ni kwa nini anafeli au amefaulu kwenye jambo lake, baadaye atajiuliza kipi apunguze au kipi aongeze.

Ili uvumbue tatizo lazima ujifanyie tathmini ili ujue ni wapi unafeli na wapi unafaulu na ujue sababu za mambo hayo. Masikini hawanaga tathmini hivyo sio rahisi kujua tatizo lipo wapi.

2.2. KUJITHAMINI NA KUJIPENDA
Masikini mara zote hajithamini wala hajipendi. Mtu anaishi mazingira magumu, mtu anakula mlo mmoja, mtu anavaa nguo moja kama sanda badala ahangaike kutatua kero zake, yeye anahangaika kuseng'enya watu wanaohangaika kujinasua na makucha ya umasikini. Tena masikini huyu anamiguu, anamikono, anaakili nzuri kabisa, hana upungufu wowote lakini kwa vile ameamua kuwa masikini kwa kutumia fomula za kimasikini analalamika.

Tajiri anajithami, anapenda ale vizuri, aishi pazuri, awe na usafiri mzuri, avae vizuri, hivyo muda wake mwingi atautumia kuhangaika kutafuta pesa ili atimize hayo. Mtu anayejithamini hawezi kuwa masikini. Mtu anayejipenda kamwe hawezi kuwa masikini.

Kujithami na kujipenda ni dalili ya akili. Ukithamini na kujpenda hata watu watakupenda na kukuthamini. Ajabu ni kuwa watu matajiri hata usipowapenda au kuwathamini wala hawajali. Wao kujipenda na kujitamini wao wenyewe inatosha. Lakini hii ni tofauti na Masikini, Masikini wanapenda kupendwa kuliko wanavyojipenda, wanapenda kuthaminiwa kuliko wanavyojithamini. Hiyo nayo ni ajabu.

2.3. KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI
Masikini ni mtu asiyesoma alama za nyakati, wakati Tajiri ni mtu asomaye alama za Nyakati. Na hii inasababishwa na tofauti za akili zao. Masikini hana ule ujanja wa kujihangaisha leo kwa vile ananafasi, ananguvu na afya kisha aweke akiba ya siku atakazokuwa hana nguvu wala afya. Hujawahi kusikia kuwa masikini akipata matako hulia mbwata. Ndivyo ilivyo; Masikini akipata pesa atahangika na wanawake, atakunywa pombe, atafanya anasa pasipo akili, badala afanye hayo yote kwa akili huku akiweka akiba, akiwekeza ili baadaye asijehangaika.

Hujawahi sikia mbuzi wa masikini hazai, ipo hivyo. Ukifika chuo utashangaa maisha ya watoto waliotoka familia masikini, wengi hufanya vioja, hufanya starehe, huvaa kupita kiasi kuliko hata wafanyakazi wa serikalini, hufanya ngono zembe, hii ni tofauti na watoto waliotoka familia tajiri, wao huvaa kawaida, huwezi wakuta wakifanya uhuni, huwezi kuta wakitumia pesa vibaya. Hayo yote sijahadithiwa nimeyaona nilipokuwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Masikini akiajiriwa, hupenda kujitukuza, hupenda mambo makubwa, masikini hajui kuwa mambo makubwa yanahitaji muda na utulivu. Masikini atapanga nyumba ya laki mbili unusu, wakati huo mshahara wake ni laki sita, kisha atanunua gari la mkopo. Badala angechukua chumba cha elfu 40 kwa vile bado yeye ni kijana, hana familia, kisha achukue mkopo afungue biashara, ili ile faida ajengee nyumba yake au anunulie gari, lakini yeye haoni hayo.

Tajiri yeye anajua kucheza na alama za nyakati, anajua ni wakati gani achukue nyumba ya gharama au gari na wakati gani asichukue.

2.4. KUMBUKUMBU
Masikini hana kumbukumbu, niliwahi kusema, kumsaidia masikini ni kupoteza muda. Masikini hanaga kumbukumbu. Hata ukimsaidia hataona ulimsaidia, usishangae yeye huyo huyo ndio akaja kukuangusha.

Tajiri anakumbukumbu, anajua wapi alitoka, nani alimtoa, wapi alipo na yupo na nani, wapi anapaswa kwenda na aende na nani.

Niliwahi kuandika kuwa usioe au kuolewa na masikini. Nilieleza mengi sana kwenye makala ile. Leo nitaongeza kidogo, ukioa au kuolewa na mtu masikini ni mwepesi kusahau mlipotoka. Usishangae ukianza kupata mafanikio akakuacha na kutafuta mwanamke au mwanaume mwingine. Masikini hanaga kumbukumbu, hajali, hathamini na wala hana upendo.

Tajiri lazima awe na watu aliotoka nao kwenye shida, lazima awe nao muda uliopo kisha atakuwa nao muda ujao.

Masikini hanaga kumbukumbu, mtu yeyote asiye na kumbukumbu ni lazima awe masikini piga ua garagaza.

Mifano ipo mingi, hata wewe unaweza kuwa na mfano wa mtu aliyewahi kutoka kwenye maisha ya chini akiwa na watu fulani baadaye akawasaliti baada ya kufanikiwa lakini baada ya miaka kumi akarudi kwenye umasikini.

Tajiri anajua kuwa mtu aliyetoka naye chini anamsaada mkubwa kwenye mafanikio yake. Wakati masikini anaamini katika ubinafsi, yaani anataka kula peke yake.

2.5. UBASHIRI NA MATARAJIO
Masikini hawezi kubashiri wakati ujao, lakini tajiri anauwezo huo. Ili uwe masikini unapaswa ukose uwezo wa kubashiri. Masikini anadhani akipata ataendelea kupata, masikini anafikiri kila siku ni jumamosi. Wakati Tajiri anajua kuwa siku zinatofautiana, leo sio kesho. Anauwezo wa kubashiri kesho akiitumia leo na jana. Kama leo ipo hivi na jana ilikuwa vile basi kesho inaweza kuwa vile.

Mara nyingi tajiri kile anachokitarajia ndicho kinachokuwa. Ili uwe tajiri ni lazima uione kesho yako ikiwezekana na kesho kutwa.

Masikini wanasema kesho ni yamungu, lakini matajiri wanajua kesho ni yake kwani keshaiona na ndio maana amejipanga, amejidhatiti.

Ndio maana Tajiri anauwezo wa kununua shamba huko maporini kwa laki mbili mbili heka kumi akitarajia miaka kumi ijayo atauza au mji utakuwa umefikia mashamba yake, hivyo atauza viwanja kwa bei nzuri ya faida.

Masikini yeye atakuambia mashamba au kiwanja kipo mbali hivyo anakusanya hela ziwe nyingi anunue kiwanja cha karibu, asijue jinsi anavyokusanya hela ndivyo viwanja vinavyopanda bei, tena pesa haikusanyiki. Mwisho umri unaenda hana kiwanja na hana uwezo wa kununua.

Kubashiri ni uwezo wa kuiona kesho au kesho kutwa au hata miaka mia ijayo kwa kutumia leo na jana.

Wazungu wao wanaona hata miaka elfu moja ijayo. Nafikiri unanielewa.

2.6. UTUNZAJI WA MALI NA MAZINGIRA
Masikini hawezi kutunza mali na hiyo ni moja ya sababu ya chanzo cha umasikini wake. Sio kila masikini ni mvivu, masikini wengine ni wachapakazi tena wanapata hela nyingi tuu lakini utashangaa kwa nini hawapigi hatua. Jibu ni kuwa sio watunzaji wa mali. Hawawezi kutunza pesa, mali kama mashamba, viwanja, nyumba n.k. Wengi wakipatwa na shida ndogo wanauza mali zao kwa bei ya hasara, atakuambia anajua kuzisaka si nilikuambia kuwa hawezi kubashiri kesho, amesahau kuwa kadiri anavyokuwa mtu mzima ndivyo nguvu ya utafutaji inapungua.

Masikini hawawezi kutunza mazingira, hawawezi kutunza viumbe wanaowazunguka. Utashangaa kuona paka au mbwa wa masikini alivyokondeana, alafu masikini hajali, haoni hiyo ni shida, au anaishi sehemu hakuna mti hata mmoja, haoni hiyo ni shida, anaishi na panya ndani, haoni hiyo ni shida, anaishi na mbu ndani na wala haweki neti, haoni hiyo ni shida. kwa ujumla masikini hajithamini na kamwe hatathaminika.

Tajiri anatunza mali yake, anajua ni wakati gani aiuze na wakati gani asiuze, anaakiba hata matatizo yakitokea anajua namna ya kuyakabili, anatunza mazingira. Nenda kwa matajiri uone jinsi walivyopanda miti na maua ya kupendeza, utafurahi mwenyewe, angalia viumbe wanaowazunguka, wajali viumbe wanaowazungika, wanajua ni sehemu ya familia. Tajir ukimuuliza mpo wa ngapi atakuambia, yupo yeye, mkewe, watoto, na junior(jina la mbwa) pamoja na senior(jina la paka) wanafurahia maisha.

Kupanda miti wala hakuna gharama, ipo miti mingi mizuri ya kuvutia huko porini kama huna hela ya kununua. Yapo maua mazuri wala sio gharama. Lakini utashangaa ukifika kwa masikini, yupo yupo tuu. Kakalia mambo ya hovyo.

2.7. MAHUSIANO
Masikini kamwe hawezi kuwa na mahusiano mazuri ndani ya ndoa na kwenye jamii. Ndani ya ndoa, hataweza kuilisha familia yake ikaridhika, hii itafanya mke aanze kuwa mjeuri, na watoto kumdharau Baba. Mke akiwa mjeuri hakuna namna utakayoweza kufanya watoto wasikudharau.Mke anavaa nguo moja kama sanda, ananuka jasho kama beberu kisa huwezi kumnunulia mafuta mazuri, na marashi, ananuka mdomo kisa umeshindwa kumnunulia dawa ya meno. Hata akikusaliti hawezi kukusaliti pakubwa kwani ataenda kwa makapuku wenzako. Tajiri hawezi chukua mwanamke kama huyo.

Kwanini usimfanye mkeo apendeze, anukie vizuri, anawiri, hata kama akikusaliti unauhakika atakusaliti sehemu inayoeleweka, Shida haina adabu, ukiona unaheshimiwa na mkeo ujue ipo sababu ya yeye kukuheshimu. Heshima yoyote inasababu. Hakuna heshima bila sababu.

Masikini wanapenda kuheshimiwa na wake zao wakati wao wenyewe hawawaheshimu wake zao. Mke anapaswa kukusikiliza na kukutii ikiwa unamheshimu. Na mwanaume anamheshimu mke wake kwa kumtunza, kumlinda, kumthamini, kumpendezesha. Sasa kama hufanyi lolote kati ya hilo unataka yeye akuheshimu kwa lipi.

Mungu mwenyewe tunamheshimu kwa sababu, kama pasingekuwa na sababu wala tusingemheshimu.

Masikini kwenye jamii hataheshimika kwa sababu, hatochangia kwenye michango ya kijamii, yeye kila siku hana pesa. Masikini viumbe wake lazima wawe wezi, ukiona masikini anafuga paka basi paka huyo lazima awe paka shume, paka jizi, paka linalosumbua mtaa. Kuku wa masikini wanasumbua mno, masikini hawezi kuwa na mahusiano mazuri na jamii.

Mbwa wa masikini kero yake ni pale umuonapo, havutii, anatapisha yaani kero tupu. Mara nyingi majibwa ya masikini hunyonyoka manyoya, hukondeana, yaani ukiliona unapoteza focus.

Tajiri anamtunza mke wake, watoto, viumbe alivyonavyo. Ukimuona mke wa tajiri lazima umtamani hilo haliepukiki. Kwanza amevaa vizuri, ananukia vizuri, amenawiri, anatabasamu lislo na mwisho, ukimsalimia anakuchekea, hata usipomsalimia hajali sana anajua umetingwa na mambo yako lakini masikini usimsalimie uone utakavyosemwa, huna adabu, umekuwa kiburi, mara unadharau. Masikini wanapenda shikamoo ungedhani ni chakula.

Paka wa Tajiri hawezi kuwa paka shume, hata umletee nyama yako hawezi kula. Yeye anakula kwa wakati. Mbwa wa tajiri ni mzuri, anavutia, anatabasamu, ni mchangamfu, anaupendo. Kumuona mbwa wa tajiri kunakufanya uwe na focus, utamani kuendelea kumuona.

Tajiri wanamahusiano mazuri kwenye familia na kwenye jamii kwani ni watu wanajali kanuni ya kila mtu na mambo yake. Tajiri hawezi kugombana na watu kwa sababu hana tabia ya kuchunguza wengine, kufuatilia maisha ya watu, ndio maana hata usipomsalimia haoni shida. Lakini masikini kazi yake kuu ni kufuatilia mambo ya wengine, kafanya nini, kasema nini, kala nini, kavaa nini. Tajiri hata uende uchi kanisani au msikitini hawezi hata kushtuka, wala hatakuuliza. Lakini masikini, vaa nguo ya ajabu, pita uone atakavyokusimanga, utafikiri anakupa yeye chakula au aliwahi kukununulia hata nguo moja.

FOMULA ZA UMASIKINI NA UTAJIRI
1. Masikini lazima uwe na akili ya kutegemea wakati tajiri anawaza kujitemea.
Masikini uamini kuwa mtu fulani akusaidie ili ufanikiwe, tajiri uamini kuwa wewe mwenyewe unaweza ukajitahidi mpaka ukafanikiwa

2. Masikini lazima utumie fomula ya ombaomba. Tajiri lazima utumie fomula ya kutafuta.
Ili uwe masikini jitahidi kuingia kwenye dini zinazosiistiza kuomba kwa Mungu ndio kufanikiwa. Ili uwe Tajiri jitahidi kuingia kwenye imani zinazosisitiza kufanya kazi asilimia 90, maombi asimilia 10

3. Masikini tumia kanuni ya ponda mali kifo chaja. Tajiri tumia kanuni ya kuweka akiba na kuwekeza.

4. Masikini penda kupendwa kuliko kujipenda. Tajiri tumia kanuni ya kujipenda zaidi ya kupendwa na wengine.

5. Masikini tumia kanuni ya kila kitu ni mali ya Bwana, MUNGU.Tajiri tumia kanuni ya kila kitu ni mali yako uliyopewa na Mungu. Ni haki yako kuwa navyo.

6. Masikini tumia kanuni ya kipya kinyemi sahau waliokutoa nyuma. Tajiri tumia kanuni ya yakale ni dhahabu au awali ni awali hakuna awali mbovu

Baada ya kuandika kwa kirefu naomba nikuache nawe utafakari kidogo.

Ulikuwa nami

Rober Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 

danielhipoliti

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
965
1,351
Mada nzuri nimeipenda mwenye masikio na asikie

Ingawa naamini Hakuna kitu kinachotea kwa bahati mbaya !

Utofauti wetu ndio uzuri wetu Ata talanta tumepewa tofauti atuwezi wote kua matajiri!

Tutazidiana attitude itatutofautisha


Ili kutimiza mapenzi ya Mungu kwa uadilifu


Lazima atakuwepo Master na slave

Mungu ndiye ameshikilia hatma zetu ni wew kuchagua

Note: jitihada haiizidi kudra.
 

Similar Discussions

41 Reactions
Reply
Top Bottom