Jamhuri yapinga dhamana kwa wanawake waliovishana pete

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,237
2,000
Mwanza. Upande wa Jamhuri umewasilisha hati ya kiapo kuzuia dhamana ya washtakiwa wanne wanaokabiliwa na kesi ya kujihusisha na vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa ya kimtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

Hati hiyo imewasilishwa mahakamani leo Jumatano Desemba 13,2017 na Wakili wa Serikali, Emmanuel Luvinga.

Washtakiwa katika shauri hilo namba 548/2017 ni Milembe Suleiman na Janeth Sonza, mwanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza, wanadaiwa kuvishana pete ya uchumba licha ya wote wawili kuwa wanawake.

Wengine ni Aneth Mukuki anayeshtakiwa kwa kufanikisha sherehe za wawili hao kuvishana pete na Richard Fabian anayekabiliwa na shtaka la kusambaza picha za tukio hilo mitandaoni.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Wilbert Chuma anayesikiliza shauri hilo, mawakili wa utetezi wameomba muda wa kuipitia na kuijibu hati hiyo kwa hati kinzani kwa sababu hawakuwa wameipata kabla ya kuwasilishwa mahakamani.

Ombi hilo lilikubaliwa na Mahakama ambayo imeahirisha shauri hilo kwa muda.
Mawakili wa utetezi ni Ogastin Kulwa, Mashaka Tuguta na Jebra Kimbole.mwananchi
 
Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,951

Watu wa namna hii mbona wengi na polisi haiendi kuwakamata? Hawa wana nini cha tofauti???
 
mij

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
1,967
2,000
Hata me pia naunga mkono hoja tena wastoke kabisa hata hao mawakili wanao watetea pia wabadilikie nao maana wanatetea maovu na mungu anawaona katika hili hawato fanikiwa maisha

Mkuu kazi ya Wakili ni kuisadia mahakama itende haki, hivyo kila mtuhumiwa ana haki ya kuwa na wakili hata aliyeua kwa kusudia. Kwa hiyo wala isikupe shida kosa lao kama ni kupata kifungo watapata tu hata wakiwa na mawakili
 
shungurui

JF-Expert Member
Sep 1, 2008
3,632
2,000
Hayo mambo hakuna atakayeweza kuzuia, devil at work, wapewe watolewe tu, sema yule ambaye anajifanya dume wampeleke jela ya wanaume wenzake kwa siku moja akawasalimie.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom