Jamhuri yampandisha kizimbani Emmanuel kwa kutoa (Publication) taarifa za uongo kuhusu KICHAA

hakukua na haja ya kuandika huo upuuzi facebook, habari za kumtuhumu mtu kuwa amemtoa kafara dada yake haipendezi, kwani bila shaka huyo mtu aliumia sana kufiwa na dada yake, hata kama huyo mtu ni 'kichaa'.
lakini pia jamuhuri iache ujinga wa kesi za hovyohovyo, inaleta tu mrundikano wa kesi zisizo na kichwa wala miguu mahakamani na kuchelewesha haki kutendeka kwenye kesi za msingi.
 
Jamhuri imempandisha kizimbani kijana Emmanuel Mahumbi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa ya uongo katika ukurasa wake wa Facebook.

Mahumbi anadaiwa kuwa mnamo September mwaka 2018 aliandika "KICHAA MMOJA ANATOA KAFARA KIBOYA KWELI. KAENDA KUMUONA DADA YAKE BUGANDO KUMBE NDO ANAMKABIDHI KWA FREEMASONS. SIKU MOJA BAADA YA KUMUONA AKAFA. KAENDA UKEREWE SIKU MBILI BAADAE WAKAFA. KUMBE ALIENDA KUWAKABIDHI FREEMASONS. BOYA KWELI LIAMBIENI LIBADILIKE LITAMALIZA WATU"

#MyTake:
Wanasheria hebu tusaidieni kidogo hapa. Hii kesi kwanini imekuwa criminal? Is there any offence against the state? Ni ajabu kuwa anayedaiwa kuchafuliwa ni kichaa halafu mlalamikaji ni Jamhuri. Tangu lini Jamhuri imeanza kutetea vichaa? Kwanini huyo kichaa mwenyewe asilalamike kwa kufungua Libel defamatory charges mahakamani? Kwanini Mahumbi ameshtakiwa kutoa taarifa ya uongo. Ni uongo upi amesema?

Huyo 'kichaa' aliyetajwa na Mahumbi kuwa anatoa kafara kiboya ni nani? Na kwanini Jamhuri imtetee mtu ambaye ni kichaa? Je Jamhuri inaweza kuthibitisha kuwa kichaa huyo hana uhusiano na Freemasons kama Mahumbi alivyodai? Je Jamhuri inaweza kuthibitisha kuwa kichaa huyo sio boya kama ilivyodaiwa?

Naona kama Jamhuri inaenda kushindwa hii kesi mapema sana kwa sababu haiwezi kuprove allegetions dhidi ya Mahumbi (kumbuka the burden of proof rely to the one who allege). ili Jamhuri ishinde inatakiwa ituambie huyo kichaa ni nani. Then ithibitishe kwamba kichaa huyo hana uhusiano na Freemasons. Tatu iweze kuprove kwamba kichaa huyo hatoi kafara kama ilivyoelezwa. Na mwisho ithibitishe kuwa kichaa huyo sio boya. Kesi kama hizi apewe Wakili Peter Kibatala Hekima Mwasipu au Sheck Mfinanga utazimia kwa burudani, jinsi mawakili wa Jamhuri watakavyokua wakiomba maji mahakamani.!


C&PView attachment 1022673
Na wewe ni walewale tu! Wewe hata mahakamani husitahili kufikishwa.
 
afungwe maisha na wengine wenye akili kama yake iwe fundisho maana kuna watu wanajifanya wanatumia maneno ya kuficha huku wakijua na sisi tuna akili timamu
fumbo mfumbie mjinga haya mafumbo watawatokea puani bavicha
wewe umeshamjua huyo kichaa ni nani?
usije ukawa unadandia treni kwa Mbele.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi ujinga na upumbavu imekuwa Ni Kama busara.huyo kijana ni mjinga japo hawezi kufungwa kwa kuwa sioni kosa kisheria lakini Ni mjinga na anabakia kuwa mjinga.sisi hatufagilii Mambo ya kijinga.
Wewe ni mnufaika makonda
 
afungwe maisha na wengine wenye akili kama yake iwe fundisho maana kuna watu wanajifanya wanatumia maneno ya kuficha huku wakijua na sisi tuna akili timamu
fumbo mfumbie mjinga haya mafumbo watawatokea puani bavicha

Watz wanne mmoja ni kichaa labda amemaanisha
 
Hivi kesi kama hizi masharti ya dhamana yakoje?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom