Jamhuri yampandisha kizimbani Emmanuel kwa kutoa (Publication) taarifa za uongo kuhusu KICHAA

Jiwe kichaa linahangaika sana na issue ndogo ndogo. Nyerere pia aliitwa mchonga.
Jiwe
FB_IMG_1549388257313.jpeg
 
Kwanza
Jamhuri imempandisha kizimbani kijana Emmanuel Mahumbi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa ya uongo katika ukurasa wake wa Facebook.

Mahumbi anadaiwa kuwa mnamo September mwaka 2018 aliandika "KICHAA MMOJA ANATOA KAFARA KIBOYA KWELI. KAENDA KUMUONA DADA YAKE BUGANDO KUMBE NDO ANAMKABIDHI KWA FREEMASONS. SIKU MOJA BAADA YA KUMUONA AKAFA. KAENDA UKEREWE SIKU MBILI BAADAE WAKAFA. KUMBE ALIENDA KUWAKABIDHI FREEMASONS. BOYA KWELI LIAMBIENI LIBADILIKE LITAMALIZA WATU"

#MyTake:
Wanasheria hebu tusaidieni kidogo hapa. Hii kesi kwanini imekuwa criminal? Is there any offence against the state? Ni ajabu kuwa anayedaiwa kuchafuliwa ni kichaa halafu mlalamikaji ni Jamhuri. Tangu lini Jamhuri imeanza kutetea vichaa? Kwanini huyo kichaa mwenyewe asilalamike kwa kufungua Libel defamatory charges mahakamani? Kwanini Mahumbi ameshtakiwa kutoa taarifa ya uongo. Ni uongo upi amesema?

Huyo 'kichaa' aliyetajwa na Mahumbi kuwa anatoa kafara kiboya ni nani? Na kwanini Jamhuri imtetee mtu ambaye ni kichaa? Je Jamhuri inaweza kuthibitisha kuwa kichaa huyo hana uhusiano na Freemasons kama Mahumbi alivyodai? Je Jamhuri inaweza kuthibitisha kuwa kichaa huyo sio boya kama ilivyodaiwa?

Naona kama Jamhuri inaenda kushindwa hii kesi mapema sana kwa sababu haiwezi kuprove allegetions dhidi ya Mahumbi (kumbuka the burden of proof rely to the one who allege). ili Jamhuri ishinde inatakiwa ituambie huyo kichaa ni nani. Then ithibitishe kwamba kichaa huyo hana uhusiano na Freemasons. Tatu iweze kuprove kwamba kichaa huyo hatoi kafara kama ilivyoelezwa. Na mwisho ithibitishe kuwa kichaa huyo sio boya. Kesi kama hizi apewe Wakili Peter Kibatala Hekima Mwasipu au Sheck Mfinanga utazimia kwa burudani, jinsi mawakili wa Jamhuri watakavyokua wakiomba maji mahakamani.!


C&PView attachment 1022673
Kwanza havieleweki, context yake haieleweki
h
 
De Minimis Non Curat Lex Definition: Latin: a common law principle whereby judges will not sit in judgment of extremely minor transgressions of the law. It has been restated as:the law does not concern itself with trifles.
 
Mna complicate maisha sijaona kosa hapo heshimuni Uhuru aisee ukifatilia watanzania million hamsini ni ukosefu wa kazi huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi huwa naheshimu sana uhuru wa mawazo lakini alichoandika huyo jamaa siyo uhuru wa mawazo, kulingana na mazingira yetu. Hayo maneno yangeandikwa kwenye nchi za watu wenye uelewa na wasioamini ushirikina mimi wala nisingeshangaa kwani ni wengi wangemdharau. Lakini maneno haya kwa nchi yetu yenye raia ambao karibu wote tunaamini ushirikina na upeo wetu wa kuchambua mambo ulivyo mdogo ni hatari tena hatari kweli! Tunapoona mambo ya ajabu kama watoto wadogo kuuawa kwa imani za kishirikina yanaanzia mbali. Ujinga kama alioandika huyo jamaa ndiyo unachipua kama mbegu na kuwa miti ya maovu.
 
I'm sure huyo.kijana alikuwa anajiropokea tu bila kuwa na uhakika maana kaingiza had u Freemason bila kujua hao Freemason ni kina nani yeye kujiandikia tu kutoa nyongo yake kupitia njia isiyo sahihi. Though huyo kaandika Facebook ila ndo maneno ya wanajamii wanayoongea kimya kimya. Wangempuuza tu hata Leo tusingeona Uzi jf
Mkuu mimi huwa naheshimu sana uhuru wa mawazo lakini alichoandika huyo jamaa siyo uhuru wa mawazo, kulingana na mazingira yetu. Hayo maneno yangeandikwa kwenye nchi za watu wenye uelewa na wasioamini ushirikina mimi wala nisingeshangaa kwani ni wengi wangemdharau. Lakini maneno haya kwa nchi yetu yenye raia ambao karibu wote tunaamini ushirikina na upeo wetu wa kuchambua mambo ulivyo mdogo ni hatari tena hatari kweli! Tunapoona mambo ya ajabu kama watoto wadogo kuuawa kwa imani za kishirikina yanaanzia mbali. Ujinga kama alioandika huyo jamaa ndiyo unachipua kama mbegu na kuwa miti ya maovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom