Jamhuri yampandisha kizimbani Emmanuel kwa kutoa (Publication) taarifa za uongo kuhusu KICHAA

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,884
Points
2,000

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,884 2,000
Jamhuri imempandisha kizimbani kijana Emmanuel Mahumbi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa ya uongo katika ukurasa wake wa Facebook.

Mahumbi anadaiwa kuwa mnamo September mwaka 2018 aliandika "KICHAA MMOJA ANATOA KAFARA KIBOYA KWELI. KAENDA KUMUONA DADA YAKE BUGANDO KUMBE NDO ANAMKABIDHI KWA FREEMASONS. SIKU MOJA BAADA YA KUMUONA AKAFA. KAENDA UKEREWE SIKU MBILI BAADAE WAKAFA. KUMBE ALIENDA KUWAKABIDHI FREEMASONS. BOYA KWELI LIAMBIENI LIBADILIKE LITAMALIZA WATU"

#MyTake:
Wanasheria hebu tusaidieni kidogo hapa. Hii kesi kwanini imekuwa criminal? Is there any offence against the state? Ni ajabu kuwa anayedaiwa kuchafuliwa ni kichaa halafu mlalamikaji ni Jamhuri. Tangu lini Jamhuri imeanza kutetea vichaa? Kwanini huyo kichaa mwenyewe asilalamike kwa kufungua Libel defamatory charges mahakamani? Kwanini Mahumbi ameshtakiwa kutoa taarifa ya uongo. Ni uongo upi amesema?

Huyo 'kichaa' aliyetajwa na Mahumbi kuwa anatoa kafara kiboya ni nani? Na kwanini Jamhuri imtetee mtu ambaye ni kichaa? Je Jamhuri inaweza kuthibitisha kuwa kichaa huyo hana uhusiano na Freemasons kama Mahumbi alivyodai? Je Jamhuri inaweza kuthibitisha kuwa kichaa huyo sio boya kama ilivyodaiwa?

Naona kama Jamhuri inaenda kushindwa hii kesi mapema sana kwa sababu haiwezi kuprove allegetions dhidi ya Mahumbi (kumbuka the burden of proof rely to the one who allege). ili Jamhuri ishinde inatakiwa ituambie huyo kichaa ni nani. Then ithibitishe kwamba kichaa huyo hana uhusiano na Freemasons. Tatu iweze kuprove kwamba kichaa huyo hatoi kafara kama ilivyoelezwa. Na mwisho ithibitishe kuwa kichaa huyo sio boya. Kesi kama hizi apewe Wakili Peter Kibatala Hekima Mwasipu au Sheck Mfinanga utazimia kwa burudani, jinsi mawakili wa Jamhuri watakavyokua wakiomba maji mahakamani.!


C&P
FB_IMG_1550161252254.jpeg
 

Ambokile Amanzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2018
Messages
459
Points
1,000

Ambokile Amanzi

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2018
459 1,000
afungwe maisha na wengine wenye akili kama yake iwe fundisho maana kuna watu wanajifanya wanatumia maneno ya kuficha huku wakijua na sisi tuna akili timamu
fumbo mfumbie mjinga haya mafumbo watawatokea puani bavicha
Nyamaza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Lyamber

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Messages
9,607
Points
2,000

Lyamber

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2012
9,607 2,000
shida ni muda wa kuletwa kichaa utakuwa umekaa zaid ya mbowe.ndio ujie mdomo hiponza kichwa
Hilo linaeleweka lakini kesi yake hio inadhaminika shida itakuja pale atakapo kiuka masharti ya dhamana na akafutiwa dhamana, zinakuja sarakasi juu ya sarakasi pingamizi juu ya pingamizi
 

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,884
Points
2,000

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,884 2,000
Siku hizi ujinga na upumbavu imekuwa Ni Kama busara.huyo kijana ni mjinga japo hawezi kufungwa kwa kuwa sioni kosa kisheria lakini Ni mjinga na anabakia kuwa mjinga.sisi hatufagilii Mambo ya kijinga.
Ushawahi kusoma caption ya Facebook sehemu ya kuandika status?!?
 

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
4,884
Points
2,000

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
4,884 2,000
afungwe maisha na wengine wenye akili kama yake iwe fundisho maana kuna watu wanajifanya wanatumia maneno ya kuficha huku wakijua na sisi tuna akili timamu
fumbo mfumbie mjinga haya mafumbo watawatokea puani bavicha
Mtajaza magereza but watu hawataacha. Tendeni haki
 

Forum statistics

Threads 1,382,257
Members 526,314
Posts 33,823,311
Top