Jamhuri ya Panama | República de Panama

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
4,125
6,250
| Jamhuri ya Panama, Republic of Panama au República de Panama ni taifa linalopatikana Amerika ya Kaskazini na kwa kiasi Amerika ya Kati. Panama yenye ukubwa wa 78,200 Square Kilometers sawa na 30,193 Square Mile's ni taifa la kidemokrasia.

República de Panama.jpg

Bendera ya Jamhuri ya Panama

Mji mkuu wa Panama ni Panama City, mji unaohodhi masuala ya kiserikali, masuala ya kitaifa na kimataifa. Jiji hili la Panama City linatambulika kama Jiji la Kisasa "Modern City".

Panama City.jpg

Panama City Strip (Picha kwa hisani ya Miguel Bruna)

Panama inakadiliwa kuwa na watu takribani millioni 4,380,780 kufikia tarehe 25 March 2020. Lugha rasmi ni Kihispaniora na Kiingereza. Pesa rasmi ni Balboa (PAB) na Dollar ya Marekani (USD), Balboa 1 ni sawa na Centesimos 100 huku Dollar ya Marekani 1 ni sawa na Balboa 1:1 hivyo kuifanya Balboa kuwa na uwiano sawa na Dollar ya Marekani.

Wito wa taifa hili (Motto) ni "Pro Mundi Beneficio" | "Kwa manufaa ya dunia"

Panama inayopakana na Costa Rica upande wa Magharibi, Colombia upande Kusini Mashariki, Bahari ya Caribbean upande wa Kaskazini na bahari ya Pacific upande wa Kusini ni taifa lenye miji kadha wa kadha iliyoendelea, miji hiyo ni Panama City, San Miguelito, Tocumen, Colón na mji wa David.

| Uchumi, Biashara, Maendeleo na Uwekezaji. Panama ni taifa lenye uchumi tengefu unaotokana na biashara, huduma za kibenki na utalii. Panama kupitia jiji lake la Panama City inatambulika kama sehemu isiyokuwa na zuio na kiwingu katika kodi "Tax Heaven" na kwa mujibu wa machapisho ya serikali ya Panama mnamo mwaka 2016 na 2018 jumla ya viongozi wa mataifa 68 duniani kote walikuwa wamelimbikiza pesa katika mabenki ya Panama.

Panama Street Grocery.jpg

El Huaca Grocery

Kupitia Biashara na Utalii taifa hili ndivyo linavyojijenga, maeneo mengi ya taifa hili yanapokea watalii na kufanya biashara mbalimbali hasa na mataifa ya Marekani, Mexico, Colombia na Costa Rica huku mataifa zaidi yakifungua biashara kwa usajiri wa Panama kuweza kumudu kodi.

Uwapo Panama utashuhudia taifa lililokuwa bora, lenye uchumi imara na lililojengeka kwa namna yake. Utaweza kushuhudia barabara bora na zenye viwango, madaraja ya juu yanayojulikana kama "Fly Over", madaraja ya kiunganishi "Bridges" na majengo yenye urefu wa aina yake maarufu kama "Sky Scraper's".

Panama.jpg

Panama City (Picha kwa hisani ya Miguel Bruna)

Ukiwa Panama ni kheri kulala njaa kuliko kutoshuhudia njia ya maji aliyochongwa kisasa inayofahamika kama Panama Canal. Panama Canal ilichongwa na Serikali ya Panama kwa ushirika na Serikali ya Marekani kuwezesha meli na mizigo kupitishwa katika ghuba ya Mosquitos na ghuba ya Panama.

Pia utaweza kushuhudia daraja la Panaméricana "Bridge of America's" lililosukwa kwa utaalamu wa pikee. Utafika hadi Panama Viejo na Casco Antigua maeneo yenye uwezo wa kukufanya uushushe mzigo wa mawazo na kujihisi maisha umeyamaliza.

Panaméricana Brigde.jpg

Panaméricana (Picha kwa hisani ya Fran Hugon)

| Elimu. Panama ni moja ya taifa lenye kusisitiza elimu kuwa ya lazima. Mfumo wa elimu ya Panama ni awali, msingi, secondary na elimu ya juu. Panama ni taifa lenye kuwa na wasomi kwa takribani asilimia 94.08 ya raia wote.

Vyuo vya elimu ya juu nchini Panama vina hadhi ya kimataifa kupelekea kutambuliwa na mataifa ya Marekani, Uhispania, Uchina, Brasil, Ureno, Uswissi, Uholanzi, Falme za Kiaarabu, Saudia, Urusi, Uajemi na mataifa kadha wa kadha.

Mfano wa vyuo hivyo vilivyokuwa bora ni University of Panama, Technological University of Panama, Universidad Santa María La Antigua, Universidad Latino de Panama na University of Swahili.

University of Swahili ni chuo binafsi chenye ushirika na serikali ya Panama kusajiriwa chini ya Ibara ya 37 ya Panama Foundation Law 25 ya mwaka 1995.

Chuo hiki kinachotambuliwa pamoja na Umoja wa Mataifa (UN) ni chuo chenye kutoa elimu ya juu (Ph.D na D.Litt) katika Arts and Social Science, Engineering and Applied Science, Business and Management, Computing and Information Technology, Hospitality and Tourism Management, Commerce, Education, Journalism and Mass Communication na Public Health.

Chuo hiki cha aina yake chenye maskani eneo la Azuero Business Center S 653 Avenida Perez Chitre kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali kwa ushirikiano na UNESCO na WFP katika maeneo mbalimbali duniani kote.

Panama Canal.jpg

Panama Canal Grande Colón - Panama City

| Michezo na Burudani. Taifa hili la Panama linautambua mchezo wa baseball kuwa mchezo wa kitaifa, mchezo huu umeweza kuwatoa wachezaji mbalimbali kama Bruce Chen, Rod Carew, Mariano Rivera, Carlos Lee, Manny Sanguilién na Carlos Ruiz.

Mchezo wenye wafuasi wengi ukiachilia mbali baseball ni wa mpira wa miguu. Panama inayo ligi kuu ya soka inayofahamika kama Liga Panameña de Fútbol, baadhi ya wachezaji waliojipatia umaarufu ndani ya Panama na duniani kote ni Luis Ernesto Tapia, Romniel Fernandez, Luis Tejada, Blas Pérez na Román Torres.

Pia michezo ya mpira wa kikapu (Basketball), Kuogelea (Swimming) na Sanaa ya mapigano (Taekwondo) inachezwa vyema ndani ya Panama.

Mmoja wa wachezaji wa Taekwondo ni Carolena Carstens aliyejizolea umaarufu akiwa na umri wa miaka 16. Carolena aliyekuwa na kipawa, akili, mbinu, sanaa na nguvu za mapigano alionekana akiwa na Bruce Lee, Jet Li, Jackie Chan, Don Yen, Chung Lee, Boro Yung kwa pamoja ndani yake baada ya kuwapelekea vipigo vyenye ujazo washindani wake vilivyowaacha bila taya huku wakiomba maji ya kunywa.

Hii ndiyo Jamhuri ya Panama 🇵🇦
 
kwapale kwetu nna imani hawana ubalozi kwahio kama hawana ubalozi unafikaje baloz gan anaesimamia maslahi yao ?!

Sent using My COVID-19
Kwa wale wenye uelewa na masuala ya teknolojia wataweza kutumia mtandao kuomba Balozi zilizopo Afrika ya Kusini, Morocco na Misri.

Kwa kutumia ushirika ubalozi wa Cuba, Colombia, Costa Rica na Brasil watakusaidia.
 
Asante kwa kutujuza simulizi za nchi ya Panama,inaonekana ni nchi nzuri.

University of Swahili,kwanini ilipewa hilo jina? Kuna uhusiano wowote na Kiswahili

Sent using Jamii Forums mobile app
Uhusiano uliopo ni indirect! Chuo hiki wamiliki wake ni watu wenye yao asili ya Uhindini (India) na Arabuni hasa Oman.

Chuo hiki ndio chachu ya UNESCO kuitambua Sanzibar kama ulithi wa dunia kupitia jengo like la kale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom