Chama cha Maigizo (CCM)

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
943
1,989
Nchi ya panama ipo gizani
Umeme ni mgawo kila siku.

Sababu ya mgawo hailezwi kinaga ubaga, nchi hii nani kawaroga viongozi wake?

Chama cha Maigizo ndiyo chama tawala toka Enzi na Enzi, kila siku wimbo ni ule ule, mbio zetu toka uhuru Hadi hapa tulipo.

Kiongozi wa nchi hii wala huelewi ana dira gani? Ana falsafa ipi? Ana maono gani? Anamwelekeo Gani? Ana Nia Gani? Ana mpango gani na ana mkakati upi? Wala huelewi.

Ziara zake wala huelewi hasa kama huwa zinaandaliwa au niza zimamoto? Hutamani hata kusikiliza, kwasababu kama upo na akili Sawa kichwani hutaelewa kama anahutubia taifa au familia.

Tazama panama ilivyojaaliwa. Ina kila kitu ambacho nchi inapaswa kuwa navyo lakini ndiyo nchi masikini ukanda wa Amerika kusini.

Mapambio ni mengi, RUSHWA imeshamiri, ufisadi umetaradadi, kiburi kimezidi na huduma za kijamii zimedoda.

Mwenyekiti wa chama yupo tu, analinda watu wake anawabadilisha tu sehemu za kazi badala ya kuwaondoa kabisa katika utumishi.

Panama inakwenda wapi? Kwanini nchi hii inataka kuwa nchi masikini ya kudumu?

Kuna wakati mwelekeo ulianza kuonekana na wananchi wakawa na Imani kubwa lakini ghafla inaporomoka kwa Kasi.

Mchwa Wana ila kila mahali. Mvuto unapotea,kiongozi mkuu hapendwi,analinda kikundi cha wazandiki. Anaongoza nchi bila ya yeye kuwa na dhamira,anaendesha nchi kwa style ya Bora liende watajua wenyewe.

Kwasasa panama wanyonge hawasikilizwi wanaswagwa kama punda. Wakitoa kero zao wanaambiwa zipelekeni kwa mbunge tutazishughulikia.

Mbunge yupi? Wabunge wa panama ni wapiga makofi tu.
Panama Jama? Chama cha maigizo kipo kwa kazi, ukiangalia huku akina mama wagalagala chini kushukru ujio wa kiongozi akina mama hao hao wananuka Shida.

Ukiangalia kule maandamano ya kumpongeza anaupiga mwingi, mara mipasho ya taarabu. Jama panama.

Sasa ni saa 2241 usiku hapa kijijini kwangu hakuna umeme. Lakini kwao upo muda wote.
Viongozi na chama cha maigizo nchini panama mnatia aibu kubwa na hamfai hata kidogo. Nchi mnaila Hadi inabaki mifupa.. wananchi wa panama mnawaona nyani.

Lakini niwaambie tu enyi viongozi ujanja wenu ni leo tu kaburi linawangoja. Ngoja muwadharau leo Wana panama.

Waishi kama nyani,mkiwahadaa kwa ukosefu wa elimu lakini mtapita na mtasahaulika lakini panama itabaki.

2025 Wana panama kataa wahuni. Inawezekana kabisa chama cha maigizo kuondoka.
 
Hujasema bado, haijasikika... Utasema

Chama cha...Maig....

Cheo cha Katibu mwenezi walikifuta?

Mbona hakuna mtu anajitokeza kujibu hoja...kama enzi za Anopheles aka 'Kataa Wahuni'...
 
Nchi hiyo ya PANAMA ni ya pekee ...

Haikufinyangwa kwa kuigwa mataifa mengine....

Ni taifa teule lenye njia zake....

Kutofanana na nyingine ndio UTUKUFU wake ,utulivu na usalama wake......

Ni taifa ambalo linalindwa na mizimu ya kule Bagamoyo.....kwenda kinyume na CCM ni kwenda kinyume na mizimu hiyo.....

Wewe kubali tu uwe chini yake...

Huna budi kutii hilo....

Ukileta ubishi ujue HUTOFANIKISHA ya huo ubishi wako......

#SiempreCCM
 
Nchi ya panama ipo gizani
Umeme ni mgawo kila siku.

Sababu ya mgawo hailezwi kinaga ubaga, nchi hii nani kawaroga viongozi wake?

Chama cha Maigizo ndiyo chama tawala toka Enzi na Enzi, kila siku wimbo ni ule ule, mbio zetu toka uhuru Hadi hapa tulipo.

Kiongozi wa nchi hii wala huelewi ana dira gani? Ana falsafa ipi? Ana maono gani? Anamwelekeo Gani? Ana Nia Gani? Ana mpango gani na ana mkakati upi? Wala huelewi.

Ziara zake wala huelewi hasa kama huwa zinaandaliwa au niza zimamoto? Hutamani hata kusikiliza, kwasababu kama upo na akili Sawa kichwani hutaelewa kama anahutubia taifa au familia.

Tazama panama ilivyojaaliwa. Ina kila kitu ambacho nchi inapaswa kuwa navyo lakini ndiyo nchi masikini ukanda wa Amerika kusini.

Mapambio ni mengi, RUSHWA imeshamiri, ufisadi umetaradadi, kiburi kimezidi na huduma za kijamii zimedoda.

Mwenyekiti wa chama yupo tu, analinda watu wake anawabadilisha tu sehemu za kazi badala ya kuwaondoa kabisa katika utumishi.

Panama inakwenda wapi? Kwanini nchi hii inataka kuwa nchi masikini ya kudumu?

Kuna wakati mwelekeo ulianza kuonekana na wananchi wakawa na Imani kubwa lakini ghafla inaporomoka kwa Kasi.

Mchwa Wana ila kila mahali. Mvuto unapotea,kiongozi mkuu hapendwi,analinda kikundi cha wazandiki. Anaongoza nchi bila ya yeye kuwa na dhamira,anaendesha nchi kwa style ya Bora liende watajua wenyewe.

Kwasasa panama wanyonge hawasikilizwi wanaswagwa kama punda. Wakitoa kero zao wanaambiwa zipelekeni kwa mbunge tutazishughulikia.

Mbunge yupi? Wabunge wa panama ni wapiga makofi tu.
Panama Jama? Chama cha maigizo kipo kwa kazi, ukiangalia huku akina mama wagalagala chini kushukru ujio wa kiongozi akina mama hao hao wananuka Shida.

Ukiangalia kule maandamano ya kumpongeza anaupiga mwingi, mara mipasho ya taarabu. Jama panama.

Sasa ni saa 2241 usiku hapa kijijini kwangu hakuna umeme. Lakini kwao upo muda wote.
Viongozi na chama cha maigizo nchini panama mnatia aibu kubwa na hamfai hata kidogo. Nchi mnaila Hadi inabaki mifupa.. wananchi wa panama mnawaona nyani.

Lakini niwaambie tu enyi viongozi ujanja wenu ni leo tu kaburi linawangoja. Ngoja muwadharau leo Wana panama.

Waishi kama nyani,mkiwahadaa kwa ukosefu wa elimu lakini mtapita na mtasahaulika lakini panama itabaki.

2025 Wana panama kataa wahuni. Inawezekana kabisa chama cha maigizo kuondoka.
thatha ndio humehandika nini?
Hau humetumwa hau humehagithwa?
unamkathirikia nani thatha!
Ntu nthima hoviyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom