isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,125
- 6,250
Jamhuri ya Mashariki ya Uruguay, República Oriental del Uruguay, Oriental Republic of Uruguay au República Oriental do Uruguai
Uruguay ni taifa linalopatikana bara la Amerika Kusini likiwa na mipaka na Ajentina, Brasil na rasi ya Rio de la Plata ndani ya bahari ya Atlantiki.
Bendera ya Jamhuri ya Mashariki ya Uruguay
Taifa hili lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 176,220 sawa na maili za mraba 68,039 ni nyumbani kwa watu takribani millioni 3,473,733 kufikia Julai 21, 2020.
Kauli kuu ya taifa (Motto) ni “Uhuru au Kifo” | “Libertad o Muerte”. Lugha rasmi ni Kihispaniola, pia Kireno ikiwa lugha ya pili kuwa na wazungumzaji wengi. Pesa rasmi ni Peso ya KiUruguay, peso 1 ni sawa na Centesimos 100.
Jijini Montevideo ©Back Parkers
Mji mkuu wa Uruguay ni Montevideo mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali, biashara na mji wenye maendeleo zaidi ndani ya Uruguay ukiwa umepakana zaidi na mji mkuu wa Ajentina, Buenos Aires.
Miji mingine bora na yenye maendeleo zaidi ni Salto, Tocuarembó, Artigas, Minas, Melo, Rivera, Durazno, Mercedes na Colonia del Sacramento.
Mto Uruguay ©Back Parkers
Uruguay kama taifa ni nyumbani kwa Mto Uruguay, chimbuko kwa jina la taifa "Jamhuri ya Mashariki ya Uruguay" kutokana na mto kuegemea zaidi upande wa magharibi huku taifa likiwa upande wa mashariki.
Taifa hili namba moja katika uhuru wa vyombo vya habari, taifa lenye mrengo wa demokrasia na taifa la kwanza dunia kuhalalisha matumizi ya bangi. Kama taifa ni huru kwa yeyote kulima, kuchakata, kuuza au kuvuta bangi, likiwa na watumiaji asilimia 17 ya raia.
Mkulima akitazamia bangi ©Tangol
Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Kilimo, Maendeleo na Utalii
Uruguay taifa lenye kipato cha juu na kipato cha kati, likiwa taifa lenye kuzalisha asilimia 95 ya umeme wote kwa kutumia Hydroelectric Plants na Wind Parks.
Taifa linao ushirika mkubwa na mataifa ya Ajentina, Brasil na Marekani katika nyanja za ulinzi na usalama, sayansi, teknolojia, nishati, usafirishaji na uvuvi.
Bangi ya Uruguay ikifungashwa ©UruguayFarms
Kinara kwa uuzaji bangi kimataifa kupitia masoko yenye kulenga tafiti na utengenezaji wa dawa. Bangi uchangia asilimia 12 ya pato la taifa nyuma ya nyama zilizosindikwa, maharage ya soya, ngozi na vitambaa.
Taifa limevutia zaidi uwekezaji katika viwanda vya chakula na vinywaji, saruji, vitambaa na mavazi pia magari chapa KIA Motors, General Motors, Ford, Fiat na Peugeot - Citroën.
Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ndio kiungo muhimu katika uchumi na ajira ndani ya Uruguay yenye kutegemea ufugaji wa ng'ombe, kondoo na farasi katika uzalishaji nyama na maziwa, kilimo cha bangi, matunda na mboga, mchele, maharage ya soya na ngano.
Uvunaji wa maharage ya soya ©UruguayFarms
Maendeleo kwa taifa ni kipimo cha maisha bora na yenye tija, uchumi imara yaliyochangamana na uwepo wa miundombinu bora ya usafirishaji, makazi bora, viwanja vya ndege mfano wa, Carrasco International Airport na Punta del Este Int. Airport.
Usafirishaji mkuu unaonganisha mikoa ni uwepo wa mabasi yafanyayo safari za ndani na nje kwa kuunganisha maeneo 17 ndani ya Brazil, 12 ya Ajentina na miji mikuu ya Chile na Paraguái.
Montevideo Peatonal ©Tangol
Utalii huchagizwa na maeneo ya Punta del Este, Rio Negro, Laguna Merin, Ziwa Mirim na Mto Uruguay.
Elimu na Afya
Mfumo wa elimu ndani ya taifa ni bila malipo kwa viwango vya elimu ya awali, msingi na upili huku kiwango cha elimu kwa taifa ikiwa ni asilimia 95.
Uruguay ndio taifa la kwanza kutoa kompyuta mpakato (Laptop) kwa kila mwanafunzi na mwalimu wa shule ya msingi na upili.
Chuo cha ORT ©Tangol
Vyuo bora vyenye kutoa elimu ya juu ni Universidad de Montevideo, Universidad de la República, Universidad ORT Uruguay na Universidad de la Empresa.
Michezo, Sanaa na Muziki
Michezo kwa taifa ni yenye historia, na historia ni Uruguay kuwa taifa la kwanza kuandaa michuano ya kombe la dunia. Fainali zilizochezwa katika uwanja wa Estadio Centanario.
Uruguay mshindi wa kombe la dunia mara mbili, nyumbani kwa wachezaji nguli Alvaro Recoba, Emo Francescoli, Diego Forlan, Luís Suàrez, Fernando Muslera, Edinson Cavani, Diego Godin, Christian Stuani, Martin Cáceres, Jose Gimenez na Lucas Torreira.
Lucas Torreira © Stuart McFarlane X Arsenal
Kupitia filamu Uruguay imezitambulisha Whisky na Los días con Ana kimataifa na waongozaji Juan Pablo Rebella, Pablo Stoll na Ana Diez. Huku muziki ukitambulishwa na Jorge Drexler, Malens Muyala na Omár Rubén Rada.
Hii ndio Uruguay 🇺🇾