Vita ilianza tu baada ya uhuru ,Wareno waliwapa MPLA uhuru kichinichini kwa maslahi yao binafsi bila kuwajulisha UNITA,.MPLA hawakutaka Demokrasia kwa sababu walijua wakiingia kwenye uchaguzi hawawezi kuwashinda UNITA,wakapewa tafu na Soviet,Cuba, China na wapambe wengine wa kisocialist wakawapa support ,wakaamua kutangaza Nchi ni ya chama kimoja,UNITA wakapewa kichapo cha mbwa koko wakaishia maporini huko,Baadaye makaburu,USA na wapambe wa kicapitalist wakampa tafu ya vifaa na intelligence,manpower kwa UNITA haikuwa tatizo mdogomdogo wakaibuka wakaushikilia mji wa pili kwa ukubwa Uhambo,Castro na wapambe zake akaona isiwe tabu akatuma mtu za kutosha,kwanza alitanguliza wanajeshi weusi kukwepa kujulikana,CIA agent mmoja akiwa hotelini jijini Luanda alishtushwa baada ya kuona kuna weusi walioshiba mia kadhaa wakipepesapepesa macho lakini wanaongea kihispania na si kireno baadaye akaja kugundua ni wacuba kukawa hamna siri tena na Castro akautangazia ulimwengu kuwa atazipiga na mabepari kokote pale duniani.Tanzania na sisi tulitoa support kwa MPLA japokuwa kichinichini sana.