James Rugemalira kuzishtaki taasisi zilizoiibia Serikali

Ajabu kuna watu humu ht kusoma hii habari wakaelewa hawajaisoma wamekurupuka ku comment mara Mwendazake kaitia hasara inchi, mara apewe bandari mara anaidai serikali...JF imekua na watu wa hovyo sana now days, ht km ni Uhuru wa mawazo huu hapana aisee...
and this is a reflection ya jinsi information warlfare ilivyo ngumu..mtu anaweza kufanya character assasination na mijitu ya hovyo yakarukia habari ki ushabiki shabiki bila ku verify habari husika
Mtanzania ametanguliza mahaba kabla ya ufahamu....

Watanzania hawasomi habari wakaelewa bali wanasoma habari ili wapate Cha kujibu huku wakiwa Wana majibu yao kichwani........
 
Et tirioni ngapi?...68 tunalipa madeni yote tangu Uhuru! Alisikika jamaa mmoja pale Waitihausi!
Baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miaka minne kabla hajaachiwa hivi karibuni, hatimaye mfanyabiashara maarufu nchini, James Rugemalira ameanza harakati za kuzishtaki kampuni na taasisi za fedha anazozituhumu kuhusika katika wizi wa fedha za Serikali zilizomsababishia kesi ya uhujumu uchumi.

Katika kutimiza azma yake hiyo, Rugemalira amewasilisha maombi ya kibali cha kufungua na kuendesha mashtaka hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya kampuni na taasisi hizo kama mwendesha mashtaka binafsi.

Mfanyabiashara huyo aliyekaa ndani kwa miaka minne na miezi mitatu, ameachukua hatua hiyo ukiwa ni mwezi mmoja na nusu tangu alipotoka mahabusu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kumfutia mashtaka yaliyokuwa yakimkabili yeye na wenzake watatu, Septemba 16.

Katika mchakato huo Rugemalira ambaye ni mmliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, amefungua maombi hayo dhidi ya watuhumiwa 11 zikiwamo taasisi za fedha na watu binafasi ambao anawatuhumu kuisababishia Serikali hasara ya Sh 61 trilioni.

View attachment 1996474

Maombi hayo tayari yamepangwa kusikilizwa mahakamani hapo Novemba 10 mwaka huu, na pande zote yaani waombaji (Rugemalira na kampuni yake ya VIP Engineering) na wajibu maombi wote wametakiwa kufika siku hiyo kwa ajili ya kuyasikiliza maombi hayo.

Wajibu maombi hao ambao Rugemalira anawatuhumu ni Benki ya Standard Chartered (Hong Kong), Benki ya Standard Chartered Tanzania, Benki ya Standard Chartered (Malaysia) Berhad, Wartsila Netherlands B.V na Wartsila Tanzania Limited.

Wengine ni Sanjay Rughani ambaye kwa sasa ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Samir Subbrwai ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered (Hong Kong), Abrar Anwai ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered (Malyasia) Berhad.

Vilevile wamo Bill Winters, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered na Hakan Agnevall ambaye ni Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wartsila Corporation.

Katika hati ya kiapo kinachounga mkono maombi hayo, Rugemalira anayejitambulisha kama mshauri binafsi wa kimataifa wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na mwanahisa mkuu wa VIP Engineering and Marketin Limited, anaanza kwa kutoa historia ya sakata hilo.

Anadai mwaka 2005 baada ya IPTL kufunga shauri lililokuwa limeanza tangu Februari 25 mwaka 2002, Benki ya Standard Chartered (SCB) kupitia kampuni tanzu yake, Benki ya Standard Chartered (Hong Kong) na Danaharta (SBCHK) walikusudia kuandaa mkataba wa makubaliano na, uuzaji na ununuzi wa IPTL.

Hata hivyo, Rugemalira anaituhumu Kampuni ya Mechmar ambayo ilikuwa mbia mkuu wa IPTL kula njama na SCB kukwepa kulipa dola 4.2 milioni za Marekani ambazo ni asilimia nne ya ushuru wa forodha katika mkopo wa IPTL wa dola 105 milioni wa Juni 28 mwaka 1997.

Rugemalira anadai katika kiapo chake kuwa kukwepa malipo hayo ni kosa la jinai chini ya Kifungu cha 73(2)(a) cha Sheria ya Ushuru wa Forodha iliyorekebishwa mwaka 2019.

Pamoja na makosa mengine aliyoyaainisha, Rugemalira anadai maombi hayo yanakusudia kurejesha Sh61 trilioni ambazo Standard Chartered Bank Group na washirika wake walifanya ulaghai kuchepusha fedha hizo kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na VIP Engineering isivyo halali.

Rugemalira na mwenzake Harbinder Singh Seth, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu Juni 19, mwaka 2017 wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa na mashtaka 12 kabla ya kuongezwa aliyekuwa mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege.

Kesi hiyo ilitokana na kashfa ya uchotaji wa mabilioni ya pesa katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu kutokana na mgogoro wa malipo ya gharama za uwekezaji kati ya IPTL na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililopinga malipo hayo kuwa yalikuwa makubwa.

Akaunti hiyo ilifunguliwa kwa pamoja na pande hizo mbili kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo hayo kusubiri utatuzi wa m
 
Kwani wewe ujui kiswahili ni lugha mbovu sana bado sasa Rais ndiyo kitu gani kwenye sarufi za kiswahili tatizo tunatabia ya kujiona wasomi kwa kushikamana na makosa ....lugha sahihi ni RAISI SIYO RAIS
Mfano maeno KAZI RAHISI huwezi kusema KAZI RAHIS kiswahili hakina mtindo huo, sema wasomi feki tulio nao ndiyo wamesababisha neno Raisi liwe kosa wakati ndiyo neno sahihi
Tetetete Bashite kwenye ubora wako
 
Nafikiria tu, mfano mzee akavuna hizo 61 trillioni anazowadai hao wachepushaji, serikali itazichukua au na yale madhila waliyomfanyia ndio watatoa kidogo hapo wamlipe fidie.
 
Huyu Mzee anajua mambo mengi sana ambayo serikali haiyajui ama imeyafumbia macho makusudi..

Kwa hii kesi ndio utajua hii nchi inaliwa kwa namna gani

Kikwete kuna maswali inabidi atusaidie kujibu hapa.
Zoezi lilianza 2002 huko,JK akusaidie nini?Y usimfufue Ben ndiyo akusaidie!.
 
Huyu Mzee anajua mambo mengi sana ambayo serikali haiyajui ama imeyafumbia macho makusudi..

Kwa hii kesi ndio utajua hii nchi inaliwa kwa namna gani

Kikwete kuna maswali inabidi atusaidie kujibu hapa.
Kikwete akikujibu unitag pleaze
 
Mwendazake ni mleta hasara tu kwa nchi.

- Alikamata meli ya kigeni,mwisho wa kesi nchi ikalipa wageni,

- Akahonga nyumba za serikali kwa washikaji na concubines,serikali ikala hasara,

- Ujenzi wa "mabharabhara" na ununuzi wa "vivukio" ukafanywa kimagumashi,serikali ikalipa na kula hasara,

- Kawasotesha "watu" bila hata hatia,wanaidai serikali.Italipa na kuleta hasara/mahasara.Yuleee,akajitorokea aibu!
Kalia dole la kati soma uelewe sio kilakitu unamuangushia jumba bovu magufuli.
 
Hapa nilimaanisha endapo ukwapuaji huu unahusisha baadhi ya vigogo wa serikali, kuna uwezekano mkubwa hii kesi ikapotezewa. Yetu macho.
Eeh hilo nalo neno! Kama kuna 10% zilishapitaga hapo kesi hamna
 
Homa ya Magufuli haitaisha sasa hivi.
Kesi za huyo mzee got none to do with Magu ila Kikwete...

Meza vidonge mkuu ..
Mwendazake ni mleta hasara tu kwa nchi.

- Alikamata meli ya kigeni,mwisho wa kesi nchi ikalipa wageni,

- Akahonga nyumba za serikali kwa washikaji na concubines,serikali ikala hasara,

- Ujenzi wa "mabharabhara" na ununuzi wa "vivukio" ukafanywa kimagumashi,serikali ikalipa na kula hasara,

- Kawasotesha "watu" bila hata hatia,wanaidai serikali.Italipa na kuleta hasara/mahasara.Yuleee,akajitorokea aibu!
 
mhaya yoyote huwa anapenda kesi kuliko kitu kingine kwao kuwa na kesi ni sifa sana mnaweza mkakaa mahakamani miaka yeye hachoki na kesi
 
Back
Top Bottom