Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA James Mbowe ameeleza kuwa Kitendo cha Chadema kukaa kimya kwa siku takribani saba tangu kushambuliwa kwa Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa Chadema BAWACHA Bi. Sigrada Mligo, sio kitendo cha kiungwana, akikosoa pia taarifa ya Chadema Taifa ya leo Machi 31, 2025 kushindwa kuwakemea aliowaita "wahuni" waliompiga Mwenezi huyo akiwa Mkoani Njombe.
Shambulio la kudhuru mwili alilolipata Katibu Mwenezi wa Bawacha lilitokea Machi 25, 2025 wakati wa kikao cha ndani cha Viongozi wa Kitaifa wa Chadema, waliokuwa wakikutana Mkoani Njombe chini ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, John Heche, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara za kueneza kuhusu vuguvugu la No Reforms, no Election.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Soma Pia: Ghasia Ndani ya CHADEMA: Mwenezi wa BAWACHA Taifa ashambuliwa na Walinzi wa Heche
"Tukio alilofanyiwa Mwenezi wa Bawacha Taifa Sigrada Mligo sio la kiungwana wala kibinadamu. Kitendo cha Chama kukaa kimya na leo ndiyo wanakuja na barua badala ya kukemea wahuni waliompiga Sigrada na kuwachukulia hatua wanasema wanachunguza kama ni kweli. Swali langu ni kwanini Hawajalaani tukio hili? Siyo Chama wala Bawacha Taifa? Umuhimu wa kuandika barua umekuja baada ya CCM kuonesha ubinadamu wao kwa Sigrada?" Ameandika Mbowe.
Kauli ya James Mbowe imekuja saa chache mara baada ya andiko lingine la aliyekuwa Mkurugenzi wa mawasiliano wa Chadema, John Mrema kueleza kusikitishwa na ukimya wa Chadema, Akilaani namna ambavyo Chama hicho kimekuwa kikimtisha Mwenezi huyo wa Bawacha.
"Chama hakikuona haja ya kulaani tukio la kiongozi wa wanawake taifa kupigwa na kuumizwa ,kipigo kilichotolewa na Mwanaume,bali kinasema ni taarifa zinazosambazwa mtandaoni. Chama hakikutoa pole kwa mgonjwa ,mbona kinatoa pole hata kwa viongozi wa CCM wanapopatwa na majanga ? Huu uadui wa kushindwa kumpa pole kiongozi umeanza lini?Chama kinamtishia mgonjwa na kumpangia nani wakumpa faraja na nani hatakiwi kwenda kumpa faraja." Ameandika John Mrema.