James Mbatia aamua kufuta kesi dhidi ya Halima Mdee

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,194
Hizi ni siasa za maji taka, leo Mbatia kafuta kesi dhidi ya Mdee.

Source: East Afrika radio saa 10 jioni

================================

Na Peter Mwenda

CHAMA cha NCCR-Mageuzi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), vimekubaliana kufutwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Kawe, Dar es Salaam. Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, dhidi ya mbunge wa sasa kwa tiketi ya CHADEMA, Bi.Halima Mdee.

Muafaka huo ulitangazwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt.Willibrod Slaa na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Bw.Samwel Ruhuza. Wakizungumza na waandishi wa habari, viongozi hao walisema kesi hiyo namba 100/2010 imefutwa rasmi jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo walalamikaji na walalamikiwa, waliweka saini zao na kila upande utabeba gharama zake.

Dkt.Slaa alisema, CHADEMA imefurahishwa na uamuzi wa chama hicho kukubali kufuta kesi hiyo bila kutaka gharama yoyote waliyoitumia kufungua shauri hilo. "Uamuzi huu umetokana na mapenzi ya vyama hivi kujali maslahi ya Watanzania zaidi kuliko ya chama, makubaliano ya kufuta kesi hii ni historia kubwa na ya kwanza kufanyika nchini," alisema.

Aliongeza kuwa, lengo la vyama vya upinzani ni kuiondoa CCM madarakani hivyo makubaliano hayo ni ushindi dhidi ya ubinafsi ambao wapinzani wakiruhusu makundi, hakutakuwa na mafanikio ya kuleta mabadiliko nchini. Alisema Bi.Mdee hakuwepo katika muafaka huo kwa sababu yupo bungeni lakini amewakilishwa na mawakili wake. Akijibu hoja kwanini wasiwasamehe madiwani waliowafukuza mjini Arusha, Dkt.Slaa alisema, kesi ya madiwani hao inatokana na kosa la kinidhamu ambapo CHADEMA haiwezi kuruhusu uvunjwaji katiba ambayo wamekubaliana kuifuata.

"Hoja iliyopo bungeni kwa sasa ni kupata Katiba Mpya, naomba Watanzania wajiandae kutoa maoni yao bila woga, hoja ya wabunge kuongezwa posho kwa kazi ya kukaa bungeni hailingani na kazi ya madaktari waliogoma wakidai posho zaidi," alisema.

Bw. Mbatia katika kesi hiyo, alikuwa akiwakilishwa na wakili Bw.Mohammed Tibanyendera, kutoka Kampuni ya Star Chambers Advocates ambapo Bi.Mdee, alikuwa akiwakilishwa na wakili Bw.Mabere Marando na Bw.Edson Mbogoro ambao wote walikuwepo katika mkutano huo.

CHANZO: Majira
 
Kupitia EAst Africa Radio, Chadema kupitia Dr. Slaa na NCCR Mageuzi kupitia Sam Ruhuza wametangaza kuanza ukurasa mpya wa mashirikiano na hivyo kuamua KUFUTA kesi kati ya Mbatia na Halima Mdee katika jimbo la Kawe.

Kwangu mimi naona hatua hiyo ni kudumaza demokrasia, Chadema baada ya kuona mwelekeo wa kesi unakula kwao wameona ni vizuri kuwapigia magoti NCCR ili wasije katwa ruzuku. Ukweli hizo ni siasa za majitaka
 
Kama mkazi wa Kawe hiyo kesi nitaivalia njuga; sijui sheria inasemaje?
 
kupitia east africa radio, chadema kupitia dr. Slaa na nccr mageuzi kupitia sam ruhuza wametangaza kuanza ukurasa mpya wa mashirikiano na hivyo kuamua kufuta kesi kati ya mbatia na halima mdee katika jimbo la kawe.

Kwangu mimi naona hatua hiyo ni kudumaza demokrasia, chadema baada ya kuona mwelekeo wa kesi unakula kwao wameona ni vizuri kuwapigia magoti nccr ili wasije katwa ruzuku. Ukweli hizo ni siasa za majitaka

crap!!!
 
Kupitia EAst Africa Radio, Chadema kupitia Dr. Slaa na NCCR Mageuzi kupitia Sam Ruhuza wametangaza kuanza ukurasa mpya wa mashirikiano na hivyo kuamua KUFUTA kesi kati ya Mbatia na Halima Mdee katika jimbo la Kawe.

Kwangu mimi naona hatua hiyo ni kudumaza demokrasia, Chadema baada ya kuona mwelekeo wa kesi unakula kwao wameona ni vizuri kuwapigia magoti NCCR ili wasije katwa ruzuku. Ukweli hizo ni siasa za majitaka

hujajenga hoja bado, rudi kasome
 
Tbc habari ya leo sa10 kamili jioni wametangaza ivo,nadhani siasa zimeanza kueleweka maana siasa si kukomoana,hongera mbatia...pia nadhani itakuwa njia sahihi mbatia ukimsamehe kafulila kwa kuwa ndo kilikuwa kilio chake kikubwa!
 
Kupitia EAst Africa Radio, Chadema kupitia Dr. Slaa na NCCR Mageuzi kupitia Sam Ruhuza wametangaza kuanza ukurasa mpya wa mashirikiano na hivyo kuamua KUFUTA kesi kati ya Mbatia na Halima Mdee katika jimbo la Kawe.

Kwangu mimi naona hatua hiyo ni kudumaza demokrasia, Chadema baada ya kuona mwelekeo wa kesi unakula kwao wameona ni vizuri kuwapigia magoti NCCR ili wasije katwa ruzuku. Ukweli hizo ni siasa za majitaka
umeshauriwa ukainunue
 
Kupitia EAst Africa Radio, Chadema kupitia Dr. Slaa na NCCR Mageuzi kupitia Sam Ruhuza wametangaza kuanza ukurasa mpya wa mashirikiano na hivyo kuamua KUFUTA kesi kati ya Mbatia na Halima Mdee katika jimbo la Kawe. Kwangu mimi naona hatua hiyo ni kudumaza demokrasia, Chadema baada ya kuona mwelekeo wa kesi unakula kwao wameona ni vizuri kuwapigia magoti NCCR ili wasije katwa ruzuku. Ukweli hizo ni siasa za majitaka
mbatia anavyopenda umwinyi akubali kufuta kesi aliyokua anaelekea kushinda? sidhani labda uniambie alikua anaelekea kushindwa.
 
Kupitia EAst Africa Radio, Chadema kupitia Dr. Slaa na NCCR Mageuzi kupitia Sam Ruhuza wametangaza kuanza ukurasa mpya wa mashirikiano na hivyo kuamua KUFUTA kesi kati ya Mbatia na Halima Mdee katika jimbo la Kawe.

Kwangu mimi naona hatua hiyo ni kudumaza demokrasia, Chadema baada ya kuona mwelekeo wa kesi unakula kwao wameona ni vizuri kuwapigia magoti NCCR ili wasije katwa ruzuku. Ukweli hizo ni siasa za majitaka
your wrong men in maana we hujui kuwa umoja ni nguvu, so ninachokiona apo ni hawa jamaa wanataka wajenge badala ya kubomoa au we unafurahia kuona watu wakitengana? ndo maana wahenga walisema tunajenga nyumba moja ya nini kugombea fito?
 
Back
Top Bottom