James Mbatia aamua kufuta kesi dhidi ya Halima Mdee

Wadau, nikiwa kama mhusika mkuu kwenye kesi. Napenda kuwahakikishia wanajamii pamoja na watanzania kwa ujumla kwamba Uamuzi wa mhe Mbatia wa kiuifuta kesi dhidi yangu ni dhamira yake njema ya kulinda maslahi mapana ya upinzani nchini. Nimesoma comments za wanajamii kadhaa ,baadhi yao wakifikiria labda kuna 'chochote kilichotolewa''ili kufanikisha kufutwa kwa kesi hiyo . Niwahakikishieni kwamba hakuna kilichotolewa zaidi ya nia njema ya pande zote mbili. Kwa waliokuwa wakijipanga kukomboa jimbo kwa gharama yoyote imekula kwao!

Najua mengi yatasemwa...lakini haiwezekani kuzuia binadamu kuzungumza. Nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati timu ya CHADEMA (chama changu) na NCCR MAGEUZI kwa kulifanikisha hili.

Asante kwa ufafanuzi, karibu sana jamvini, tunategemea mchango mkubwa kutoka kwako kama ilivyokuwa kwa hayati Regia Mtema, alikuwa na mchango mkubwa sana, naamini wewe ni mbunge shupavu mwenye uwezo wa kujenga hoja na kuitetea, sina shaka kwa hilo.
 
Wadau, nikiwa kama mhusika mkuu kwenye kesi. Napenda kuwahakikishia wanajamii pamoja na watanzania kwa ujumla kwamba Uamuzi wa mhe Mbatia wa kiuifuta kesi dhidi yangu ni dhamira yake njema ya kulinda maslahi mapana ya upinzani nchini. Nimesoma comments za wanajamii kadhaa ,baadhi yao wakifikiria labda kuna 'chochote kilichotolewa''ili kufanikisha kufutwa kwa kesi hiyo . Niwahakikishieni kwamba hakuna kilichotolewa zaidi ya nia njema ya pande zote mbili. Kwa waliokuwa wakijipanga kukomboa jimbo kwa gharama yoyote imekula kwao!

Najua mengi yatasemwa...lakini haiwezekani kuzuia binadamu kuzungumza. Nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati timu ya CHADEMA (chama changu) na NCCR MAGEUZI kwa kulifanikisha hili.
Mh Mdee, NCCR Mageuzi (james Mbatia) wamefuta kesi kwa mustakabali wa wananchi wa kawe na Dsm kwa ujumla. Nikuombe uwaombe viongozi wenzio wa kamati kuu wakubali muafaka wa umeya arusha kwa mafanikio ya wana arusha.If a=b, b=c then a=c. that is another episode in politics.
 
JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam John Utamwa , jana ilishindwa kutoa uamuzi wa ama hati ya madai katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge(NCCR-Mageuzi) dhidi ya mbunge Jimbo hilo Halima Mdee(Chadema) ifanyiwe marekebisho au la kwa maelezo kuwa bado hajakamilisha kuandaa uamuzi huo.

Wakili wa Mbatia, Mohamed Tibanyendera aliikumbusha mahakama hiyo kuwa jana kesi hiyo ilikuja kwaajili ya mahakama kutoa uamuzi huo na kwamba pande zote mbili zipo tayari kwaajili ya kupokea uamuzi huo.

Hata hivyo kwa upande wake Jaji Utamwa alisema hataweza kutoa uamuzi huo jana kwasababu bado hajamaliza kuandaa uamuzi huo hivyo akaiarisha kesi hiyo ya uchaguzi hadi Septemba 29 mwaka huu, ambapo atakuja kuitolea uamuzi.

Hatua hiyo ya mahakama kutaka kutoa uamuzi kuhusu hati hiyo ya madai, kunafuatia pingamizi lilowasilishwa na wakili wa Mdee, Edson Mbogoro la kuiomba mahakama hiyo imwamuru mlalamikaji aifanyie marekebisho hati yake ya madai na kuyaondoa baadhi ya madai ambayo Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni Mdee alimwita yeye kuwa ni Fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na CCM hivyo kuwataka wapiga kura wa jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.

Mdee anadai tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake na Mbatia ndani ya hati hiyo ya madai zinamletea kinamkera na hataweza kuziandalia utetetezi na kusisitiza kwa kuomba mahakama hiyo imwamuru Mbatia aondee hizo tuhuma kwenye hiyo hati ya madai.

Novemba 25 mwaka 2010 Mbatia alifungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee(CHADEMA) kuwa ndiye aliyeshinda na ataliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Chanzo:
Chazeti la Tanzania Daima la Septemba 22 mwaka 2011.
 
Sasa unalalamika nini post kama hii ikibadilishwa au kufutwa kabisa.It doesn't make any sense!!!!!!!!!!

Chanzo:ni Chazeti au (Gazeti) la Tanzania Daima la Septemba 22 mwaka 2011.
 
vyama vya siasa vinabidi vitoke kule vilikokuwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. Lazima vifanye siasa shirikishi.
 
Back
Top Bottom