G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,416
- 39,522
Mbunge wa jimbo la Kahama ndugu James Lembeli (CCM) amewaeleza bayana viongozi wa CCM wilaya ya Kahama kuwa hana hamu tena na hataki kuisikia CCM.
James Lembeli hata hivyo hajabainisha rasmi mustakabali wake mpya wa kisiasa ingawa habari zilizozagaa mjini Kahama ni kuwa mbunge huyo aliyemaliza muda wake yupo mbioni kutimkia Chadema.
Aidha katika hatua nyingine, mbunge wa viti maalum CCM ndugu Esta Bulaya naye amesema wazi kuwa hana tena mpango wa kuendelea kubaki CCM.
Mbunge huyo machachari bado hajadokeza chama atakachohamia na/au kuachana na siasa na hakuna uvumi wowote unaomhusu ulioenea au kuenezwa mpaka sasa.