James Bond sinema 23 kwa miaka 50 dhidi ya Bongo movies sinema 1 kwa mwezi

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,384
17,960
James Bond kwa takriban miaka 50 (1962 - 2011) ametoa sinema 23 ambazo ni wastani wa sinema 2 kwa mwaka kwa kuanza na Dr No ya 1962 hadi Quantum of Solace ya 2009. Katika kipindi hicho kuna madirector tofauti na Ma star tofauti ambao wamehusika katika hizo films.

Hawa watu ni matajiri wa dunia kwa hizo films chache walizocheza na familia zao zinaishi vizuri tu kwa movie hizo chache. Hapa Tanzania kila ukisoma kurasa za burudani za magazeti utaona matangazo ya wasanii wetu wakitangaza film mpya kila mwezi. Kwa harakaharaka wasanii kama akina JB, Kanumba, Ray au Richie wanapaswa kuwa ni mabilionaire kupita hata kiwango cha akina Sean Connery au akina Leonardo Di Caprio. Kinyume chake watu hawa wanaonekana bado wachovu ingawa wana kiasi cha kubadili mboga na kununua jeans na cream. Je wadau tatizo liko wapi?
 
Tofauti kubwa ya kwanza ni kuwa hizo series za James Bond zime base kwenye vitabu vya Ian Fleming na vilikuwa mashuhuri kama vitabu kabla ya kuwa movie.

Pili hivyo vitabu umashuhuri wake sio Uingereza tu, bali duniani kote na kusababisha movie zake pia kupendwa duniani kote.

Siwatetei kina Kanumba lakini kufananisha hivyo viwili ni sawa na kichunguu na mlima.
 
Sawa Gaijin na asante kwa mwomgozo na kwa kumjibu Ngallo mimi siangaliagi hizo sinema za akina Kanumba zaidi ya kusoma promo kwenye magazeti. Ila kwa mawazo yangu nilikuwa nafikiri pengine Watayarishaji wa Bongo movies labda wajifunze kutoka kwa magwiji wa film industry. Sijui hilo unalionaje
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Tatizo kubwa la hawa akina jb, kanumba, etc hawana ubunifu hata. Movie zoote zinahusu mapenzi. Thats why wanaweza kutoa edition mpya kila mwezi. Ni makosa kuziita sinema. Nadhani hz ni
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Nadhani ni tamthilia au tumiwa sekondari tulikuwa tunaita michezo ya kuigiza
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Na hao translators sijui wanawatoa wapi? Kingereza kibovu sana nadhan hiyo inachangia kuwa na limited market.
 
Wasanii wetu elimu duni nyenzo duni= WAGANGA NJAA!! Kibaya zaidi hawapendi kukosolewa!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Serikali haiwapi support kabisa! Kungekuwa na mkono wa serikal katka kudhibiti kwa namna moja ama nyingine vipato vyao vingeongezeka.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Serikali haiwapi support kabisa! Kungekuwa na mkono wa serikal katka kudhibiti copy fake,kwa namna moja ama nyingine vipato vyao vingeongezeka.
 
"Wastani wa sinema mbili kwa mwaka" hapo mkuu umekosea hesabu ni wastani wa sinema moja kila baada ya miaka miwili, maana miaka 50 sinema 23 au?
Hawa wenzetu ukiona Title tu umeshajua picha yote inazungumzia nini, sinema zao unaweza kuoneshwa m2 anatoka G/mboto mpaka posta ktk scene moja kisha unatakiwa kuangalia part 2 muendelezo baada ya muhusika kufika Posta.
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
bongo moviez ni vichekesho,kuna muvi 1 waliigiza wakaweka eti behind the scene. Yaani director anatunga movie on set eti anamwambia jamaa "embu pita huku tuone,ukipita hapa atakuona huyu jamaa..." actor nae anasema "amna bana nipite hapa ntainama tu jamaa asinione..." nikasema kwel hii ndo Bongo movie. Teh teh
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Hata mimi siangaliagi hii michezo ya kuigiza lakini inaonekana ina soko kubwa sana kwa akina mama wa nyumbani ambao ndiyo soko kubwa sana la hii michezo ya kuigiza. Kwa hiyo as long as kuna soko la hii michezo ya kuigizwa inayo pakuliwa kila asubuhi na DVD kuuzwa kati ya Sh 3,000 na 5,000 basi tasnia hii mbovu itaendelea kukua nchini
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
"Wastani wa sinema mbili kwa mwaka" hapo mkuu umekosea hesabu ni wastani wa sinema moja kila baada ya miaka miwili, maana miaka 50 sinema 23 au?
Hawa wenzetu ukiona Title tu umeshajua picha yote inazungumzia nini, sinema zao unaweza kuoneshwa m2 anatoka G/mboto mpaka posta ktk scene moja kisha unatakiwa kuangalia part 2 muendelezo baada ya muhusika kufika Posta.

Thanks Likwanda for spotting the arithmetic error
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Sawa Gaijin na asante kwa mwomgozo na kwa kumjibu Ngallo mimi siangaliagi hizo sinema za akina Kanumba zaidi ya kusoma promo kwenye magazeti. Ila kwa mawazo yangu nilikuwa nafikiri pengine Watayarishaji wa Bongo movies labda wajifunze kutoka kwa magwiji wa film industry. Sijui hilo unalionaje
Mkuu ulivyokana juu ya kuangalia movie za Kanumba as if its a crime 2do so. Nyingine zipo fresh, kama unafuatilia promo za uzinduzi si vibaya ukawaunga mkono, wewe mwenyewe umeshangaa kwanini wana kipato kidogo, 7bu moja ndo hyo, kazi zao hazinunuliwi.
 
Apta kinachonisikitisha na sinema zetu ni kwamba msanii anashirikishwa siku ya kwanza kama underground baada ya sinema hiyo anataka naye awe 'star wa sinema'. Akimaliza kuwa star ataanza kudai kuwa producer, siku nyingine atajiita 'Director' na hicho ndiyo taabu ya hii michezo ya kuigiza ya bongo. Ukichukulia mfano sinema za James Bond unakuta wasanii Kama watatu tu kwa miaka yote hiyo yaani Sean Connery, Roger Moore na Craig?. Then hata Ian Flemming inawezekana hakutunga novel zote yeye mwenyewe, pengine kuna watu walikuwa na episodes zao wakaamua kuingia mkataba na Ian Fleming ili hadithi itoke kwa jina hilo. Kwa hiyo hata hapa nyumbani angalao tungekuwa na nyota wachache tu ambao watakuwa vinara wa kucheza hizo movies na wengine waandike tu na kuwapa hao vinara kwa mkataba maalum.Lakini kwa huu uelekeo kila mwigizaji kujiita Director au Producer kila uchao hatuna namna tutaendelea kupata sinema zenye viwango duni ambazo soko lake haliwezi kuvuka sh 5,000
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Back
Top Bottom