Jambo limezua jambo

Jambo limezua jambo

Mnataka msikie mnayoyapenda, yanayowafurahsha tu? Kimsingi hakuna serikali tatu hapa....hata kwa damu

Bahati mbaya yako unatetea kitu ambacho hukijui. Siku ukijua kweli kwamba ni kweli utarudi kufuta kauli hapahapa. Tusubiri yangu macho.
 
Kufufuka kwa Tanganyika mbona kunakuwa kugumu namna hii jamani?

Ccm wamefanya na wanaendelea kufanya mazindiko ya damu.sasa wanaotaka kuwepo serikali tatu wanapigana kirahisirahisi ndio maana ugumu huu upo.kuleta serikali tatu kunahitaji kuelewa adui anayeing'ang'ania anapiganaje vita hii.
 
Shivji sijui amekubali vp kununuliwa na ccm na kuwatosa watz.wakati alikuwa muhamasishaji mzuri sana wa vijana na wanaharakati kutokubali kununuliwa na ccm.siamini anabadilika siku hadi siku
 
ushahidi please...

Ushahidi wa nini kama unapinga kuwa CCM hawakufadhiri Kongamano hilo tuambie ni nani aliyefadhri kwani Ukumbi uliotumika ni wa kulipia, wajumbe waliohuduria wengine walitoka mikoani mbali na DSM ni nani aliwalipia gharama za Ufafiri na maradhi hapo DSM.
 
Wengi humu naona hamjamsoma wala kumsikiliza Profes Shivji, mnakurupuka tu kufata mkumbo hata hamjui alichokiongea. Kama mpo aliomsoma wekeni nukuu iliyowaudhi na muijengee hoja, yeye aliyoyasema yote kayajengea hoja amesema hivi:

Katika mjadala unaoendelea kumekuwa na malumbano na mabishano kati ya wasemaji, wafuasi na wapigadebe wa ama serikali tatu au serikali mbili. Wachambuzi, kama wapo, ni wachache sana – na hata hao wachache hawasemi au hawasikiki. Rai yangu kwenu ni kwamba sisi kama wanazuoni tusijidandie kundi lolote kati ya makundi hayo matatu.

Jukumu na wajibu wetu ni tofauti kabisa. Wajibu wetu ni kuchambua hali halisi bila jazba; na kutokana na uchambuzi wetu kuonesha uzuri na ubaya wa mambo. Sisi wanazuoni nafasi yetu ni kuwa kioo cha jamii, kuonesha jamii uzuri na ubaya wake na kwa vipi na kwa njia gani uzuri unaweza kuimarishwa na ubaya kupunguzwa.

Baada ya kusema hayo kaanza kuchambuwa na kutoa hoja zake, sasa nyinyi mnakurupuka humu hata hatujui mnachokipinga kutoka kwa Shivji ni nini?

Ndiyo maana mkaambiwa Watanzania ni miongoni mwa watu wenye IQ ndogo duniani.
 
Mara nyingi nasema siasa haihitaji watu werevu sana isipokuwa wabobezi kwenye fitna! Haya ndiyo nayoyashuhudia sana watu waliopata kuheshimika kutokana na werevu wao kuamua kupiga teke heshima zao na kujikita kwenye malumbano ya kisiasa ambayo kimsingi yalitakiwa kuendeshwa na naowaita wabobezi wa fitna!
 
Mnataka msikie mnayoyapenda, yanayowafurahsha tu? Kimsingi hakuna serikali tatu hapa....hata kwa damu

Nampongeza sana mwanasheria makini issa shivji

CHADEMA mbona mnaogopa kivuli chenu?

Heshima ya Prof Shivji haiwezi kushushwa kirahisi namna hiyo

Nani kwa kumlinganisha na shivji kwenye uga wa sheria hapa nchini?

Umemsahau na profesa kulikoyela Kahigi

Mnataka Watanzania wote wawe na maoni kama ya magwanda?

Mwanasheria msomi issa shivji, ngumi jiwe

Buku 7 mpo kazini kutetea serikali 2
 
Mjadala alioendesha Shivji ulilipiwa na CCM,kabla ya mdajala alionekana akiwa katika kikao na viongozi wandamizi wa CCM,mkakati mpya wa CCM kuvuruga mbunge ndani ya wiki mbili zijazo ili Tanganyika huru isipatikane,wanaharakati tumejipanga kufanya mandamano ya kufunga jiji zima.

Maandamano na migomo ndio silaha pekee iliyobakia ya kupata Tanganyika yetu na kuwang'oa hawa wakoloni weusi
 
Ccm wamefanya na wanaendelea kufanya mazindiko ya damu.sasa wanaotaka kuwepo serikali tatu wanapigana kirahisirahisi ndio maana ugumu huu upo.kuleta serikali tatu kunahitaji kuelewa adui anayeing'ang'ania anapiganaje vita hii.

Inabidi tufanye kazi ya ziada. Kama wao wanatumia nguvu za giza tunaoitaka Tanganyika tumwombe Mungu wa kweli kwa bidii zote ili Mungu awajalie wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba upako wa kipekee wa kujenga hoja za kutetea Tanganyika kwa bidii kubwa. Mazindiko ya CCM hayatafua dafu kwa maombi ya Wacha Mungu wanao omba kwa bidii usiku na mchana.
 
Amekuta yale aliyoyaandika kwa vitendo hayatatekelezeka;
ana akili sana.
 
Ameshakengeuka huyu mzee,ila ninachojifunza ni kwamba wasomi siku hizi ni njaa kali.
 
Mzee Warioba aliwahi kusema kila mtu ananunulika ishu ni kujua bei tu, sikuamini mpaka niliposhuhudia Prof Shivj ametinga price tag, trust no one.
 
Wahindi huwa ni wanafiki. Nani asiyejua tabia zao. Alivyokuwa anashawishi kuhusu serikali tatu alifikiri ni mchezo. Sasa keshapitwa na muda na tabia yake halisi inaanza kuonekana. Wala na watoa rushwa tu wahindi hao. Mhindi hawezi kuwa mtanganyika wala mtanzania. Anayebisha aende kwenye jumuiya zao ndo atajua kuwa muhindi ni muasia tu na yote mengine ni unafiki wa kuhakikisha wanafanikisha maslahi yao.
 
Hakuna Profesa yeyote aliyewahi kufanikisha jambo lililoacha alama duniani.
 
Hivi kweli kuna mwenye akili timamu atampuuza Shivji na kumsikiliza Lisu au Jusa.......

Tatizo la kizazi hiki cha karibuni mnapotaka kuhalalisha hata bangi na mirungi, basi mtazipamba kwa maneno meengi matamu kiasi kwamba hata baadhi ya wazee wenye roho ndogo wanalegea na kufikiri mnajua mnachokiongea.
 
Hata kama inasemwa mtoto akililia wembe mpe, lakini bado inategemea mzazi na mzazi,uchungu alionao mzazi husika na kiwango cha ujinga alichonacho Lis....sorry mtoto.
 
Shivji ni msomi mwoga na msaliti wa wanzanzibari na watanganyika
 
Nani kwa kumlinganisha na shivji kwenye uga wa sheria hapa nchini?

Rafiki "KAMA ANAJUA SHERIA MBONA ANAJICHANGANYA MWENYEWE?" kama amehongwa pesa sawa, maana pesa mwana malevya.
 
Hivi kweli kuna mwenye akili timamu atampuuza Shivji na kumsikiliza Lisu au Jusa.......

Tatizo la kizazi hiki cha karibuni mnapotaka kuhalalisha hata bangi na mirungi, basi mtazipamba kwa maneno meengi matamu kiasi kwamba hata baadhi ya wazee wenye roho ndogo wanalegea na kufikiri mnajua mnachokiongea.

kwanini anajichanganya katika maandishi ya vitabu vyake mwenyewe? Tunaelewa kuwa ni msomi mzuri lakini kama ananza kujichanganya , ukiendelea kumwaamini maana yake wewe una matatizoya akili huwezi hata kuhoji kujichanganya huko?
 
Back
Top Bottom