Jambo leo: Mtwara wakubali gesi itoke.

Jambo leo: Mtwara wakubali gesi itoke.

Wana mtwara wamechochewa na wanasiasa, sio akili yao ile

Wewe unakaa Mtwara? mimi nipo mtwara na nimefuatilia sana hoja zao,wamakonde hoja wanayo tena wamedhamiria hasa. ukienda maeneo ya soko kuu na vijiwe maarufu kuwasikiliza ndio utagundua ni watu wenye kumbukumbu ya wanakotoka, walipo na wanako kwenda.wanazo hoja za maana sana na ndio maana hawapendi wavurugwe na wanasiasa kati suala hili la gesi.
 
Hakuna kitu kama hicho,machafuko mengine yametokea usiku wa jana huko msimbati,
unasomaje gaezi la habari leo na kusikiliza Tbccm?
Soma nipashe upate habari yote...
Ngoma hii wataisoma mwaka huu...

Mkuu THE BIG SHOW.

Natambua kuwa bado hali ni tete (kwa mujibu wa vyombo vya habari na taarifa za milipuko ya jana usiku), natambua pia uwepo wa propaganda za kufifisha ukweli wa juu ya kile kinachotokea Mtwara kwa sasa.

Niko makini sana na vyombo vya habari kwa sasa, tbc1 zaidi ya bunge na ze comedy sina kipindi kingine ninacho angalia. Habari hii nimeipata kwenye tuongee asubuhi kipindi cha magazeti.

By the way, hali ikoje sasa huko N'twara.
 
Last edited by a moderator:
Gazeti la jambo leo limeandika "Mtwara wakubali gesi itoke" wanasema ni baada ya jeshi la wananchi wa Tanzania kwenda kurejesha amani, salamu ya wana mtwara imebadilika kutoka "Gesi haitoki" hadii kuwa "Gesi inatoka".

CC THE BIG SHOW
Hata mkikesha Tanzania Daima kuandika uchochezi gesi itatoka Mtwara; hiyo ni rasimali ya Taifa hizo kelele zenu hazitaifanya serikali kuacha mikakati ya maendeleo; Mtwara ilikuwa haina kitu chochote cha maendeleo baada ya korosho kuanguka bei; walikula kwa hela za pamba; katani; tumbaku,almasi; kahawa na chai;kama wamesahau wakumbusheni; je leo na wasukuma; wabena; wagosi; wachaga na wanyamwezi wadai fadhila zao?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
Hilo gazeti linashiriki kufanya uchochezi wa ghasia kwa kuwakejeli watu wa mtwara.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hata mkikesha Tanzania Daima kuandika uchochezi gesi itatoka Mtwara; hiyo ni rasimali ya Taifa hizo kelele zenu hazitaifanya serikali kuacha mikakati ya maendeleo; Mtwara ilikuwa haina kitu chochote cha maendeleo baada ya korosho kuanguka bei; walikula kwa hela za pamba; katani; tumbaku,almasi; kahawa na chai;kama wamesahau wakumbusheni; je leo na wasukuma; wabena; wagosi; wachaga na wanyamwezi wadai fadhila zao?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz

Ulivyo pimbi unadhan wana mtwara hawataki gesi itoke.
 
Last edited by a moderator:
Mtwara ilikuwa haina kitu chochote cha maendeleo baada ya korosho kuanguka bei; walikula kwa hela za pamba; katani; tumbaku,almasi; kahawa na chai;kama wamesahau wakumbusheni; je leo na wasukuma; wabena; wagosi; wachaga na wanyamwezi wadai fadhila zao?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz

Uzuri ni kwamba unaandika haya ukiwa umejificha nyuma ya kibonye chako. Ungeitoa kauli hii ukiwa Mtwara ningekuelewa hasa kutokana na kauli yako ya kusema korosho imeanguka bei bila kugusa kiini cha bei kuanguka.
 
Last edited by a moderator:
Hata mkikesha Tanzania Daima kuandika uchochezi gesi itatoka Mtwara; hiyo ni rasimali ya Taifa hizo kelele zenu hazitaifanya serikali kuacha mikakati ya maendeleo; Mtwara ilikuwa haina kitu chochote cha maendeleo baada ya korosho kuanguka bei; walikula kwa hela za pamba; katani; tumbaku,almasi; kahawa na chai;kama wamesahau wakumbusheni; je leo na wasukuma; wabena; wagosi; wachaga na wanyamwezi wadai fadhila zao?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz

Msikilize Maige
 
Last edited by a moderator:
Tusikie kwa wana Mtwara waliomo humu
 
Yaani baada ya kichapo sasa gesi inatoka,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Uzuri ni kwamba unaandika haya ukiwa umejificha nyuma ya kibonye chako. Ungeitoa kauli hii ukiwa Mtwara ningekuelewa hasa kutokana na kauli yako ya kusema korosho imeanguka bei bila kugusa kiini cha bei kuanguka.

Serikali haipangi bei ya kuuza korosho; Chicago Mercantile Exchange ndio bei za bidhaa za nafaka zinapopangwa kutegemea wazalishaji na walaji; unapiga kelele kujifanya unatetea wamakonde kumbe ni unafiki wenu hata korosho zenyewe hununui kuboresha soko la ndani ; kaa ukijua gesi itatoka tu bila wasiwasi wowote; vipi ajira Tanzania Daima imejipa?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kazi moja wapo ya JF nikutunza kumbukumbu......haya tuendelee Mheshimiwa nani sijui...wewe hapo nyuma unaechungulia endelea....
 
Hata mkikesha Tanzania Daima kuandika uchochezi gesi itatoka Mtwara; hiyo ni rasimali ya Taifa hizo kelele zenu hazitaifanya serikali kuacha mikakati ya maendeleo; Mtwara ilikuwa haina kitu chochote cha maendeleo baada ya korosho kuanguka bei; walikula kwa hela za pamba; katani; tumbaku,almasi; kahawa na chai;kama wamesahau wakumbusheni; je leo na wasukuma; wabena; wagosi; wachaga na wanyamwezi wadai fadhila zao?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz

Katika siku ambazo umeongea Pumba leo umeongoza,wewe hukujui kusini ungea upendavyo ukizani unakisaidia Chama chako.

Sawa gesi itatoka lakini baada ya kuwaua maelfu ya watu wa kanda ya kusini,hatutakubali kufanya ujinga wa songosongo.

Kwa taarifa yako kuanzia saa sita usiku mpaka saa kumi na moja alfajiri ya leo mabomu na risasi za moto zilikuwa bado zinarindima.Polisi walikuwa wanakimbizana na vijana usiku kucha.

Mohammedi Mtoi hao waliowahoji Jambo Leo ni Hawa Ghasi,Mkuchika,Sinani na Anna Abdallah.
 
Tangazo kwa wana kusini tu:

Kuna kijimradi changu nimeanzisha,natafuta form four wote waliofeli katika shule za kata niwaajiri.Kama una mwanao tafadhali mlete maeneo ya msimbati na maeneo yote ambayo Bomba la gesi litapita.
 
Maigizo mengine yanoyotokea Mtwara.

Ni kwamba Polisi na Wanajeshi(JWTZ) wakikutana na Raia wanamuuliza"Gesi inatoka au haitoki".Raia akijibu haitoki wanampa kipigo mpaka aseme inatoka.

Naona hawa ni miongoni mwa watu waliohojiwa na Jambo leo,ukiwaongeza Hawa ghasia,Mkuchika,sinani na Anna Abdallah.
 
Gazeti la jambo leo limeandika "Mtwara wakubali gesi itoke" wanasema ni baada ya jeshi la wananchi wa Tanzania kwenda kurejesha amani, salamu ya wana mtwara imebadilika kutoka "Gesi haitoki" hadii kuwa "Gesi inatoka".

CC THE BIG SHOW

Nadhani hili gazeti kila siku kwao ni 'siku ya wajinga duaniani'...
 
Back
Top Bottom