Mkuu
Mohamedi Mtoi, jambo lolote linalohusisha watu wengi huwa na mushkeli. Jambo Leo linaripoti kuwa WAMEKUBALI, hizi tutaita propaganda, lkn litakaloripoti WAMEKATAA tutasema limesema kweli. Jambo la kujiuliza ni kwamba hawa wote wawili wanamhoji nani?
Wakati tunaona watu na mabango mitaani na nyumba zikichomwa moto, kuna ambao wamesalia majumbani mwao wakikerwa kweli kweli na hayo maandamano. Ila kwa kuwa hawa wameamua kufanya fujo, basi wanaonekana kuwasemea wenzao.
Hata mimi nina jamaa zangu Mtwara, wao maoni yao ni kwamba, fujo hizi zinaletwa na watu wasio na kazi na ni kwa yale walioambiwa na wanaowachochea.
Kuna bwana mdogo mmoja aliwahi kuniambia hivi wakati wa zile fujo za kwanza:
HATA MTWARA NAYO INATAKIWA KUENDELEA KAMA BAGAMOYO NA KATAVI. Ukiyatafakari haya utaona ni upuuzi wa kuambiwa, ila kwa mimi niliyefika Mtwara, Katavi na Bagamoyo namuonea tu huruma kwa kuwa na mshawasho wa kujitafutia madhila kwa jambo la kijinga kabisa kwani Mtwara ni mji mkubwa kuliko Katavi na Bagamoyo.
Hapa utaona ni kwamba kalishwa tu maneno kwa kuwa Katavi anatoka PM na Bagamoyo President. Sasa je, tunapaswa kuamini kuwa kila aishie Mtwara anaamini haya? Na Mtwara haiishii Mikindani, mpaka Newala ni Mtwara, je huko nako wanasemaje?