Jambo leo: Mtwara wakubali gesi itoke.

Jambo leo: Mtwara wakubali gesi itoke.

Hongereni wana mtwara kwa kukubali gesi itoke, na kama hivyo, basi na wale watu 91 waliokamatwa, waachiwe, kwa kuwa mgogoro umekwisha. na wale waliopoteza maisha, wajengewe mnara wa kumbukumbu za wahanga wa gesi.
 
Gazeti la Jambo leo ni chombo cha propaganda za CCM na serikali.
Bora gazeti la Uhuru kuliko jambo leo.
Hata vitumbua halifai kufungia.
Linafaa kutumika chooni tu.

JF kuna vichwa!!!,
 
Wamefanya uamuzi mzuri. Pongezi kwa wananchi wa Mtwara.

Tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?

nyumba ipi?mbona nimeona mabomba yapo pale Kerege kwenda bagamoyo?
 
hicho kikao wamekaa saa ngapi kukubaliana hivyo, wakati wengi wao wapo jela na wangine wamekimbilia porini.?
 
Hilo gazeti linashiriki kufanya uchochezi wa ghasia kwa kuwakejeli watu wa mtwara.



Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums


kp24052013.jpg
 
Serikali haipangi bei ya kuuza korosho; Chicago Mercantile Exchange ndio bei za bidhaa za nafaka zinapopangwa kutegemea wazalishaji na walaji; unapiga kelele kujifanya unatetea wamakonde kumbe ni unafiki wenu hata korosho zenyewe hununui kuboresha soko la ndani ; kaa ukijua gesi itatoka tu bila wasiwasi wowote; vipi ajira Tanzania Daima imejipa?

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu.
Naomba nianze na angalizo maana kwenye ule mjadala wa Prof J ulijivua ufahamu na kuporomosha matusi. Ukitaka mjadala na mimi ujifunze kujadili kwa kutumia lugha za staha na kistaarabu, tunasomwa na wadogo zetu na wakubwa wetu walio tuzidi umri humu.

1. Umesema "Chicago Mercantile Exchange ndio mahali ambapo bei za nafaka zina pangwa kutegemea wazalishaji na walaji " kauli hii na jibu hili lina mwanya mpana sana kwa sababu sio kweli kwamba bei zote zina pangwa CME kama ulivyo sema na si kweli kwamba hao CME ndio wamepanga na kusema wakulima wa korosho wakopwe na wasilipwe fedha zao kwa wakati.

2. Umesema "napiga kelele kuwatetea wamakonde kumbe ni unafiki na hata korosho zenyewe sinunui". Ninacho kifanya hapa sio kupiga kelele bali natumia haki yangu ya msingi kikatiba kama jinsi ilivvyo ainishwa kwenye ibara ya 18 haki ya uhuru wa mawazo (a) "... Uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra" usianze kuwa kiranja wa kuelekeza kipi nijadili na kipi nisikijadili.

Lakini pia najadili mambo ya Mtwara kwa kuwa mimi ni Mtanzania na yanayotokea Mtwara yananigusa kijamii, ibara ya 8 (1), (a) inasema ..."Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi" kwa ibara hii, kama. Serikali ingetambua nafasi ya wananchi wa Mtwara busara za kawaida zina nituma kuamini kuwa hakukupaswa kuwa na vurugu kama serikali ingewashirikisha wana Mtwara ipasavyo. Nayaongea kwa kuwa serikali imeshindwa kutimiza takwa la kikatiba, hili lina onwa na mtu yoyote sio lazima awe mkazi wa Mtwara, sio lazima anunue au asinunue korosho.

Lakini pia ibara hiyohiyo ya 8 Ibara ndogo kifungu (b) na (c) inasema ... " Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi, na serikali itawajibika kwa wananchi". Kimantiki, kifungu (b) na (c) kinawapa nguvu wananchi kuhakikisha ustawi wa nchi yao na kimsingi nchi inaanza kwenye eneo la kijiografia mahali ulipo, kama hivyo ndivyo wanamtwara wana haki ya kufaidi na madini kamaa jinsi watu walioko kwenye mbuga za wanyama wanavyo faidi raslimali hizo.

Mwisho
Umeongelea ajira Tanzaniadaima. Asante kwa kuonyesha upendo kwangu lakini nasikitika kuwa siko hapa kutafuta ajira, ajira niliyo kuwa nayo inanitosha, tafiti ninazo fanya kule kwenu Kwale wilaya ya mkinga zinanitosha na zimeanza kuonyesha matunda maana fukwe za bahari sasa hazitumiki tena kama vyoo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
ata ikitoka acha tu japo matumbo la jk, pinda na muhongo yafanane na ya komba mwimbaji wa pambio za kunadi vtumbua vya wendawazimu ccm!
 
Gazeti la jambo leo limeandika "Mtwara wakubali gesi itoke" wanasema ni baada ya jeshi la wananchi wa Tanzania kwenda kurejesha amani, salamu ya wana mtwara imebadilika kutoka "Gesi haitoki" hadii kuwa "Gesi inatoka".

CC THE BIG SHOW

Hivi Jambo leo nalo ni gazeti la kutumia kama credible source of information?!
 
gazeti la jambo leo limeandika "mtwara wakubali gesi itoke" wanasema ni baada ya jeshi la wananchi wa tanzania kwenda kurejesha amani, salamu ya wana mtwara imebadilika kutoka "gesi haitoki" hadii kuwa "gesi inatoka".

Cc the big show
mmh tatizo umekuwa biased umesoma jambo leo umesha amini kuwa kweli watu wa mtwara tumebadilisha kauli,huo ni uongo wanajeshe tangu wamekuja wanawaambia watu waendelee na shughuli zao tu kama kawaida wala hawagusii swala la gesi wala hawapigi watu kama ilivyokuwa kwa polisi,jaribu kufuatilia na upande wa pili sio kukurupuka tu kuja kupost hapa,hakuna aliyesema gesi inatoka zaid ya watu kukaa kimya tu sasahivi watu hawazungumzii hadharani kama gesi haitoki ni minong'ono ya chini kwa chini tu ndio ipo kuwa gesi haita toka
 
Gazeti la jambo leo limeandika "Mtwara wakubali gesi itoke" wanasema ni baada ya jeshi la wananchi wa Tanzania kwenda kurejesha amani, salamu ya wana mtwara imebadilika kutoka "Gesi haitoki" hadii kuwa "Gesi inatoka".

CC THE BIG SHOW

Waache wajidanganye! Mtwara hawataki masihara katika hili. Usanii kama wa akina Kova kule utasababisha vifo vingi sana ukitumika
 
Gazeti la jambo leo limeandika "Mtwara wakubali gesi itoke" wanasema ni baada ya jeshi la wananchi wa Tanzania kwenda kurejesha amani, salamu ya wana mtwara imebadilika kutoka "Gesi haitoki" hadii kuwa "Gesi inatoka".

CC THE BIG SHOW

Jambo leo gazeti gani hilo? Si kweli hadi tuone waongeaji ktk kikao.
 
Last edited by a moderator:
I don't think so, mtwara wamejipanga Hasa. Wamekuwa marginalized for so long.....waki give up hata vizazi vijavyo vitawahukumu!

Gesi itoke as permatakwa ya wanamtwara but not otherwise! Wakitumia nguvu kweli gesi bomba litatoa maziwa na si gesi. Tupo na tutaona.
 
Back
Top Bottom