Jambo leo: Mtwara wakubali gesi itoke.

Jambo leo: Mtwara wakubali gesi itoke.

Katika pitia pita ya magazeti asubuhi hii imedaiwa kuwa wana Mtwara wamekubali kuwa gesi itoke mkoa humo kwa kuwa walikua hawajui faida za gesi watakazo pata kwa ujumla.

Napenda kujua habari hizi ni kweli kwa Wanamtwara??

Kama ni kweli hongereni sana kwa vikao mlivyokaa na kuamua hayo

JAMANI, naomba tusiingize SIASA katika maisha ya watu, suala la GESI MTWARA, inaonesha hali si shwari kabisa, bado wananchi wanajisasi sana, believe me or not, THINGS GONNA BE MORE THAN WORSE U ESPECT unless the govnt seat in a round table with these people. NI JANA ALFAJIRI wakati RPC akitangza amani kutawala mtwara, bomo lililosadikiwa kutegw na wananchi huko MSIMBATI kwenye visima vya GESI kama hiyo haitoshi jana kuamkia leo MABOMU MAKUBWA YALIYOTIKISA MJI MZIMA WA MTWARA YALILIPUKA hapa mtwara; suala la gesi hapa MTWARA lipo kwenye mioyo ya watu ni VIGUMU KULIPORA KWA NGUVU bali kwa uelewano na kusikilizano.
 
tanzania daima wameandikaje?
Wewe nawe unatiaga aibu tu humu jamvini, nakushauri usipost chochote humu kwenye mitandao kwa muda,ili uwe unaangalia tu namna wenzio wanavyoandika,au kama una mtoto hata wa Std 4
Mwombe akuandikie, ni ushauri tu mheshimiwa.
 
Hizi sio habari za kuzinyamazia haata kidogo...ni nyie watu mnatumia masaburi kufikiria na kujadili mambo ya jamboleo osio?hali ya mtwara bado sio shwari ni lini na ni wapi wamefanya mkutano na wanamtwara wakakubaliana kwamba gesi itoke? hiyo kauli mbiu "GASI ITATOKA" imetumika wapi?? Na nani kafanya huo mkutano na wanamtwara akakubaliana nao? Pinda mwenyewe mpaka bungeni kapotosha bado tu hamjafikiria kuhusu huu upuuzi?

Wanamtwara are not that much loose...sawa!! They are stronger enough on these issues....kwani gesi ikibaki mtwara na process kufanyiwa kule ndo inaondoa umaana kwamba gesi ya mtwara ni ya watu wote? Sasa kwa taarifa tu...kuna meseji zinasambaa kwa kasi sana kwamba mtu yeyote atakayekuja kwenye ujenzi wa hili ibomba, awe mzungu, mchina hata mtu wa kaskazini basi ni halali yake arudi maiti...(sio maneno yangu)!! Watu wananoa zana tu!! Pambav sana!!
 
Wamefanya uamuzi mzuri. Pongezi kwa wananchi wa Mtwara.

Tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?

Ila tu tusije rudi huku


Chanzo chetu mkoani Mtwara kilisema; “Watu wa Mtwara tumekuwa tukikutana tangu Waziri Mkuu aondoke wiki iliyopita, kwa kweli hatujaridhika kabisa, na tunashangaa mambo aliyokwenda kuzungumza kule Dodoma.


“Sisi tulikaa naye, na alipomaliza kazi yake kabla ya kuondoka alitupata ahadi moja tu, ahadi yenyewe alisema anayachukua yote na kuyapeleka kwa Rais ili yapatiwe ufumbuzi.


“Lakini kesho yake tunashangaa kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa Waziri Mkuu amefanikiwa kuuzima mgogoro wa gesi Mtwara, hili si kweli hata kidogo na Serikali wanafahamu.


“Lakini pamoja na yote hayo, tuliposikia Bunge linaunda kamati kuja Mtwara kuchunguza mgogoro huu, hapo tukawa na matumaini kwamba wawakilishi wanakuja, ili tuwaeleze ni nini hasa tunakitaka.


“Lakini baadae tena tunasikia hiyo kamati haiji tena Mtwara kwa sababu mgogoro umekwisha. Baada ya kusikia hivyo basi tukajua kuna kitu kilishakusudiwa tangu awali, kwa hiyo kitabaki kama kilivyo.


“Kwa hiyo sisi tutaendelea kudai haki yetu mpaka pale tutakaporidhika kwamba haki yetu itabaki hapa Mtwara na kutunufaisha kwanza, na katika hili hatutaki siasa wala maneno matamu.”


Wakati hali ikiwa hivyo, taarifa zaidi zinasema kuwa, idadi ya polisi mitaani na hata wale wa usalama barabarani imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na hali ya usalama kuwa tete.


“Mtu yoyote akija Mtwara atajionea mwenyewe, idadi ya polisi barabarani imepungua sana, hata watu wanaokwenda polisi kwa ajili ya kuripoti matukio madogo kama ya wapenzi kupigana kwa sasa hawasikilizwi.


“Polisi wanajaribu sana kuepuka kutengeneza mazingira yanayoweza kusababisha vurugu, hii ndio hali halisi ya Mtwara na maeneo ya jirani,” alisema mtoa habari wetu.


Akizungumzia hali hiyo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara (RPC), Maria Nzuki, alisema Jeshi la Polisi mkoani humo mpaka jana lilikuwa halina taarifa zozote kuhusiana na maandalizi ya maandamano hayo.


RPC Nzuki alisema; “Sisi hatuna taarifa za maandamo hayo ya tarehe 10, lakini kwa sababu tumeulizwa, basi kama polisi tutazifanyia kazi mara moja taarifa hizo.


“Kuhusu askari polisi kutoonekana barabarani, si kweli, askari wapo, isipokuwa kwenye vituo vidogo hawapo kwa sababu vilichomwa moto. Tunasubiri hali ya usalama itakapotengemaa, basi watarejea.”


Baada ya kutokea kwa machafuko makubwa mjini Mtwara Desemba 27, 2012, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alikwenda mjini humo, ambapo pamoja na mambo mengine alizungumza na viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, kisiasa na Serikali.


Baada ya ziara yake hiyo, aliporejea mjini Dodoma alizungumza na vyombo vya habari na kusema moja ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwao Rais Jakaya Kikwete.


Pinda alisema mbali na imani hiyo, alibaini kuwapo mpasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mtwara, na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.


“Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa si kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja.


“Pamoja na hayo nikachukua maelezo kuhusu matatizo yao mengine na nikawaahidi kwamba nitayafikisha katika mamlaka husika, ili waweze kuona namna ya kufanya.”


Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya mabango wakati wa maandamano hayo ambayo yalidaiwa kuratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa.


Pinda alisema viongozi wa kisiasa mkoani Mtwara wakiwamo wabunge, wameonekana kuwa na mpasuko unaosababisha uchochezi kwa makundi ya watu.
 
Nchi yetu bado ina mambo ya kitamadun-had ktk mambo ya msingi kabisa bila shaka mmeshuhudia maamuz juu ya mitihan-hii ni shangwe kwa mabeberu-kulikuwa na ubaya gan kuwekeza ntwara?kukubar gan huko kwa jeshi?
 
Wamefanya uamuzi mzuri. Pongezi kwa wananchi wa Mtwara.

Tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?

Aaahh! Nyumba moja wapi bwana! Yaani nyumba ikajengwe Bwagamoyo halafu useme nyumba hiyo ni ya wana Mtwara pia?!! Hayo ndio maajabu ya kila siku Tanzania.

Kama ingekuwa hiyo, maeneo ya kusini yasingekuwa nyuma kimaendeleo kutokana na rasilimali zinavyo vunwa Kanda ya Ziwa, Mbuga za Wanyama Kaskazini kwa mapato yake kupelekwa kusini kwa ajili ya maendeleo.

Kwa ufupi "HIZO NI SIASA ZA KILAGHAI".
 
Mkuu Mtoi hizo ni akili za matope kabisa za gazeti la jambo leo,siku zote naamini katikakulizungumza jambo kwa uwazi kwa kufuatilia kiini cha tatizo,kisha kwa pamoja kutoka pande mbili zinazosigana kutafuta muafaka.
si kwa jinsi hii ya kuandika propaganda za hovyo,kumbukeni wadau previous tuliwahi kuambiwa waziri mkuu mtoto wa mkulima alimalizana na watu wa mtwara,leo hali ikoje?waandishi waliandika kwa nguvu lakini kiko wapi?maoni yangu ni upuuzi wa hali ya juu kujiongopea mwenyewe huku ukuijua unajidanganya.
 
kweli labda gesi yaushuzi toka tumboni mwamagamba itatoka lkn sio yamtwara!yaani juzi tu,mmewaua hadi wanawake nawatoto tumboni,mmekamata watu zaidi ya91,mapoliccm mmeiba mali zawananchi nakuwabaka wakezao!leo very simple eti wamekubali gesi itoke?hizo nihadidhi zakusadikika,gesi kwanza uhai baadae!labda wawaue wanamtwara wote!tunako enda watu wataanza kuvaa mabomu yakujitoa mhanga ktk nchi hii subiri muone,hamuwezi kuwanyanyasa wananchi kiasi hicho!
 
Wamefanya uamuzi mzuri. Pongezi kwa wananchi wa Mtwara.

Tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito?

Ni kweli tunajenga nyumba moja lakini inakuwaje chumba kimoja ndio kinawekwa marumaru na vikolombwezo vyote na vyingine vinaachwa?

Hivi mpaka wa leo hujajiuliza kuhusu Bandari kubwa moya pale BYO wakati ile ya Mtwara ni hoi?
Hivi hujajiuliza ile industrial zone ya pale Kerege BYO?
Hivi hujajiuliza ule uwanja mpya kabisa wa ndege unaopangwa kujengwa kule BYO?
hivi huoni hivyo vinahitaji hiyo gas ?
Hivi hujui Dar es salaam gas inapita njia tunkuelekea BYO?
 
Muulize Pinda alisema kila kitu kimeisha na wamekubaliana mambo yoote ya msingi!imekuwaje tena?yaani wana Ntwara kama wanataka visasi na serikali wataumia bure!wajipange tena maana ule mkopo umeshatoka na watu wana maslahi pale ikiwemo uchaguzi ujao.....hawatakubali kamwe!bomba lazima litajengwa hata kwa kusimamiwa na kulindwa na jeshi miaka 50
 
Nina wasi wasi na uwezo wako wakufikiuri unachouliza ninin?au hujui upi usku upi mchana au ndo walewale siaf wa mafisadi wakujixafisha humu n ukweli m2pu pumba zako peleka facebook
 
Serikali inapotosha Umma,ila haisaidii hujuma zitakazotokea baada ya ujenzi ndiyo zitajibu hayo maswali vizuri.Tuliopo Mtwara ndiyo tunaona hali halisi,haiitaji kufungamana na upande wowote ili kutambua madai ya wanamtwara,KWENYE VITA YA HAKI USHINDI NI LAZIMA.
 
Gazeti la jambo leo limeandika "Mtwara wakubali gesi itoke" wanasema ni baada ya jeshi la wananchi wa Tanzania kwenda kurejesha amani, salamu ya wana mtwara imebadilika kutoka "Gesi haitoki" hadii kuwa "Gesi inatoka".

CC THE BIG SHOW
mbona tunaambiwa watu wengi wamekimbilia porini? na aliyeandika sms za uchochezi amekamatwa, sasa ni nani tena ameandika sms ya kukubali gesi kwenda dar. kama maneno hayo ni hila yatazidisha mgogoro, kwa nini kutumia hila? hila kwa sasa haifai maana kwa wakati huu hila ni pembe la ng`ombe hazifichiki, hivi kwa nini watu wanashindwa kuelewa hili?
 
Back
Top Bottom