Jamani wanawake mtatumaliza

Mangimeli

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
1,151
286
NNAOMBENI USHAURI WAKUU,nina ndugu yangu alioa kama mwaka ivi umepita, na kwa sasa wamebaatika kupata mtt mmoja,tatizo lililopo sasa ni kwamba yule shemeji yetu ni( postive) na alijua toka mwanzo ,nikisema mwanzo namaanisha ni kabla ya ndoa yao yani,ila mungu alivyo mkubwa broo ameenda kupima akakuta ni (negative) na amecheki zaidi ya mara mbili,alichokiamua yy ni kwamba hme kaama ila mtt anamuudumia na mtoto yupo salama,UAMUZI ALIOUCHUKUA WA KUAMA NYUMBANI NAI SAHIHI????au kama siyo sahihi afanyaje pia?nawasilisha kwa ushauri wenye kuleta tija.
 
usimtengeeee ndugu yangu usimtengee...sio vizuri kumkimbia mwezie alie athirika,chukulia upande wa pili wa shilingi angekuwaa yeye ndo mwanamke kamkimbia,inatiaa faraja pale unapo jua mwezako anakujali na kukupa tumaini jipya.sio kuishi nae ndo asiriki nae tendo au vitu ambavyo nirahisi kuambukizwaaa.je?kama tokea mwazo alijua mwezio muathirika kwaninii ali zaa nae.........
 
sasa arudi kufanya nini wakati tayari kashaokolewa na gonjwa....ila sasa namshauri jamaa yeye amfanyie kitu mbaya huyo mkewe kama vile kumtia kilema ili akome....maana ni muuaji sasa akimtia kilema atateseka kabla ya kufa. loh! kweli nimeamini tuwaheshimu hawa wanawake kama mama zetu lakini usishikwe masikio kabisa kwenye suala la mapenzi.
 
usimtengeeee ndugu yangu usimtengee...sio vizuri kumkimbia mwezie alie athirika,chukulia upande wa pili wa shilingi angekuwaa yeye ndo mwanamke kamkimbia,inatiaa faraja pale unapo jua mwezako anakujali na kukupa tumaini jipya.sio kuishi nae ndo asiriki nae tendo au vitu ambavyo nirahisi kuambukizwaaa.je?kama tokea mwazo alijua mwezio muathirika kwaninii ali zaa nae.........
labda ukunielewa kaka broo yye hakujua kama mke wake ni muathirika alikuja kujua baadae tena baada ya mke wake kujifungua, na shem alijua ali yake
 
labda ukunielewa kaka broo yye hakujua kama mke wake ni muathirika alikuja kujua baadae tena baada ya mke wake kujifungua, na shem alijua ali yake

Mmm kwa hiyo mkewe alikuwa haendi clinic au?
 
arudi tu kuokoa na maisha ya mkewe ila asile mzigo.Na akae hadi mwezi sita alafu akapime tena.
alafu sasa baada ya ayo yote pia mwanamke mwenyewe jeuri sana,alitakiwa awe mpole na aombe samaani
 
asimtenge jamani mana unaambiwa tenda wema usisubirie shukurani
then asimnyanyapae atamfanya mwenzie afufe haraka bure ..........
 
siujui nisemeje, maana ukivaa viatu vya mke unaona jinsi anavyohitaji faraja ya mumewe

na ukivaa viatu vya mume unaona hofu na woga alonao

ukivaa viatu vya mtoto anayehitaji mapenzi ya baba na mama?

nitarudi...................
 
makosa ya mwanaume
si mnaambiwa kila siku tumieni kinga na mkitaka kavu mpime kwanza??????

sasa anamlaumu nani?
 
Kila siku ni story za "Ndugu yangu" na "Rafiki yangu" si useme tu kuwa ni wewe, mbona hicho ni kitendo cha kijasiri sana???
 
Hii ilishamtokea ndugu yangu kabisa, mke alijijua muathirika akamtia kingi mwenzake....baada ya muda akawa anamfanyia visa na matendo mengi ya kinyama na alishafikia hatua ya kutaka kumdunga sindano yenye damu usiku akiwa amelala ili amuambukize lakini Mungu mkubwa ndugu yangu kustuka anaona mwenzake yuko na bomba!!, ndugu yangu alimsamehe bure na aliamua kumuuguza kwa upendo hadi kifo kilipompata. yule ndugu yangu hajaathirika kwa bahati nzuri...so tenda wema ndenda zako!kisasi ni cha Mungu.
 
usihame mangimeli,mwanaume hua hakimbii shida/matatizo! ni mkeo na mmefunga ndoa.
 
Kama amekula mzigo muda wote huo na hajapata....then aendelee tu kwani inaonesha jamaa ni sugu....
 
Asimhame aendelee kuishi nae, mbona ya kawaida hayo. Ila kwenye kuduu lazima watumie kinga.
Na huyo shem wako unasema ana jeuri, kivp?
 
Duh,usiseme wanawake tutawauwa,mnajiuwa wenyewe....hata biblia imesema, watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...tunajua kuna ukimwi unaoambukizwa kwa njia tofauti kubwa ikiwa ngono....utakuwaje salama,kapime au tumia kinga. Mwanaume hupimi, tatizo liko kwa nani?? kama hujipendi wewe mwenyewe,mwanamke ndo akufundishe jinsi ya kuishi??? Tumieni akili,tatizo mnatumia viungo vya uzazi kufikiri....amuache tu huyo dada,ila somo amelipata,na wengine wengi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom