Jamani: Tujikumbushe (2010) kuhusu zitto

Jamani: Tujikumbushe (2010) kuhusu zitto

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
Usalama wa Taifa wavamia CHADEMA

​

Na Saed Kubenea - Imechapwa 08 December 2010


VIGOGO kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wametajwa "kuingilia" Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI limegundua.
Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya idara hiyo zinaeleza kuwa vigogo hao wana mahusiano ya karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe.
Anayetajwa rasmi kuwa na mahusiano na Zitto ni Naibu Mkurugenzi wa TISS, Jack Zoka.
Kufichuka kwa taarifa za kuwapo "uswahiba" kati ya Zoka na Zitto kumekuja katika kipindi ambacho CHADEMA kimekuwa kikituhumu maofisa wa juu wa usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, kuibuka kwa tuhuma hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuchapisha taarifa mbalimbali za mawasiliano kati ya Zitto na Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya mawasiliano hayo, ambayo Zitto ameyapeleka kwa rais, aliyapeleka pia kwa baadhi ya watuhumiwa ufisadi nchini.
Kwa mujibu wa mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Kikwete; viongozi wa TISS walihusika, kwa kiasi kikubwa, katika kile alichoita, "Kuchakachua matokeo ya uchaguzi."
MwanaHALISI limefanikiwa kupata rekodi ya mshororo wa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka.
Kuna mwingiliano wa simu za mdomo na maandishi (sms) kutoka kwa Zitto kwenda kwa baadhi ya vigogo wa ngazi ya juu serikalini na TISS, hasa Zoka.

Nyaraka za mawasiliano zinaonyesha kuwa Zitto amekuwa akiwasiliana na naibu mtendaji mkuu wa TISS huyo zaidi ya mara tatu kwa siku.

Kwa mfano, Zitto na Zoka walifanya mawasiliano ya simu mara tisa hapo tarehe 8 Agosti. Simu iliyotumika katika mawasilino hayo, ni Na. +255756809535 ambayo hutumiwa na Zitto na +255754787550 ambayo hutumiwa na Zoka.
Wakati mawasiliano hayo yanafanyika, Zitto alikuwa katika maeneo tofauti.
Mawasiliano ya kwanza kati ya Zitto na Zoka yalipokuwa yanafanyika, simu ya Zitto ilisomeka kuwa alikuwa katika maeneo mbalimbali.
Mathalani, wakati mwingine simu ilikuwa ikisomeka kuwa yuko Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, Kigoma Urban (Mjini), Kigoma Rural (Vijijini), Mtwara, Uwanja wa ndege-Ilala, Oyster Bay, Ukonga, Upanga na katikati ya mji.
Gazeti hili halikuweza kugundua mara moja undani wa mawasiliano ya Zitto na Zoka.
Kinachofanya baadhi ya wachunguzi wa mambo kujenga shaka ni kwamba mmoja ni mwanasiasa, tena kutoka chama kilichopo nje ya utawala; na mwingine ni mtumishi wa idara ya usalama inayolalamikiwa kukandamiza upinzani nchini.
Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa mawasiliano kati ya Zitto na Zoka yalianza kupamba moto kuanzia tarehe 6 Agosti 2010, siku moja baada ya CHADEMA kuzindua kampeni zake za urais.
Kulingana na uchunguzi, siku hiyo, tarehe 6 Agosti, simu ya Zitto ilisomeka kuwa yuko Kigoma Urban.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, CHADEMA kupitia kada wake mashuhuri, Mabere Marando, iliibuka na lundo la tuhuma dhidi ya vigogo kadhaa wa serikali, CCM na idara ya usalama wa taifa.
Akizungumza na maelfu ya wananchi katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, Marando alisema wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT), ulifanywa na serikali na washirika wake.
Miongoni mwa vigogo aliodai kuwa walihusika kufanikisha wizi huo, ni rais wa sasa, Jakaya Kikwete, rais mstaafu Benjamin Mkapa, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa.
Akiongea kwa kujiamini, Marando alisema, "fedha za EPA ni wizi uliotiwa baraka na serikali ya CCM na ndio uliomsaidia rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005."
Kuanzia hapo hadi sasa, Zitto na Zoka wamekuwa na mawasilino ya mara kwa mara, na karibu kila siku huzungumza kwa simu.
Mawasiliano mengine ya mara kwa mara yalifanyika tarehe 7 Agosti 2010, siku mbili tangu hotuba kali ya Jangwani. Yalianza saa 10:17 na kuendelea tena saa 10:50, saa 10:51:31, saa 11:46:13, saa 12: 14:46, saa 12:26:48 na saa 13:50: 21.
Lakini Zitto alipoulizwa kuhusu sababu ya yeye kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na vigogo wa TISS, alisema hajui na hakumbuki lolote kuhusu kuwapo mawasiliano hayo na Zoka au mkuu yeyote wa idara hiyo.

Zitto amesema yeye, akiwa mwanasiasa na kiongozi, anazungumza na watu wengi kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ndani na nje ya nchi, lakini hajui kitu kuhusu usalama wa taifa.

Alipobanwa kuhusu mazungumzo yake na Zoka, hasa yale ya 3 Novemba 2010, saa nne na dakika 56 asubuhi, siku mbili baada ya uchaguzi kumalizika, Zitto alisema, "Siku hiyo nilizungumza na watu wengi sana. Siwakumbuki ni akina nani hasa."

Alisema, "Hicho ndicho kipindi ambacho matokeo ya uchaguzi nchini kote yalikuwa yakizuiwa ikiwamo kwetu Kigoma. Na ukumbuke mimi nilipigwa mabomu na polisi na usalama wa taifa. Nakumbuka viongozi wengi wa vyombo vya ulinzi na usalama walinipigia simu kunijulia hali na kupata taarifa ya kilichotokea," anaeleza.

"Sasa kama Zoka naye alinipigia siku hiyo sikumbuki; lakini nilipigiwa na wengi…Naomba uniambie kitu, hivi mnachokitafuta hasa ni nini?" aliuliza.

Katika njia ya kujitetea, Zitto aliuliza, "Mwanasiasa kuongea na wakuu wa vyombo vya usalama ni kosa? Maana, hata kama ningekuwa nimezungumza naye, kosa langu liko wapi?" alieleza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini.

Alipoelezwa kuwa haoni hiyo ni hujuma dhidi ya chama chake kwa kuzungumza na viongozi wa TISS na kile ambacho amekuwa akikizungumza kikiwa hakifahamiki kwa viongozi wake, Zitto alisema, "Sijawahi kukihujumu chama changu mahali popote, siku yoyote."

Jitihada za gazeti hili kuzungumza na Zoka hazikufanikiwa katika kipindi chote
cha mwishoni mwa wiki, kwa vile kila alipopigiwa, simu yake ya mkononi ilikuwa haipokelewi.

Hata ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kwenye simu yake saa 2:53 asubuhi ya Jumapili; ukieleza sababu za gazeti kuzungumza naye, haukujibiwa.

Aidha, tarehe 2 Novemba, siku moja baada ya kuzungumza na Zitto, Zoka alinukuliwa akikana madai ya Dk. Slaa, kuwa TISS imesaidia kuvuruga uchaguzi.

Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Zoka alisema, "Dk. Slaa amekuwa akidanganywa na watu wanaojiita maofisa wa usalama wa taifa."
Hata hivyo, kuna meseji mbalimbali kuhusu udini na uamuzi wa CHADEMA kususia hotuba ya rais Kikwete ambazo zilitumwa na Zitto kwa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ambazo zinadaiwa kuandaliwa na idara ya usalama wataifa.
Ujumbe huo unadaiwa kuandaliwa kwa ustadi mkubwa katika kukuza suala la udini na kuleta mtafaruki katika chama.
​
 
1st September 2010 12:26
MBUNGE mteule wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ameingia katika kashfa ya rushwa ya uchaguzi na huenda akapoteza ubunge, MwanaHALISI limeezwa. Mkono ametajwa kutoa mlungula kwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo hilo, Michael Makanja ili ampe nafasi ya kupita bila kupingwa.

Katika kufanikisha mkakati huo, Mkono inadaiwa kuwa alisaidiwa na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika chama hicho (jina tunalo) ili kumshawishi Makanja kujitoa.

Katika maelezo yake kwa maofisa hao wa chama, Makanja alikiri kupokea kiasi hicho cha fedha na kuongeza kwamba fedha zilizobaki alikuwa akabidhiwe na kigogo wa chama chake ambaye alikuwa nyuma ya mpango huo.

……Katika andishi lake hilo, Makanja anasema alishawishiwa na viongozi wake hao wawili na kigogo mmoja kuachia jimbo kwa Mkono kwa kile alichodai, "walimtisha kuwa angefukuzwa kazi."…

Hata hivyo, mawasiliano kati ya Makanja na kigogo huyo wa Chadema yanaonyesha kulikuwa na aina fulani ya makubaliano kati ya Mkono na kigogo. Kwa mfano, ujumbe wa simu ya mkononi uliotumwa kwa kigogo huyo kutoka kwa simu ya Makanja (namba tunaihifadhi) unasema, "Mzee ameshanikatia tiketi ya kwenda Dar. Sasa mhimize amalize kiasi kilichobaki, maana hali yangu kiuchumi si nzuri…." Mwingine ulisema, "Tumeshamaliza kama tulivyokubaliana." Ujumbe huo ulitumwa tarehe 21 saa 8:21 mchana. Ujumbe mwingine uliotumwa juzi Jumatatu, mara baada ya Makanja kuingia "mtegoni" ulisema, "Niko makao makuu ya chama. Nimewekwa chini ya ulinzi...." Akijibu katika namna ya kushtuka, kigogo huyo alijibu, "Wewe nani kakwambia uende huko… Watakuua. Siwezi kuja huko kukutetea...."
Source: Mwanahalisi

Link in JF: https://www.jamiiforums.com/tanzani...kwa-mgombea-wa-chadema-musoma-vijijini-3.html

1st September 2010 11:30
Zitto rafiki wa kweli wa Mkono mbunge wa Musoma Vijijini, TAFAKARI

Mjumbe wa NEC CCM na mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Nimrodi Mkono muda huu amesaini waraka ambao utapelekwa Bungeni kesho kuhusu kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu. Huyu ni mjumbe wa NEC ya CCM , tafsiri ya jambo hili nini maana yake .....
Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rod-mkono-asaini-kumwondoa-waziri-mkuu-8.html
 
wana JF heshima kwenu wakuu.
Mie binafsi nakubaliana na alicho kiongelea ndugu ndiyomkuusana. Ni dhahiri Zitto ni mnafiki, kigeugeu,mwenye kiburi,ndumilakuwili na mpenda sifa, hivyo siyo mpiganaji wa kweli na hafai kuwa hata kiongozi wa familia yake. Lakini ndiyomkuusana kwa hili la ndugu Mnyika umepotoka. On other hand wapambanaji twaweza tukafikiri ndiyomkuusana unatumiwa na mafisadi kuendeleza zile propaganda zenu. Kama ni kweli hiyo dhambi itakurudia na itakutafuna wewe na kizazi chako.
 
wana JF heshima kwenu wakuu.
Mie binafsi nakubaliana na alicho kiongelea ndugu ndiyomkuusana. Ni dhahiri Zitto ni mnafiki, kigeugeu,mwenye kiburi,ndumilakuwili na mpenda sifa, hivyo siyo mpiganaji wa kweli na hafai kuwa hata kiongozi wa familia yake. Lakini ndiyomkuusana kwa hili la ndugu Mnyika umepotoka. On other hand wapambanaji twaweza tukafikiri ndiyomkuusana unatumiwa na mafisadi kuendeleza zile propaganda zenu. Kama ni kweli hiyo dhambi itakurudia na itakutafuna wewe na kizazi chako.

Mkuu Mnyika Tena kafanya nini mkuuu?
 
Alichokifanya ndio kazi aliyoitaka na akapewa. Zitto hawezi kuomba msamaha huyu maana CCM itamshangaa na kumtapika. Hata suala la kutaja wenye fedha Switzerland ni moja ya mikakati yake ya kisiasa ya kutupa mashambulizi ya kupumbaza watu mapema kujihami au kutimiza lengo lake au la waliomtuma (political phony pre-emptive strikes). Kwa vile baadhi ya watu ni wavivu kusumbua vichwa vyao kutafakari kwa undani hayo mashambulizi anayoyafanya kama vile hoja binafsi basi tukafikiri kuwa Zitto ni Mtetezi wa wanyonge.

Hakuna hoja yoyote ya Zitto iliwahi kuzaa matunda mwishoni (kwa ajili ya wanyonge), kwani makusudi yake huwa si kuzaa matunda bali kunyanyua umaarufu wake na kuwalinda wale ambao wamemtuma. Mtakumbuka habari ya wenye fedha (jambo ambalo halikuwa jipya nchini Tanzania kusikika hata kusomeka) but was another phony pre-emptive strike ambapo aliishia kusema hakukuwa na haja ya kuwataja wahusika maana hana imani na Serikali kama itafanya chochote, mara akajisahahu tena akasema atashirikiana na Mwanasheria Mkuu kusaidia kutoa taarifa kwa kumtumia Confidant wake wa huko Switzerland na tena akasema atakwenda mwenyewe huko kuibua wahusika. Kwa kufanya hivi akateka mjadala wa wezi wetu na hivyo hakuna anayeshughulika na hilo, watu wanakaa wanaota eti tunamsubiria Zitto (mtu ambaye hana chombo chochote cha dola wala hata saini inayotambulika ndani wala nje ya nchi yetu kama kiongozi wa Serikali) eti ndiye apewe na mabenki ya Switzerlands majina ya Watanzania wateja wao wenye fedha huko, kiasi cha fedha na zaidi ya yote eti aweze kutueleza pasi na shaka njia walizozitumia kuzipata hizo fedha eti kazi ambayo yeye anaiweza lakini Serikali yetu haiwezi! Kusudi lake lilisha timia maana alipata umaarufu toka kwa wanaCCM na Wapinzani wengi at the same time in the house on that material day lakini siku zote tupo wachache tusiokubali kudanganywa!
Hata Leka dutigite haikuwa kwa ajili ya kuwanyanyua akina Kiba, Mwasiti, Banana, Chege, Diamond, Ommy wala wenzao bali kwa ajili yake ndio maana akasema eti aliguswa sana na Wabunge (aliokuwa amewateka pasipo kujua) walipochochewa kutamka hadharani kuwa hakutakuwa na mgombea Urais kama yeye. Siku iliyofuate,Zitto akaanza kuwadhalilisha wenzake kwa kusema analiamini gazeti lililoandika habari hizo kuliko Wabunge wenyewe akina Halima Mdee!
Je tayari mmeshasahu michango yake ya utetezi wa majenereta ya mafisadi yanayoifilisi TANESCO hadi leo na sisi wateja kubebeshwa gharama kubwa? Hebu nikumbusheni, matokeo ya ile Tume iliyoundwa na Rais na yeye akazawadiwa ujumbe; je mwishoni ilizaa matunda gani kwa wanyonge?
Sitashangaa kikao cha Bunge lijalo akazuka na hoja nyingine ya kuzuga watu. Anaweza kuzuka na hoja binafsi Bungeni ya kum-impeach Rais (kwa vile watu wanasema ni rafiki yake) na wasiohangaisha vichwa watashangilia na kusema "huyu ndiye Zitto asiye na uoga", lakini watu wenye akili watasema, subiri mwisho wa hiyo hoja binafsi tuone matunda yake mwishoni! Zitto ni kama Lowassa hasafishiki hata kwa the strongest bleaching agent. Watu wa namna hii, hata kama wangeweza kufanikiwa kuwanunua baadhi yetu; wakanunua na baadhi ya watu kwenye media ikiwemo na mitandao ya kijamii; wakaweza kutoa michango mikubwa sana makanisani, misikitini na kwa vijana-Masalia wenye njaa kwa mtaji wa umaskini wetu na ujinga wetu; Wallahi, wataibuka watu WASIODANGANYIKA NA WATAKATAA USALITI WAO NA WATAWAADHIBU VIKALI SANA SIKU ZA USONI!!
 
Back
Top Bottom