Jamani Swaga Zilikuwa Zamani

jrmlaurence

Member
Dec 2, 2010
80
125
Maendeleo yameua swaga nakwambia. Watu siku hizi wanajidaiii eti wana swaga, aa wapi! swaga zilikuwa zamani bwana. Enzi hizo za redio moja, mtu ukitoka kijijini na kuweza kuja kukaa mjini hata wiki moja tu, ukirudi unajikuta wewe ndiye mjanja wa kijijini, na kama ulibahatika kuja jiji la Dar es Salaam, basi watu wote wanakusikiliza wewe.
Unavyowahadithia jinsi ulivyopanda basi la ghorofa, au hata ulivyoibiwa mara baada ya kushuka kituo cha basi, na kila anayetaka kusafiri anakutafuta kukuomba ushauri jinsi ya kujilinda na wezi Dar es salaam.

Swaga zilikuwa enzi hizo ambapo mtu unakuwa ndiye mwanafunzi pekee aliyevaa viatu shule nzima, walimu wenyewe wanakuogopa maana lazima wazazi wako wana uwezo mkubwa. Hizo ndizo zilikuwa swaga bwana. Kila asubuhi kulikuwa na ukaguzi wa wanafunzi, mwalimu anakagua kucha, meno na lazima kila mtu aonyeshe mswaki wake.

Swaga ni pale wanafunzi watatu tu shule nzima ndiyo mna miswaki ya plastiki wengine wote wana miswaki ya miti, hapo utakuta mwalimu mkuu anawatoa mbele na kuonyesha miswaki yenu kwa wengine kama mfano na kuwaambia shule nzima; “What is this? This is a toothbrush, haya semeni wote toothbrush”, acha bwana.

Enzi ya Mwalimu hali ilikuwa ngumu, mtu ukiwa na ndugu yako yuko nje ya nchi, tulikuita Mamtoni, akakuletea suruali ya jeans basi wewe unaweza kuoa chaguo lako, na mji wote wanakutambua kuwa una jeans, enzi hizo kinaitwa ‘kigozi’.

Ukiwa na raba zilizoitwa ‘raba mtoni’, au baadaye ‘za kuchumpa’ mtaa mzima wanazijua hizo raba, siyo siku hizi kila nyumba watu wana raba, hakuna swaga bwana siku hizi, swaga zamani ndugu yangu.

Watu wengine hawajui kulikuwa na wakati kuwa na TV ilikuwa uhujumu uchumi, hivyo kuwa na TV ilikuwa boooonge la swaga, japo kulikuwa hakuna kituo cha TV cha kurusha matangazo, TV ilikuwa inaenda na video kaseti, basi kwenu mkiwa na TV, washambawashamba wote wa mtaa unawakaribisha washangae wakati unatafuta mita.

TV za siku hizo zilikuwa hazina rimoti, hivyo kuna kigudumu unazungusha hicho hata nusu saa ndipo unaanza kupata picha au sauti, lazima uzungushe mpaka sauti na picha zitokee pamoja, washamba lazima wabaki wanakodoa macho kukuangalia unapofanya maufundi yako, na baadaye kwenda kuhadithiana kwao..!

Swaga ilikuwa pale kwenu tu ndiyo kuna simu mtaa mzima, watu wanakuja kubembeleza simu zao zifikie kwenu na wanalipa wakitaka kupiga kwa ndugu zao, watu walikuwa wakipiga magoti wakati wanaongea na wakubwa zao kwenye simu, na watu wote wanajua mna simu maana waya wa simu ulikuwa ukionekana unaingia kwenu.
Swaga zamani bwana, baba yako akinunua Vokswagen hata kama mko watoto wanane na mama yenu na hausigeli juu, mnajazana kwenye kivokswagen kwa starehe kabisa na mzee anazunguka mitaa yote mjini washamba wanawaangalia.
Hizo ndo swaga bwana!

Nakumbuka swaga za mwalimu wangu wa hesabu aliyekuwa anavaa kaptura nyeupe shati jeupe, saspenda nyeusi zimeshikilia kaptura, soksi ndefu zimefika chini ya magoti, viatu vya ngozi vyekundu. Kwenye soksi alikuwa anachomeka kiko na peni aina ya BIC mbili.

Kwenye mfuko wa shati peni tatu, mkono wa kushoto ana leso nyeupe, mkono wa kulia ameshika kiboko.

Swaga zilikuwa zamani bwana siku hizi ni usharobaro tu
 

the american dream

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,761
1,225
Swagger bado zipo mkuu

These days zimehamia kwenye vitu vya ghali mf magari,cellphones,tabs nk

Akipita mtu na Range HSE/BMW X6 nk lazima macho yakutoke manake unakuta home mwenye gari kali ni Voxy

Wakati unajishow na Techno Phantom lako unamuona mtu anatumia Iphone 6 ambayo bei yake ni sawa na ada ya semister nzima chuoni

Wakati kwenu bado mnatumia TV ya chogo ya Hitachi na king'amuzi cha Zuku unaenda kwa mshikaji unamkuta ana 48 inches Tv ya LG

Aaaaaaa swagger bado zipo mkuuu
 

Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,523
2,000
Kwa maelezo yako hapo juu labda mimi ndiye sijui maana ya swagga:confused2:.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom