Jamani NMB ni uozo, balaa...

Muajiri wangu alitaka wafanyakazi wote tukafungue account NMB house pale azikiwe hili tuweze kuchukulia mishahara kwenye account zetu,
Mwajiri anataka wafanyakazi wafungue account NBC, hivi kwa nini vitu kama hivi vinakubalika kwenye hili li nchi letu? Kwa nini hakuna labor law inayokataza mwajiri kukuamulia mahala pa kufungua account?
 
hivi ni matawi kwa matawi nini mbona lile la morogoro rd halina matatizo

Morogoro RD wapo smart sana huwezi amini kama ni NMB, nilifungua Iringa-Mkwawa branch mwaka 2009 mpaka mwaka jana (2010) Octoba nilikuwa nazumgushwa kadi ya ATM. Kuna jamaa yangu akanielekeza nenda Morogoro RD, sikuamini kabisa kama ni NMB kwa huduma walizonipatia siku hiyo na ndani ya wiki tatu nishapata ATM card yangu tena walinitumiai sms kunijulisha kuwa ipo tayari!!

Siku zote tangu hapo nikiwa na shida na bank ya NMB nasafiri mpaka Dar kuwafuata Morogoro rd, maana vituo vingine sitaki hata kuwasikia
 
Leo nimeeenda tena, mmmh hayo maelezo niliyojaza....we acha tu, haya nimeambiwa niende saaa saba mchana leo nikachukue hio "account" sijui ni kubwa kiasi gani
 
Leo nimeeenda tena, mmmh hayo maelezo niliyojaza....we acha tu, haya nimeambiwa niende saaa saba mchana leo nikachukue hio "account" sijui ni kubwa kiasi gani

Mkuu nenda na canter kabisa maana hiyo account itakuwa kubwa sana
 
Back
Top Bottom