Jamani NMB ni uozo, balaa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani NMB ni uozo, balaa...

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lyampinga, Aug 30, 2011.

1. Lyampinga

Lyampinga Senior Member

#1
Aug 30, 2011
Joined: Apr 13, 2008
Messages: 143
Likes Received: 52
Trophy Points: 45
Muajiri wangu alitaka wafanyakazi wote tukafungue account NMB house pale azikiwe hili tuweze kuchukulia mishahara kwenye account zetu, lakini leo ni mwezi wa pili, napigwa danadana kuhusu kadi yangu ya kuchukulia hela kwenye ATM. Na mwezi wa kwanza nikaambiwa picha yangu haipo kwenye system kwahiyo siwezi kupewa pesa, na mimi nilipeleka picha wakati wa kufungua, sasa ilibidi meneja aanze ku sign karatasi nipewe hela, Yaani nashindwa kuelewa hii bank ya makabwela...NAWAOMBA WANA JF MSITHUBUTU KWENDA KWENYE HII BANK HATA KWA KUFUNGUA ACCOUNT

2. Henge

Henge JF-Expert Member

#2
Aug 30, 2011
Joined: May 14, 2009
Messages: 6,762
Likes Received: 78
Trophy Points: 145
miezi miwili unalalamika khaaaa!
wewe vp bank za tz zipo hivyo bana!
nenda hata NBC uone zoea matatizo!
acha uvivu by MAGAMBA!

3. jameeyla

jameeyla Senior Member

#3
Aug 30, 2011
Joined: Aug 12, 2011
Messages: 119
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
nmb ni uozo kweli kuanzia kwenye systems zao mpaka kutoa huduma kwa wateja yaani languaje baina yao na wateja ni zeeeero,,

4. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#4
Aug 30, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160
kuna wengine hata hawajui kadi zao zinafanana vipi lakini komaa tu utakuja ipata halafu baada ya miaka miwili imeexpire..

5. Lyampinga

Lyampinga Senior Member

#5
Aug 30, 2011
Joined: Apr 13, 2008
Messages: 143
Likes Received: 52
Trophy Points: 45
Yaani kwa kusema kweli nimejifunza na sidhani kama nitaweza kumwambia mtu akafungue account NMB, NIMEKOMA

6. B

Bakeza JF-Expert Member

#6
Aug 30, 2011
Joined: Jun 30, 2011
Messages: 328
Likes Received: 76
Trophy Points: 45

si bora ucheleweshewe kadi. Mi siku moja nimenunua muda wa maongez kupitia simu mtandao ukawa unasumbua nikawa narudia kama mara tano. Muda wa hewan sikuupata lakin kumbe wakawa wanakata hela. Siku naenda kuchukua balance sheet nikakuta wamekata hela. Ni wapuuz sana sio bank ya makabwela tena n majizi makubwa. Ipo siku hiyo bank nitahama

7. Rweye

Rweye JF-Expert Member

#7
Aug 30, 2011
Joined: Mar 16, 2011
Messages: 15,025
Likes Received: 3,051
Trophy Points: 280
Mie niliwahi kusema,kuondoa jina lakini NMB ni bank kama zingine na ina sifa zote za kuitwa sawa na benki zingine za kibepatari japo tofauti ni kwamba NMB inazorota sana...namaanisha ni less competitive

8. Jituoriginal

Jituoriginal JF-Expert Member

#8
Aug 30, 2011
Joined: Feb 8, 2010
Messages: 362
Likes Received: 5
Trophy Points: 35
LAKINI PROFIT YAO NI KUBWA KULIKO BANK ZOTE .

9. Elli

Elli JF-Expert Member

#9
Aug 30, 2011
Joined: Mar 17, 2008
Messages: 26,816
Likes Received: 10,106
Trophy Points: 280
Nimeiona hii thread nikaurukia haraka, maana mimi huwa sipendi kuanzisha thread but sikiliza hii; mwezi wa tatu mwaka huu 2011 nilipata kazi mahali fulani, nikaenda kuripoti mwezi wa nne tarehe fulani hivi, nikapewa mikataba na yote yanayohusika ila salary wao wanapitishia NMB account yangu ni NBC so ikabidi nianze kufuatilia NMB, nikaenda kwa Mjumbe akala buku mbili kwajili ya barua, mtendaji akala buku tatu jumla tano, kufika NMB Mlimani City wakasema hawataki zile barua wanataka barua ya mwajiri....nikarudi kwa mwajiri akaandika barua ya utambulisho, nikaenda tena wiki iliyofuata kufika palepale wakasema wanataka kitambulisho changu cha kazi/kadi ya mpiga kura au pasport, kwakuwa ndio nimeanza kazi sikua na kitambulisho nikabeba pasport kufika wakakuta jina moja ni tofauti (other given names) ambalo liko kwenye pasport wakagoma, nikaenda nikarekebisha, nikarudi tena, wakasema wanataka barua ya kunitambulisha toka kwa mwajiri na barua ya mwajiri hapa ikabidi niulize hio barua ya mwajiri aandikaje? mmmh nilivyojibiwa nadhani yule binti alikuwa na ..... haya nikaondoka. Nikaenda nikaja kurudi tena, kufika wala hawakushughulika hata kukagua fomu zangu wakasema hakuna mtandao/mtindio, nikanuna tu kimoyomoyo nikaondoka.

Nikahama tawi so ikabidi nikaanze process upya, kufika kule nako wakagomea ila barua ya mwajiri na barua ya kitambulisho cha muda wakati kitambulisho changu kinafanyiwa kazi wakasema wanataka vitambulisho tu vya kazi tu. mmh nikachoka, nikamia tawi la Magomeni sasa wiki tatu zilizopita (August mwanzoni) nikajiandaa vizuri sana this time nikaenda jumamosi bhana si unajua katikati ya wiki lazima uwepo kazini, kufka nikakutana na dada mmoja kavuta mdomo usiambiwe, akanijibu kwa kifupi sana, leo jumamosi hatufungui account asipojua kuwa yale matawi mengine yote nilikokwenda nilienda jumamosi, haya nikarudi nikaisubiri jumatatu (yaani jana) ikabidi nichelewe kazini nipitie magomeni tena kufika akanijibu simple tu, "leo hatufungui account hadi baada ya sikukuuu..." shenzi, nikataka nimtukane ila nikawa mpole tu, nikamkumbusha kuwa jumamosi alisema jumatatu, akawa ameshasahau kuwa alisema hawafungui account jumamosi yeye akasema eti alinijibu vile kwakuwa kulikuwa na matatizo ya network.....sasa nasubiri Idd iishe ijumaa niende sijui wataniambiaje huko. Yaani sikushauri hata uende huko, uende ukiwa umelazimika kwenda kama mimi, hebu imagine kuanzia April hadi september sijafungua account.

10. Lyampinga

Lyampinga Senior Member

#10
Aug 30, 2011
Joined: Apr 13, 2008
Messages: 143
Likes Received: 52
Trophy Points: 45
Mzee sasa cha kufanya na hii bank ni kumwandikia boss wao kwenye email hii Mark.Wiessing@nmbtz.com au ARJAN.MOLENKAMP@nmbtz.com...Sasa mwandikie kwa kizungu au kiswahili na matatizo ya hawa jamaa, mimi nimeshachoka na huduma zao na ijumaa naenda kuomba kwa boss ofisini kama naweza kuruhusiwa mshahara wangu ukaamishiwa CRDB...Sisi waswahili tunafanya kazi kwa mazoea sana na ninawaandikia bonge ya email.

11. Lambardi

Lambardi JF-Expert Member

#11
Aug 30, 2011
Joined: Feb 7, 2008
Messages: 10,306
Likes Received: 5,596
Trophy Points: 280
Ni kweli sijui wanadhani wao ni bora zaidi ya wa tanzania woote wanaoenda pale kufuata huduma inatia hasira sana sana wangejua bila wateja wao pale hawatahitajika kamwe!!wangekuwa na target kwa kila mtu na sectio yake wangewagombania wateja!!

12. Lyampinga

Lyampinga Senior Member

#12
Aug 31, 2011
Joined: Apr 13, 2008
Messages: 143
Likes Received: 52
Trophy Points: 45
Nadhani wanajitamba sana na wateja insi walivyo wengi, wewe waache tu, ushindani unakuja

13. Ndumbayeye

Ndumbayeye JF-Expert Member

#13
Aug 31, 2011
Joined: Jan 31, 2009
Messages: 4,784
Likes Received: 1,038
Trophy Points: 280
jamani wavumilieni hao ni walipa kodi wazuri

14. Mzito Kabwela

Mzito Kabwela JF-Expert Member

#14
Aug 31, 2011
Joined: Nov 28, 2009
Messages: 17,515
Likes Received: 1,685
Trophy Points: 280
Mkuu acha kutuongopea. Balance sheet unaifata Bank? Usituandikie mataputapu humu.

15. Mzito Kabwela

Mzito Kabwela JF-Expert Member

#15
Aug 31, 2011
Joined: Nov 28, 2009
Messages: 17,515
Likes Received: 1,685
Trophy Points: 280
Mimi nilifungua akaunti NMB Iringa tawi la Mkwawa jirani kabisa na chuo cha RUCO. Nikahamishiwa Dar kikazi, sasa kadi yangu imeexpire nikajua ni kama CRDB kadi ikiexpire unaenda tawi lolote wanakukong'oli picha mambo yanaendelea, wao wakasema kadi ishatumwa Iringa nijaze form nitakatwa sh 10,000/= eti kadi yangu italetwa Dar tawi la hapa Chuo Kikuu UDSM. Buku kumi yangu wamelamba na na kadi sijaipata mwezi wa sita sasa. Mimi NMB basi tena

16. Desteo

Desteo JF-Expert Member

#16
Aug 31, 2011
Joined: Jul 27, 2011
Messages: 446
Likes Received: 7
Trophy Points: 35
nendeni kwa makaburu basi

17. The Son of Man

The Son of Man JF-Expert Member

#17
Aug 31, 2011
Joined: Feb 9, 2010
Messages: 12,126
Likes Received: 1,705
Trophy Points: 280
Cheap is expensive!

18. B

Bakeza JF-Expert Member

#18
Aug 31, 2011
Joined: Jun 30, 2011
Messages: 328
Likes Received: 76
Trophy Points: 45

sorry mangi nilitaka maanisha bank statement

19. k

kasimba123 JF-Expert Member

#19
Aug 31, 2011
Joined: Apr 18, 2010
Messages: 1,318
Likes Received: 188
Trophy Points: 160
hivi ni matawi kwa matawi nini mbona lile la morogoro rd halina matatizo

20. k

kasimba123 JF-Expert Member

#20
Aug 31, 2011
Joined: Apr 18, 2010
Messages: 1,318
Likes Received: 188
Trophy Points: 160
au kila nikitaka huduma zao nakutana na wahudumu wazuri.

Loading...