Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 34,961
- 80,197
Ni kwa vile hana kazi ya maana ndio maana hiyo namba moja imekuwa ishu kwako. Embu jiulize endapo angekuwa na kazi nzuri wewe usinge penda kujua mshahara wake na matumizi yake? Acha unyanyapaa
Naona umeng'ang'ania kuuliza kama ni sawa yeye kuomba kusaidiwa mahari na gharama za ndoa. Tatizo ni wewe na sisi yeye dada yangu, una expectations za kuolewa na Mume mwenye hela,hapo ndio tatizo lilipo. Aliye kwambia kuwa huwezi kufunga ndoa mpka uwe na mamilioni ni nani? Ndoa ni jukumu la jamii iliyo kuzunguka,Nyie Si mmechangia wenzenu wengi tu kwenye harusi Kwahiyo na nyie mta changiwa.halafi Kwani wazazi wako wana mpango wa kumtajia mahari ya Milioni ngapi? Hakuna anaye shindwa kuoa kwasababu ya kukosa posa. Acha kumnyanyasa aisee,maisha ni kupanda na kushuka dada yangu.
Mke mwema humpa Moyo na kumsaidia mwenzake kwa hali na mali. Hiyo ndio dhana na ya maisha ya ndoa na mapenzi,kuwa karibu na kumpa support mwenzako hasa wakati wa shida.
Mwisho niseme kwamba binafsi sioni ubaya wa kujua mshahara wa mwenzako. Kama mnaweka siri katika mahusiano then nini maana ya kuwa mwili mmoja? Kuna sababu gani ya msingi ya kuficha kipato chako? Huoni kuwa inaweza kuwa na faida kama akijua ili endapo utakuwa ni mtumiaji mbaya wa hela akukosoe? Au mwenzetu una kiserengeti boy una kihonga?
"Upendo uwe kwenye kweli na kweli kwenye Upendo"
Kama inatosha vile. .ila mbona wanaume tunaoaga wanawake wasiokuwa na kazi