Hongera sana na endelea kumshikilia huyu YESU usimwache, wala usikatishwe tamaa na hao wanaokubeza, unajua binadamu saa zingine ni watu wa ajabu huwa sijui tunataka nini. mtu angetangaza ameamua kuwa jambazi au mchawi humu, bado watu wangembeza, sasa mtu ametangaza ameamua kuokoka watu wengine bado pia wanambeza!! songa mbele ndugu maisha haya ya duniani yana mwisho lakini roho zetu ndio zitaishi milele. sioni shida kujitangaza kwako kwani hata YESU alisema "Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni (Mathayo 10:32,33). keep on katika wokovu.