Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 51,046
- 22,249
Michael Momburi, Bukoba
PAMOJA na kuiwezesha Yanga kuvunja mwiko kwenye Uwanja wa Kaitaba na kuiba ubingwa mara mbili mfululizo, kocha Dusan Kondic amethikitishwa na vitendo vya uongozi wa mabingwa hao kuto thamini mchango wake.
Kondic amethibitisha kwamba hatakuwa kwenye benchi la ufundi timu hiyo itakavyoivaa Simba, Oktoba 31, na kuwashangaa viongozi wake kwa kutomjali na kushindwa kumlipa mshahara wa miezi mitatu.
"Naishi maisha ya shida sijalipwa fedha zangu miezi mitatu, nashindwa kuelewa hata viongozi wangu wanategemea nini, Yusuf Manji ana uwezo wa kunilipa madai yangu, lakini amekaa kimya wala hakuna lolote linaloendelea."
"Wanilipe fedha zangu tu nikapumzike, sijagombana na Manji wala Yanga, tumeishi vizuri kwa muda wote, lakini nashangaa kwa nini wananitesa kiasi hiki," alisema Mserbia huyo aliyeiwezesha Yanga kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo.
"Mimi ni kocha mwenye taaluma nitavumilia nione mwisho wake utafikia wapi, hiyo mishahara ni haki yangu kwa vile nimefanya kazi waliyonipa ningekuwa sikufanya nisingedai, najikuta kwenye wakati ngumu nipofikira suala hili."
"Baada ya mechi ya Toto nitakwenda likizo kwa muda nikirudi nitakabidhi majukumu yote kwa watakaokuja.
"Nitahakikisha mikataba yote ya wachezaji naiweka sawa kuhakikisha kila mmoja analipwa haki yake ndio niondoke sitaki kuacha matatizo Yanga kila mtu napenda anielewe sina tatizo hapa."
Alipoulizwa kuhusiana na mechi ya Simba alisema"Mkataba wangu unamalizika mwezi ujao siongezi. Hiyo ndiyo habari mpya na nina likizo yangu ambayo inabidi kuitumia ndani ya hiki kipindi kilichobaki.
"Ndio maana baada ya mechi na Toto Africa nitacheza mchezo mmoja Dar es Salaam halafu nakaa pembeni kupumzika. Hizo mechi zingine wataendelea wengine."
Kocha huyo amekuwa akilalama kutopewa ushirikiano na viongozi na ni kati ya sababu zilizopelekea timu hiyo kuyumba kipindi cha awali.
Mserbia alisema nimefungiwa mechi tatu kuwa kwenye benchi la ufundi, lakini hakuna kiongozi hata moja aliyekuwa tayari kunitetea hiyo imekuwa ni ishara nzuri kuwa hawanitaki tena.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega alisema kuhusiana na madai ya Kondic kuikacha timu hiyo kwa sababu ya kukataa kusaini mkataba mpya wataliozungumzia baada ya timu hiyo kurejea baada ya kucheza na Toto Afrikan.
Alisema kuanza kwao vibaya ni moja ya mchezo na ili kuleta ushindani lazima kuwe kuna mambo kama hayo katika soka kwa ujumla.
Tayari Yanga ina majina kadhaa ya makocha watakaochukua nafasi ya Kondic kutoka nchi za Ujerumani na Serbia. Kondic ataliacha benchi la Yanga chini ya Meneja Kenny Mkapa kwa vile Spaso Solokovisk hana mkataba.
Wakati huo huo; Kondic ambaye mkataba wake unamalizika mwezi Novemba amesema ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Kagera umeonyesha kwamba timu yake imeshakaa sawa.
Bosi huyo aliyetangaza kwamba hataki kuongeza mkataba na Yanga amesisitiza hatakuwa kwenye benchi baada ya mechi mbili zijazo.
"Ushindi dhidi ya Kagera umekuja wakati muafaka kabisa na umeonyesha kwamba Yanga ni timu bora na ambayo inacheza soka ya kufundishwa,"alisema Kondic.
"Timu imebadilika inacheza vizuri sana kila idara watu kama Nurdin Bakar na Godfrey Bonny wako juu sana sasa.
"Lakini hawa wachezaji wengine wako kwenye kiwango hicho hicho, nimefarijika sana na ushindi wa Kagera na najua ndio kitu kitakachoendelea kwenye mechi zijazo.
"Ninachoweza kukwambia ni kwamba Yanga inacheza kwa mikakati na mipango thabiti ndio maana unaona mafanikio ingawa kuna baadhi ya vitu vilikuwa vinaingilia."
Yanga kwa sasa ina ponti 12 huku mahasimu wao wakubwa Simba wakizidi kujikita kileleni baada ya kutopoteza hata mchezo mmoja na kuwa na pointi 18.
NB: TFF msaidieni apate haki yake