Jamani nilipeni mshahara wangu - Kocha wa Yanga

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Michael Momburi, Bukoba

PAMOJA na kuiwezesha Yanga kuvunja mwiko kwenye Uwanja wa Kaitaba na kuiba ubingwa mara mbili mfululizo, kocha Dusan Kondic amethikitishwa na vitendo vya uongozi wa mabingwa hao kuto thamini mchango wake.

Kondic amethibitisha kwamba hatakuwa kwenye benchi la ufundi timu hiyo itakavyoivaa Simba, Oktoba 31, na kuwashangaa viongozi wake kwa kutomjali na kushindwa kumlipa mshahara wa miezi mitatu.

"Naishi maisha ya shida sijalipwa fedha zangu miezi mitatu, nashindwa kuelewa hata viongozi wangu wanategemea nini, Yusuf Manji ana uwezo wa kunilipa madai yangu, lakini amekaa kimya wala hakuna lolote linaloendelea."

"Wanilipe fedha zangu tu nikapumzike, sijagombana na Manji wala Yanga, tumeishi vizuri kwa muda wote, lakini nashangaa kwa nini wananitesa kiasi hiki," alisema Mserbia huyo aliyeiwezesha Yanga kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo.

"Mimi ni kocha mwenye taaluma nitavumilia nione mwisho wake utafikia wapi, hiyo mishahara ni haki yangu kwa vile nimefanya kazi waliyonipa ningekuwa sikufanya nisingedai, najikuta kwenye wakati ngumu nipofikira suala hili."

"Baada ya mechi ya Toto nitakwenda likizo kwa muda nikirudi nitakabidhi majukumu yote kwa watakaokuja.

"Nitahakikisha mikataba yote ya wachezaji naiweka sawa kuhakikisha kila mmoja analipwa haki yake ndio niondoke sitaki kuacha matatizo Yanga kila mtu napenda anielewe sina tatizo hapa."

Alipoulizwa kuhusiana na mechi ya Simba alisema"Mkataba wangu unamalizika mwezi ujao siongezi. Hiyo ndiyo habari mpya na nina likizo yangu ambayo inabidi kuitumia ndani ya hiki kipindi kilichobaki.

"Ndio maana baada ya mechi na Toto Africa nitacheza mchezo mmoja Dar es Salaam halafu nakaa pembeni kupumzika. Hizo mechi zingine wataendelea wengine."

Kocha huyo amekuwa akilalama kutopewa ushirikiano na viongozi na ni kati ya sababu zilizopelekea timu hiyo kuyumba kipindi cha awali.

Mserbia alisema nimefungiwa mechi tatu kuwa kwenye benchi la ufundi, lakini hakuna kiongozi hata moja aliyekuwa tayari kunitetea hiyo imekuwa ni ishara nzuri kuwa hawanitaki tena.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega alisema kuhusiana na madai ya Kondic kuikacha timu hiyo kwa sababu ya kukataa kusaini mkataba mpya wataliozungumzia baada ya timu hiyo kurejea baada ya kucheza na Toto Afrikan.

Alisema kuanza kwao vibaya ni moja ya mchezo na ili kuleta ushindani lazima kuwe kuna mambo kama hayo katika soka kwa ujumla.

Tayari Yanga ina majina kadhaa ya makocha watakaochukua nafasi ya Kondic kutoka nchi za Ujerumani na Serbia. Kondic ataliacha benchi la Yanga chini ya Meneja Kenny Mkapa kwa vile Spaso Solokovisk hana mkataba.

Wakati huo huo; Kondic ambaye mkataba wake unamalizika mwezi Novemba amesema ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Kagera umeonyesha kwamba timu yake imeshakaa sawa.

Bosi huyo aliyetangaza kwamba hataki kuongeza mkataba na Yanga amesisitiza hatakuwa kwenye benchi baada ya mechi mbili zijazo.

"Ushindi dhidi ya Kagera umekuja wakati muafaka kabisa na umeonyesha kwamba Yanga ni timu bora na ambayo inacheza soka ya kufundishwa,"alisema Kondic.

"Timu imebadilika inacheza vizuri sana kila idara watu kama Nurdin Bakar na Godfrey Bonny wako juu sana sasa.

"Lakini hawa wachezaji wengine wako kwenye kiwango hicho hicho, nimefarijika sana na ushindi wa Kagera na najua ndio kitu kitakachoendelea kwenye mechi zijazo.

"Ninachoweza kukwambia ni kwamba Yanga inacheza kwa mikakati na mipango thabiti ndio maana unaona mafanikio ingawa kuna baadhi ya vitu vilikuwa vinaingilia."

Yanga kwa sasa ina ponti 12 huku mahasimu wao wakubwa Simba wakizidi kujikita kileleni baada ya kutopoteza hata mchezo mmoja na kuwa na pointi 18.

NB: TFF msaidieni apate haki yake
 
Soka la Tanzania daah, eti Yanga timu tajiri africa mashariki na kati, labda yanga timu pekee inayofaziliwa na fisadi Afrika mashariki na kati.. mme akinuna watoto wana lala njaa...wamekuwa watu wa kwanza kuleta wachezaji kwa gharama kubwa mwisho wa siku wana shindwa kuwalipa...Mfano kwa Lukunku mpaka akapeleka swala hilo tff, Owino walipo mtema akataka chake wakashindwa kumlipa nasikia njoroge nae anataka chake..hivi leo hii Manji akikamatwa kwa kesi ya kifisadi yanga si itashuka daraja...Kodic achape zake mwendo amekaa na timu miaka 2 lakini hakuna kituna alipewa fungu na fisadi bado akashindwa kutumia vizuri...kasajili wachezaji 11 wa kimataifa bado timu inache mchezo m'bovu afazali hata manyema..eti Nurdin Bakari na Godfrey Bonny wanacheza vizuri vipi hao akina kabogo...unanunua wachezaji 11 mechi sita hakuna aliefunga teh teh au mimi sina kumbux2....mwaka wa simba huu
 
funga mdomo wako wewe usiolijuwa litakusumbuwa fisadi fisadi fisadi kelele wewe we unawajuwa mafisadi katika historia ya soka la tanzania? nani fisadi zaidi ya sitta? alifisadi CDA Mamlaka ya ustawishaji kwa ajili ya kuipeleka Simba Brazil kwa pesa za walipa kodi ya maendeleo enzi hizo mwl. nyerere akamfukuzilia Mbali yeye na Aden rage Shenzzzzzzzzzzzzzy type
 
funga mdomo wako wewe usiolijuwa litakusumbuwa fisadi fisadi fisadi kelele wewe we unawajuwa mafisadi katika historia ya soka la tanzania? nani fisadi zaidi ya sitta? alifisadi CDA Mamlaka ya ustawishaji kwa ajili ya kuipeleka Simba Brazil kwa pesa za walipa kodi ya maendeleo enzi hizo mwl. nyerere akamfukuzilia Mbali yeye na Aden rage Shenzzzzzzzzzzzzzy type
Najua hiyo mimba inakusumbua, punguza jaziba....Binafsi sihitaji kujua ufisadi uliofanywa enzi za Mwalimu..maana sijui nilizurika vipi... tuzungumzie huu uliopo fisadi kaiba kajidai kujiingiza kwenye michezo tunajua ni fisadi tu, subiri siku kikiwaka atalazwa sana Nairobi eti ana malaria!?...
 
Na bado mtatukana sana mwaka huu,kwani kondic akiondoka sidhani kama mtapata kocha. ambae sio-msimamizi wa mazoezi kama alivyo kondik?
Hebu niambie anafundisha nini pale Yanga zaidi ya kutaka kuponda starehe New africa,kariakoo alipo sasa ni size yake kabisa.
Na subirini kichapo 31 /10/2009.- wafuliaji wakubwa nyie.
 
Na bado mtatukana sana mwaka huu,kwani kondic akiondoka sidhani kama mtapata kocha. ambae sio-msimamizi wa mazoezi kama alivyo kondik?
Hebu niambie anafundisha nini pale Yanga zaidi ya kutaka kuponda starehe New africa,kariakoo alipo sasa ni size yake kabisa.
Na subirini kichapo 31 /10/2009.- wafuliaji wakubwa nyie.
mwaka huu hawana chao maana walisha zoea mpira wa mezania na rushwa mwaka tumejipaga...wajipage msimu ujao na usajili wao wa mbonanza...
 
mwaka huu hawana chao maana walisha zoea mpira wa mezania na rushwa mwaka tumejipaga...wajipage msimu ujao na usajili wao wa mbonanza...
 
Hamna kitu mwaku huu nyie Yebo Yebo aka makanda mbili...mtakula vichapo baada ya vichapo...hakuna ushindi wa mezani wala nini...mnatia aibu ktika medani ya soka....wachezaji wote wenu wa kigeni wanaboa na timu zimejipanga vizuri hata sijui kama mtapata kucheza mechi za kimataifa kwani Azam, Mtibwa na JKT wamejipanga vizuri na huyu mbasha wenu Fisadi namba moja dawa yake imekamilika tuu...atakimbia Nairobi kila wakati...
 
LOL napenda mipira ya kibongo, mie hata uwanjani siendi tena!

Full ubabaishaji!
 
Alikuwa hwajui Yanga huyu, Ana bahati hakukaa sana hadi kufungwa na Simba, wangemfukuza kwa bakora!
 
Alikuwa hwajui Yanga huyu, Ana bahati hakukaa sana hadi kufungwa na Simba, wangemfukuza kwa bakora

KASOMA NYAKATI HUYU MSERBIA;LIJANJA....SASA YANGA JAMANI SIJUI HATA HUO MSHARA MNATAKA MKAMKATIE RUFAA TFF ILI ALIPWE AMA??
MAANA KILA KITU MWAKA HUU NI RUFAA HAWANA HELA ZA KUWAPA MOYO WACHEZAJI WANA HELA ZA KULIPA RUFAAA RUFAAA RUFAAA MNALO BABU
 
Wezi tuu wote hapo jangwani..wana angalia maslahi yao tuu...ngoja tu wakutane na mnyama..watakatiana rufaa wenyewe kwa wenyewe kutafuta mchawi...
 
huyu babu naye toka lini mshahara unadai magazetini and TFF watakusaidiaje?kwani TFF walikuwa witness wakati unasaini mkataba wako?kama hulipwi mshahara unangoja nini timka
 
funga mdomo wako wewe usiolijuwa litakusumbuwa fisadi fisadi fisadi kelele wewe we unawajuwa mafisadi katika historia ya soka la tanzania? nani fisadi zaidi ya sitta? alifisadi CDA Mamlaka ya ustawishaji kwa ajili ya kuipeleka Simba Brazil kwa pesa za walipa kodi ya maendeleo enzi hizo mwl. nyerere akamfukuzilia Mbali yeye na Aden rage Shenzzzzzzzzzzzzzy type
Ibwanaeeeeeeeeeeeeee,yani lengo lako lilikuwa ni kumtaja baba wa taifa tuu ili ufurahi,haya umeshamtaja nenda kanawe miguu ulale!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom