Jamani Nauliza Nipate Kujua..... Ilikuwaje?

Jamani Nauliza Nipate Kujua..... Ilikuwaje?

Athumani:
Alimkosea nini Mungu mpaka ikaibuka huu msemo: MUNGU SI ATHUMANI

Sikukuu ya Iddi
Ina nini hasa mpaka wakaidi ndo inakuwa kimbilio lao "MKAIDI HAFAIDI MPAKA SIKU YA IDDI"


Wewe umeanza kuwa mdini sana!
 
Mkuu kama maswali ya ngurumo nashindwa kuyajibu na hata ikulu uwa awawezi kuyajibu,sijui kama yako nitaweza.
Ngoja niende chimbo mkuu,nitarudi.
Ama kweli, Sulphadoxine si Ngurumo, na Mungu si Asumani......
 
Athumani:
Alimkosea nini Mungu mpaka ikaibuka huu msemo: MUNGU SI ATHUMANI

Mtemakuni
Huyu alipata adhabu gani mpaka huu mkwala ukaibuliwa "UTAKIONA CHA MTEMAKUNI"

Sikukuu ya Iddi
Ina nini hasa mpaka wakaidi ndo inakuwa kimbilio lao "MKAIDI HAFAIDI MPAKA SIKU YA IDDI"

Babu amejuiliza amekosa majibu.
Hebu msaidieni majibu apate cha kulonga na wazee wenzake kaunta ya juu Ijumaa hii wakati akigida Castle Milk Stout ya baridi kwenye glasi ya moto, iliyochemshwa.

Afu nawatakieni Wikiendi njema:

Msiendeshe mkiwa mmelewa, msifanye ngono zembe...tumieni kondom, ikibidi mzimeze kabisa kwa ajili ya kinga zaidi endapo mtabusiana na maulimi yenu

Ngoja kwanza nikamsalimie bibi ...halafu nimkubushe kuwafungia wajukuu dawa penzi shule zikifunguliwa!!
 
Nitakuadhibu na crate la Heineken za Kichina! watch ur steps usimkanyage shemejio Mzenji!
hebu fanya fasta, hiyo adhabu hata Mungu ambeye si Athumani atanisamehe

Babu naye.siku ya idi tutakula wali na nyama:
Hahahaha...we hatari sana.... Kumbe we mkaidi?

Ngoja kwanza nikamsalimie bibi ...halafu nimkubushe kuwafungia wajukuu dawa penzi shule zikifunguliwa!!
Mzee mwenzangu, hebu saidia hayo maswali...Huyo Athumani alikuwa nani mpaka iwe Mungu si Athumani na wala si Rashidi, JUma, Jacob au Kennedy
 
Huyo athumani atakuwa alikuwa mtu mbahiri sana...Kama angekuwa ni "she"...basi angekufa na utando wako!!
 
Huyo athumani atakuwa alikuwa mtu mbahiri sana...Kama angekuwa ni "she"...basi angekufa na utando wako!!
Mi nahisi alikuwa mbabe sana, alikuwa hashindwi kitu.... Anajiona kama Mungu, au labda alijiita Mungu.....mtaani wakawa wanamuogopa...sasa alivyokufa watu ndo............ Aaaah...kweli Mungu si Athumani
 
Aiseee hapa umenitega... majibu mbona ka ya kimbia vilee??
Alafu hio ya mtema kuni siku zoote nilifikiri kua ukipiga huo mkwara
maanake the intended utampiga na shoka kama mtema na kuni zake...lol
 
Aiseee hapa umenitega... majibu mbona ka ya kimbia vilee??
Alafu hio ya mtema kuni siku zoote nilifikiri kua ukipiga huo mkwara
maanake the intended utampiga na shoka kama mtema na kuni zake...lol
Hapo kumbe mwenzetu una ka-idea.... Mtema na kuni ndo kitu gani? Wallah kiswahili kimenipiga chenga....
 
Athumani:Alimkosea nini Mungu mpaka ikaibuka huu msemo: MUNGU SI ATHUMANIMtemakuniHuyu alipata adhabu gani mpaka huu mkwala ukaibuliwa "UTAKIONA CHA MTEMAKUNI"Sikukuu ya IddiIna nini hasa mpaka wakaidi ndo inakuwa kimbilio lao "MKAIDI HAFAIDI MPAKA SIKU YA IDDI"Babu amejuiliza amekosa majibu.Hebu msaidieni majibu apate cha kulonga na wazee wenzake kaunta ya juu Ijumaa hii wakati akigida Castle Milk Stout ya baridi kwenye glasi ya moto, iliyochemshwa.Afu nawatakieni Wikiendi njema:Msiendeshe mkiwa mmelewa, msifanye ngono zembe...tumieni kondom, ikibidi mzimeze kabisa kwa ajili ya kinga zaidi endapo mtabusiana na maulimi yenu
1. Mungu sio Athumani...sijui kwanini walichagua hilo jina ila msemo wenyewe unamaanisha Mungu sio mwanadamu.Wanadamu tunajulikana kwa uchoyo...wivu na roho mbaya...Mungu hana wivu na watu wake wala hatunyimi yale tunayostahili wala hatuchukii kiasi cha kutopenda tuendelee...kama unaweza unawezeshwa.Na ndio maana huu msemo hua unatumika pale mtu anapopata mafanikio.2. Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Iddi....ni wazi kwamba siku za sherehe hakuna ubaguzi...hata yule mkorofi wa wote atatritiwa kama wenzake...ubwabwa atapata...nguo mpya atavaa.Yani yule ambae katika hali ya kawaida kila mtu anamnyooshea vidole au anamkwepa siku ya sherehe wanakula nae ubwabwa bila matatizo!!3.Mtema kuni ngoja nimfikirie!Btw nimesign in kuchangia hapa tu kwahiyo nategemea Thanks na Likes za kumwaga!Weekend njema kwa wote nnaowapenda na nsiowapenda.MNAJIJUA!!
 
Back
Top Bottom