Jamani naomba msaada wenu wa sheria dhidi ya madai

Kuna mtu nilimwazima pesa kiasi cha mil 1.5 na kuweka dhamana ya nyumba kwa maandishi mbele mtendaji wa kijiji kwa makubaliano ya kulipa ndani ya kipindi cha miezi mitano, alifanikiwa kulipa laki mbili tu hadi muda wa ahadi kuisha na zaidi, hajalipa tena ili kumaliza deni hilo lililobaki...
ulichotoa ndio haki yako. katika misingi ya sheria kila mkataba, uwe wa maandisha au si wa maandishi ni sharti utimilizwe. Hata hivyo kama mkataba ni kinyume cha sheria au unakiuka misingi flani basi huo ni batili na hauna mashiko.

kwa suala lako sahau nyumba, zingatia Mil. 1.5 tu ulizo mpatia huyo mtu. dhamana si haki yako wa mkopo haufanyi dhamana ikawa haki ya mtu mwingine. kwa kifupi dhamana au hata riba si mali ya mkopeshaji.
 
Mkuu NAHUJA, Milamule. J na wengineo, napenda kuchukua fursa hii kuwapa somo dogo juu ya 'mikopo' baina ya marafiki, ndugu au jamaa. Kwanza, watu wengi hawafahamu kuwa kukopesha ni haki ya taasisi za kifedha kama benki. Hizo ndizo zenye haki ya kudai amana mfano nyumba, makato ya mshahara na kadhalika. Mtu binafsi hana hiyo haki hadi asajiliwe kisheria kuwa 'taasisi' ya kifedha...

Ndugu, nakubali kuwa watu hukopeshana kiholela lakini je, hakuna uwezekano wa mdai kumshitaki mkopshwaji kama yeye sio taasisi? Ukisema kumpeleka polisi au mahakamani kwa kujaribu, je huyu mtu aliyemkopesha hana haki popote kisheria kupata pesa yake?
 
Back
Top Bottom