Jamani naomba msaada wenu wa sheria dhidi ya madai

Milamule. J

Member
Nov 23, 2013
9
45
Kuna mtu nilimwazima pesa kiasi cha mil 1.5 na kuweka dhamana ya nyumba kwa maandishi mbele mtendaji wa kijiji kwa makubaliano ya kulipa ndani ya kipindi cha miezi mitano, alifanikiwa kulipa laki mbili tu hadi muda wa ahadi kuisha na zaidi, hajalipa tena ili kumaliza deni hilo lililobaki.

Nina haki ya kwenda mahakamani kudai haki yangu na kukabidhiwa nyumba endapo mtuhumiwa atashindwa kulipa au nifanye nini ili mtuhumiwa asitoe ahadi za kulipa kidogo kidogo?
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,159
2,000
Kwa hiyo sasa hivi hutaki pesa unataka nyumba yake? Nauliza kwa sababu sasa unasema hutaki za kidogo kidogo..
Je akikulipa 1m mara moja yoteeee.. iliyobaki bado utaenda mahakamani?
 
fred1149

JF-Expert Member
May 30, 2016
207
250
Kuna mtu nilimwazima pesa kiasi cha mil 1.5 na kuweka dhamana ya nyumba kwa maandishi mbele mtendaji wa kijiji kwa makubaliano ya kulipa ndani ya kipindi cha miezi mitano, alifanikiwa kulipa laki mbili tu hadi muda wa ahadi kuisha na zaidi, hajalipa tena ili kumaliza deni hilo lililobaki.
Nina haki ya kwenda mahakamani kudai haki yangu na kukabidhiwa nyumba endapo mtuhumiwa atashindwa kulipa au nifanye nini ili mtuhumiwa asitoe ahadi za kulipa kidogo kidogo?
Una haki ya kwenda mahkmni kudai hela yako pamoja na fidia juu. Kama utaweka wakili basi gharama zake atabeba yeye iwapo utashinda kesi.

Suala la kulipa taratibu ni suala ambalo mnaweza kukubaliana iwapo wewe utaona inafaa, lakini iwapo kama kavunja makubaliano yenu, automatically huwa ni lazima arudishe hela yote kwa mara moja.

Kuhusu wewe kuchukua nyumba, Hilo haiwezekani, ila mahakama inawez toa Muda wa huyo mtu kulipa in full, au siku let say, 14 na akishindwa, mahakama itateua court broker ndo aweze kuiuza kwa mnada. Hata hvyo na wewe unaweza kuwa ni sehemu ya wateja hvyo ukijichanga fresh unawez nunua katika mnada huo.
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,565
2,000
1) Unaweza kwenda mahakamani, kuiomba mahakama ili wakupe ruhusa ya kumiliki hio ardhi au wakupe idhini ya kuiuza ili upate pesa yako (na gharama ulizoingia zote).

2) Unaweza ukaiuza nyumba bila kwenda popote, ila baadae utasumbuka mwenye nyumba akiamua kukupeleka mahakamani mpaka case iishe. (Japo utashinda tu, kwasababu mnamkataba/makubaliano).

Njia namba moja ndio nzuri zaidi, mahakama ikitoa idhini umiliki/uuze hio nyumba hataweza kwenda kukusumbua kwengine popote, labda aende magogoni tu.

NB Kama jamaa ana mke/mume, na kauchukua huo mkopo kwako kwa kuweka bondi hio nyumba, bila kumshauri mke/mume wake. Mahakama inaweza ikauvunja huo mkataba na kuufanya uwe batili (kifupi; itakula kwako)
 
Milamule. J

Member
Nov 23, 2013
9
45
Kwa hiyo sasa hivi hutaki pesa unataka nyumba yake? Nauliza kwa sababu sasa unasema hutaki za kidogo kidogo..
Je akikulipa 1m mara moja yoteeee.. iliyobaki bado utaenda mahakamani?

Asante chief kwa mchango wako wa mawazo, maana yangu nataka kuepuka ahadi za malipo madogo madogo. Mimi sheria sijui, stori za mitaani ni kwamba mdaiwa anahaki ya kuahidi mahakamani kuwa ana uwezo wa kulipa hata elfu mbili mbili hasa mahakama inapogundua kuwa alishaanza kulipo malipo ya awali sasa hiyo itaisha lini. Sasa nifanye mini kuepuka hili?
 
Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,556
2,000
Mkuu NAHUJA, Milamule. J na wengineo, napenda kuchukua fursa hii kuwapa somo dogo juu ya 'mikopo' baina ya marafiki, ndugu au jamaa. Kwanza, watu wengi hawafahamu kuwa kukopesha ni haki ya taasisi za kifedha kama benki. Hizo ndizo zenye haki ya kudai amana mfano nyumba, makato ya mshahara na kadhalika. Mtu binafsi hana hiyo haki hadi asajiliwe kisheria kuwa 'taasisi' ya kifedha.

Niliwahi kuwa na kesi moja kwenye mahakama mojawapo hapa Dar es Salaam. Mteja wangu alishtakiwa na aliyedai ni mkopeshaji wake. Nikaweka pingamizi la awali la kisheria kwa hoja kuwa Mkopeshaji si Taasisi ya kifedha yenye uwezo wa kukopesha na kudai amana na/au riba. Tukasikilizwa na kesi ikatupwa kwa hoja kuwa Mkopeshaji si Taasisi ya kifedha ili aweze kukopesha. Taasisi za kifedha zinaratibiwa na sharia za kifedha hapa nchini.

Hoja yangu ni kuwa kukopeshana hufanyika kiholela tu. Katika uga wa kisheria, kama si taasisi ya kifedha, Mkopeshaji hawezi kumshtaki Mkopeshwaji kama ilivyo kwenye mada hii. Katika utaratibu wa kawaida, haiwezekani kwenda kuidai nyumba iliyowekwa amana mahakamani kwakuwa mkopo wenyewe tangu mwanzo ni batili kwakuwa haukutolewa na Taasisi ya kifedha. Kinachoweza kufanyika, katika Maisha yetu ya kawaida, ni kumpeleka polisi au mahakamani 'kwa kujaribu' kama atalipa au la.
 
Milamule. J

Member
Nov 23, 2013
9
45
Una haki ya kwenda mahkmni kudai hela yako pamoja na fidia juu. Kama utaweka wakili basi gharama zake atabeba yeye iwapo utashinda kesi.

Suala la kulipa taratibu ni suala ambalo mnaweza kukubaliana iwapo wewe utaona inafaa, lakini iwapo kama kavunja makubaliano yenu, automatically huwa ni lazima arudishe hela yote kwa mara moja.

Kuhusu wewe kuchukua nyumba, Hilo haiwezekani, ila mahakama inawez toa Muda wa huyo mtu kulipa in full, au siku let say, 14 na akishindwa, mahakama itateua court broker ndo aweze kuiuza kwa mnada. Hata hvyo na wewe unaweza kuwa ni sehemu ya wateja hvyo ukijichanga fresh unawez nunua katika mnada huo.

Nashukru kwa mchango wako. Kama nitasimama mwenyewe kuna uwezekano wa kunishinda ikiwa nina hati ya makubaliano iliyothibitishwa na serikali za mitaa na familia ya mdaiwa, kuna sababu zipi? na nizikabili vipi?
 
Milamule. J

Member
Nov 23, 2013
9
45
Mkuu NAHUJA, Milamule. J na wengineo, napenda kuchukua fursa hii kuwapa somo dogo juu ya 'mikopo' baina ya marafiki, ndugu au jamaa. Kwanza, watu wengi hawafahamu kuwa kukopesha ni haki ya taasisi za kifedha kama benki. Hizo ndizo zenye haki ya kudai amana mfano nyumba, makato ya mshahara na kadhalika. Mtu binafsi hana hiyo haki hadi asajiliwe kisheria kuwa 'taasisi' ya kifedha..

Nimekusoma sana, nashukru sana kwa ushauri huo. Barua ya makubaliano inaonesha kuwa nilimuazima kiasi hicho cha cha fedha na sio kumkopesha, vipi unanishauri nini kuhusu kauri hii bado sina haki kisheria au nifanye nini badala yake?
 
Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,556
2,000
Nimekusoma sana, nashukru sana kwa ushauri huo. Barua ya makubaliano inaonesha kuwa nilimuazima kiasi hicho cha cha fedha na sio kumkopesha, vipi unanishauri nini kuhusu kauri hii bado sina haki kisheria au nifanye nini badala yake?
Mkuu, kumuazima na kumkopesha hakuna tofauti. Tafadhali nisome tena. Nimeshauri umpeleke polisi au mahakamani 'kujaribu' kama atalipa.
 
Milamule. J

Member
Nov 23, 2013
9
45
Mkuu, kumuazima na kumkopesha hakuna tofauti. Tafadhali nisome tena. Nimeshauri umpeleke polisi au mahakamani 'kujaribu' kama atalipa.

Saw a mkuu, kwa maana hiyo hata nikipeleka kesi mahakamani, mdaiwa akakaidi kulipa sitakuwa na msaada zaidi. Naomba unisaidie zaidi nini kifanyike tofauti na hilo?
 
Regnatus Cletus

JF-Expert Member
May 26, 2018
1,114
2,000
Absolutely!
Mkuu NAHUJA, Milamule. J na wengineo, napenda kuchukua fursa hii kuwapa somo dogo juu ya 'mikopo' baina ya marafiki, ndugu au jamaa. Kwanza, watu wengi hawafahamu kuwa kukopesha ni haki ya taasisi za kifedha kama benki. Hizo ndizo zenye haki ya kudai amana mfano nyumba, makato ya mshahara na kadhalika. Mtu binafsi hana hiyo haki hadi asajiliwe kisheria kuwa 'taasisi' ya kifedha...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom