Jamani mna-manage vipi password zenu???

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,533
Habarini,

Ukubwa ni jalala jamani.
Sasa hivi nimegundua nina vitu vingi sana nashindwa kuvimanage. Mfano nina password za bank 3 tofauti, jamii forums, yahoo, hotmail, Vodacom Mpesa, facebook....nakadhalika.
Juzi nahitaji mtumia mtu pesa kwa M-pesa ya voda nimesahau pin no yangu siwezi kumtumia.....
Wakuu huwa haya ma-password munaya-manage vp? Je munakua na password moja kwa mambo yote yahitajiyo password? Na hii naiona ni risk au ?!....
Hem sheeeni ujuvi hapa
 
Kama uwezi kutunza siri ya nywila (password),basi ushauri ni kutumia nywila moja au zisizo zidi tatu...!

Nywila ya kwanza ni kwa ajili ya yanayo husu simu, namba mbili ni kwa ajili ya social network kama JF, Facebook a twitter, namba tatu ni kwa ajili ya kusoma email zako
kwenye hotmail au yahoo.

Binafsi ninazo nywila kumi tofauti tofauti, na ninazikumbuka zote
...!
 
Ziandike hizo password sehemu na uzifunge kwa "password" ili mtu mwingine asiweze ku-access...lol :teeth:
 
Ziandike hizo password sehemu na uzifunge kwa "password" ili mtu mwingine asiweze ku-access...lol :teeth:

Shida hapa ni kusahau..je akisahau password aliyofungia hizo zote itakuwaje..si ndo balaa kubwa tena?
 
unaweza kuwa na password hata Mbili au tatu lakini ukazitumia kote.
password ya Yahoo/hotmail Mpesa zinaweza kufanana
faceBook sijui nini na kadharika zikafanana pia mambo yanachanganya kweli kweli
Pole ila iwe siri yako binafsi nyie si mnapenda kuaminiana na rafiki/kaka/dada/ na kupeana password :A S-alert1:
 
Social network na emails-Tumia jina la kipenzi chako/mke la kinyumbani e.g kama ni mchaga manka1985 au mkapesa au mkashilingi.
Kwenye ATMS au unakohitajika tarakimu tu tumia mwaka wa kuzaliwa wa babu yako au bibi ya bibi yako.
 
Kama uwezi kutunza siri ya nywila (password),basi ushauri ni kutumia nywila moja au zisizo zidi tatu...!

Nywila ya kwanza ni kwa ajili ya yanayo husu simu, namba mbili ni kwa ajili ya social network kama JF, Facebook a twitter, namba tatu ni kwa ajili ya kusoma email zako
kwenye hotmail au yahoo.

Binafsi ninazo nywila kumi tofauti tofauti, na ninazikumbuka zote
...!

Ha ha haa, Binafsi nina NYWILA ( Nimeipenda hii kitu Nywila) tatu tu kama Ulibainisha mkuu E-PASTER
 
Kwa kweli paswords ni nyingi, wengine hata 30 zinazidi,kwani mbali ya hizo zilizotajwa kuna pia namba za kufungia/kufungulia masanduku na briefcase, passwords za frequent flyers airlines tofauti, password za kwenye uanachama mbalimbali kwenye mtandao, sites za kudownload majarida, muziki na vitu vingine kibao. Mi nilichofanya ni kufungua text file lenye passwords zangu zote na kujitumia kwenye email. Nikihitaji password kama nimeisahau nadownload hicho kifaili toka kwenye email. Ni hatari kulihifadhi hilo file la password kwenye laptop au PC - ikiibiwa imekula kwako. Ndani ya email hakuna kitakachopotea, labda mtandao ukosekane hapo ndiyo kasheshe, lakini siku hizi huwezi kushindwa hata kufungulia kwenye simu yako kama LAN au wireless havipo. Mbali ya passwords, hata documents zangu muhimu nimeziscan na kujitumia kwenye email ili hata kukitokea moto nyumbani nina vivuli vya vyeti vyangu muhimu ndani ya mtandao.
 
Habarini,

Ukubwa ni jalala jamani.
Sasa hivi nimegundua nina vitu vingi sana nashindwa kuvimanage. Mfano nina password za bank 3 tofauti, jamii forums, yahoo, hotmail, Vodacom Mpesa, facebook....nakadhalika....
Siku ya kusahau jina la mama watoto wako (kama unaye) ndio utatia akili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom