Mrejesho:Baada ya Kuibiwa na Mtumiaji wa Kupatana

Zungo

Member
Nov 24, 2015
18
32
Habarini....Itakumbukwa kuwa nilokuja hapa na Thread ambayo nilielezea jinsi yule jamaa alivyo niibia baada ya kunambia angeniuzia Mackbook pro kwa Laki 2.5! yule jamaa anae jifanya anatokea Njombe Ludewa

Wengi walinishauri na kunipa pole na kutoa mitazamo yao Thanks for that! Lakini pia ilikuja kujulikana kuwa yeye siye mwenye kitambulisho anatumia cha mtu

Tarehe 10/3/2016 ndio nilimtumia pesa hiyo laki mbili na nusu ile sa Tatu asubuhi na aliniahidi laptop nitaipata jioni sa 12 baadae akanambia nipata usiku wa sa nne hadi hapo sikuwa na shaka lakini nikaambiwa tena laptop itanifikia sa 9 kesho!
1458836422097.jpg

Tarehe 11/3/2016 aliniletea zengww hadi kufikia usiku ndo nikajua kuwa nimeibiwa,Nilimua lakini nilijipa moyo japo sikuwa na imani kama ipo siku nitapata hio pesa yangu niliumia sana nikasema let by gone be by gone! nimeibiwa kizembe kwa tamaa zangu na kuto kuwa makini

Tarehe 12/3/2016 niliamua kujaribu kuwapigia Voda na kuwaambia kuwa nimekosea kumtumia mtu pesa mtanisaidiaje? yule dada wa Voda aliniuliza namba ya mtu niliye mtumia na kiasi nikamwambia ni mtu wa tigo(Mpesa-tigopesa) yule dada akasema nimeona lakini umechelewa sana kupiga simu ilibidi siku ile ile upige now its too late lakini kwa sababu ni mtu wa mtandao mwingine siwezi kujua kama ametoa au vipi ila swala lako nitaliwasilisha idara husika lakini akanishauri pia nijaribu kuwapigia watu wa Tigo kama wanaweza zuia huo Muamala hapo ndo nilkata tamaa!

Nikawapigia wahudumu wa tigo wakaniambia Umechelewa sana kutupigia simu bahati mbaya pesa yako imetolewa na alie pokea ameshatoa hivyo hatuwezi zuia huo muamala! Nikawauliza so solution ni nini? wakasema labda uwe unajaribu kutupigia simu mara kwa mara ili ukiotea siku kaweka pesa tutakurudishia!

Nilikata tamaa kabisa na kusema sitawapia tena acha iwe nitolee nikampigia simu jamaa namba zote aliniweka blacklist! kesho yake nikawapigia tigo kuwakumbushia wakasema wao hawana uwezo labda voda ndo wakusaidia,nikawapigia voda tena wakanambia swala lako liko idara husika!

Nilikata tamaa na kuacha kabisa na kusema sasa basi ndo nikaja kuleta uzi hapa! Leo sina hili wala lile Sina hata mia mfukoni asubuhi ya sa 3 nikaona SMS ya mpesa ikionesha hela yangu imerudi leo tarehe 24/3/2016 sikutaka kuichelewesha nikaitoa
1458837095142.jpg

Nikajisemea Moyoni huyu jamaa kamuibia mwingine sasa hela yake imekuja kwangu! Thanks God now am happy na nina washukuru sana Vodacom kwa kurudisha 250 yangu! kikubwa jamani tuwe makini sana na mitandao lakini sijakata tamaa ya kumsaka huyu mwizi! Tuwe makini jamaa bado anaendelea kuiba

Asanteni!
 
Hahaha ndio ujifunze hakuna shortcut kwenye maisha na wahenga walisema bure ya ghali bora upite njia ndefu yenye uhakika utafika kuliko fupi isiyokuwa na uhakika
 
Kumbe JF inasaidia, Kumbe lile tatizo langu la muamala wa kununua ticket zafastjet kufail na hela wakakata ningelega hapa wangenirefund fatsa fasta,

Wenye matatizo ya hii mitandao muwe mnapost hapa ss :)
 
Hahaha ndio ujifunze hakuna shortcut kwenye maisha na wahenga walisema bure ya ghali bora upite njia ndefu yenye uhakika utafika kuliko fupi isiyokuwa na uhakika
Kweli mkuu tamaa iliniponza sanaaaaa kwa kupenda Slope jamaa akawa kaniweza
 
Duuu hivi yule wa kumuita mc pilipili kalipwa ya matangazo au an hisa pale tuumuulize kulikoni????
 
Dah huyo jamaa wa njombe ni noumaa... Alinitumiaga na picha za masimu kibaoo ili nijue ana piga na issue nyingine nyingine nimuamini hakujua kumbe ninae YESU moyoni Akili Kichwani na PESA yangu mfukoni.

Pole kaka na hongera kupata fwedha yako
 
Du kumbe hawa jamaa ni wa kukaa nao mbali pole mkuu matapeli wamejaa Sana mjini na kila siku wanabuni njia mpya za kuibia raia...
 
Mimi niliibiwa sio na huyu nikawapigia voda wakanipiga kiswahili nikaenda polisi hapa mwanza nako nikaishia kuwalipa laki mbili na nusu wamfatilie jamaa Dar nao wakala hela yangu,nimeona nitulie tu.Polisi mwanza kitengo cha cyber crime.
Alienibia yuko insta atanatumia nunua_simu nililipa simu ya Sony Xperia laki nne.
 
....TUPENDE KULIPA AFTER DELIVERY! SENDING MONEY ......
I DONT UNDERSTAND!
mtu hawezi kukutumia mzigo kama hujampa pesa ama hakuna agent katikati atakaehold pesa mpaka pale mzigo uwe delivered ndo pesa iwe released.

Kwa system hiyo hata kama mnunuaji hataridhika na mzigo pesa itashikiliwa mpaka mzigo urudi kwa muuzaji ndo pesa zirudishwe kwa mnunuzi.

Hivyo ndo makampuni makubwa kama ebay na alibaba wanafanya
 
Kumbe JF inasaidia, Kumbe lile tatizo langu la muamala wa kununua ticket zafastjet kufail na hela wakakata ningelega hapa wangenirefund fatsa fasta,

Wenye matatizo ya hii mitandao muwe mnapost hapa ss :)

Labda hukufuatilia mimi nilikula nao sambamba na walirejesha ingawa ni wabishi hakuna ten a it is never too late fuatilia mkuu
 
Hongera bro...achna na wale walikushaur uende kwa waganga kuroga..nakumbuka comment ya jamaa mmoja alisema mungu afanye wepesi and finally amefanya.
 
mtu hawezi kukutumia mzigo kama hujampa pesa ama hakuna agent katikati atakaehold pesa mpaka pale mzigo uwe delivered ndo pesa iwe released.

Kwa system hiyo hata kama mnunuaji hataridhika na mzigo pesa itashikiliwa mpaka mzigo urudi kwa muuzaji ndo pesa zirudishwe kwa mnunuzi.

Hivyo ndo makampuni makubwa kama ebay na alibaba wanafanya
***
GUARANTOR/ SAFET PROCURER!
 
Hongera bro...achna na wale walikushaur uende kwa waganga kuroga..nakumbuka comment ya jamaa mmoja alisema mungu afanye wepesi and finally amefanya.
Yah Mkuu ni kweli acha Tu kweli Mungu kafanya Wepesi
 
Back
Top Bottom