Jamani MKIBAKWA msioge!!!

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Madaktari wamewatahadhirisha watu wanaobakwa kwamba wakishatendwa hivyo wasioge au kubadili nguo kwa sababu kufanya hivyo kunapoteza ushahidi muhimu wa kumtia hatiani kisheria mbakaji.

Imeelezwa kuwa mtu akibakwa, anapaswa kwenda Polisi haraka kupata fomu namba tatu (PF3) na awahishwe hospitali ya wilaya ambako atapewa matibabu ikiwa ni pamoja na dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).

Dawa ya kuzuia maambukizi ya VVU inayojulikana kama PEP, inaweza kufanya kazi endapo tu mwathirika atapewa ndani ya saa 72 baada ya kubakwa kama kabla ya kubakwa hakuwa na maambukizi.

wasichana na wanawake wengi wanaofika hospitalini baada ya kubakwa na kunajisiwa, huwa wamepoteza ushahidi kwa kuoga na kubadili nguo walizovaa wakati wakibakwa. Wanawake wengi hufika hospitalini wamechelewa na hivyo kuwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya VVU.

Kesi nyingi za ubakaji zimekuwa zikikosa ushahidi wa madaktari, kwa sababu aliyebakwa anatakiwa kupelekwa hospitalini akiwa na nguo zake na ‘uchafu', kwa sababu ushahidi wa Polisi na daktari kuwa tendo la ubakaji limefanyika ni nguo alizobakwa nazo mwathirika.
 
sasa hata kama asipooga kama huyo mbakaji alitumia condom...would it really matter??

We kweli mtotowamjini. Hivi ulishasikia wapi mtu anabaka kwa kutumia kondomu? Anakuwa amejiandaa kiasi gani kubaka? Lol, this is really funny
 
Last edited by a moderator:
We kweli mtotowamjini. Hivi ulishasikia wapi mtu anabaka kwa kutumia kondomu? Anakuwa amejiandaa kiasi gani kubaka? Lol, this is really funny

kuna watu wanabakwa na ndugu zao, waume zao, marafiki...kuna wengine wanakua prepared.. kwani what is kubakwa? kubakwa ni pale mwanamke anaposema hapana hata kama alisema ndio kaabla na akalazimishwa...hiyo inaweza kutokea hata kwa mume wake...so whats so funny there:wink2:, uuliza mapolisi watakuambia kuna wabakaji wanatumia kondomu kwani wao hawajui kuna ukimwi
 
Back
Top Bottom