Jamani mbona google map wamekwishatoa hukumu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani mbona google map wamekwishatoa hukumu?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KIBURUDISHO, Sep 1, 2012.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Nasikiliza sasa hivi hotuba ya Mh,Rais kuhusu mpaka kati ya Malawi na Tanzania ndipo nilipoingia kwenye google nilichokiona kimenishtua kidogo hebu chungulia na wewe urudishe hapa majibu.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  google map sio legitimate authority kuthibitisha kuwa kile walichokichora kwenye ramani yao ndio kilivyo....google ni wadogo kuliko nchi....hata wewe ukianzisha web yako unaweza kuchora ramani ukaiweka hewani kuonyesha kuwa ziwa lote ni la tz na watu wakaiona hiyo ramani.
   
 3. m

  matubara JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Angalia google map utaona kuwa mipaka ya nchi zote iko katika continuous line isipokuwa Malawi na Tz kwenye ziwa uko dotted wakiwa na maana kuwa kuna dispute au mgogoro.
   
 4. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  KATIKA suala hili, mpaka kati ya MALAWI & TANZANIA ktk ziwa NYASA/MALAWI, TANZANIA haina hoja kabisaaaaaaaaa bali ubabe tu. KWANZA, MALawi haijawahi kupakana na TANZANIA bali TANGANYIKA, na ukisoma MKATABA wa MUUNGANO utaona kuwa TANZANIA haikuwepewa haki ya kurithi haki na mikataba ya TANGANYIKA: hizi ndizo hasara za kufanya mambo kwa kukurupuka (KAMA MUUNGANO WA TANGANY & ZANZ). KWA hiyo TANZANIA haina haki kisheria kusema inapakana na MALAWI. PILI, MALAWI wana hoja nzito, kwamba kuna mkataba unaowapatia haki ya kumiliki ziwa lote (mkataba wa JULAI 1, 1890), wakati TANZANIA wana hoja nyepesi sana kwamba, kimataifa pale nchi mbili zinapotenganishwa na maji basi mpaka huwa ni kati2 ya maji hayo: kisheria MALAWI wana treaty (ambayo ni sheria inasimamiwa na mahakama, mkataba) wakati TANZAN sisi tuna convention (ambayo ni maelewano tu,mahakama haiwezi kuisimamia). KWA KWELI hatuna hoja.

  IMANI yangu ni kuwa CCM wanataka kupindisha siasa za nchi kama BUSH alivyofanya kule MAREKANI: kama JK na CCM, BUSH alitangazwa kuwa the most incompetent presid ever, akaamua kwenda vitani na IRAQ kwa makusudi, lengo likiwa ni kwamba nchi inapokuwa vitani wananchi wote huungana nyuma ya kiongozi wao dhidi ya adui. VITA ikaanza, WAMAREKANI wakawa kitu kimoja, BUSH akashinda awamu ya pili kwa kishindo. CCM nayo inataka kufanya kama BUSH, wanataka 2015 waseme kuwa CDM haina uzoefu wa kuweza kukabidhiwa nchi "wakati huu wa vita." WATACHAGULIWA, lengo litatimia. JK anasema nchi haijiandai kwa vita, siyo kweli, kwa sababu (1) mwaka 2012/13 bajeti ya ulinzi imeongezwa hadi zaidi ya sh trilioni 1; (2) JKT nayo yaja; na (3) sasa hivi ninapoandika wanajeshi wanakusanywa kutoka pande zote za nchi nzima (kutoka kambi zilizopo MWANZA, TABORA, MARA, MOROGORO nk) kwenda RUVUMA, MBEYA mpakani na MALAWI... kama siyo kwa maandalizi ya vita ni kufanya nini?
   
 5. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Wewe ni mmalawo piwa. Unajifanya kushabikia cdm lakini tumekushtukia.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Na mimi nimemshtukia mkuu, eti "Tanzania haijawahi kupakana na Malawi kwa kuwa haikupewa mamlaka na Mkataba wa Muungano!" Amesahau kuwa Malawi yenyewe ilijulikana kwa jina la Nyasaland na hivyo 1890 Treaty haiihusu Malawi bali Nyasaland ambayo haipo! Tukiendana na argument za majina nafikiri hatutafika mbali!
   
 7. Lait noir

  Lait noir Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama mkataba upo au haupo, kama uliandikwa na wajerumani sijui na nani basi ni muhimu kuubadilisha sasa, haiwezekani ziwa lote liwe nchi moja bana, kwa hiyo hamna ruhusa kuvua samaki hata mita moja upande wa TZ? Au ukiogelea bichi uko nchi ya ng'ambo?
   
 8. n

  ngonani JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 1,371
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Jana nimeukuta huu mjadala sehemu watu wakidai kuwa kwa vile ni wazi sasa kwamba CHADEMA haizuiliki katika lengo la kuchukua nchi 2015,na hata kura zikichakachuliwa uwezekano wa kuwazuia haupo,basi njia pekee iliyobaki ni kuanzisha vita na Malawi ili ikiwezekana 2015 Uchaguzi uhairishwe sababu ya vita na pia Vita ujenga mshikamano baina ya wananchi,watasahau tofauti zao za kiitikadi na wote wataungana pamoja katika kukabiliana na adui yao mpya,hivyo wananchi watasahau kabisa na hawatakuwa na muda na M4C na by the time vita inaisha na ushindi kupatikana basi kete ya kisiasa itakuwa imepatikana,MIMI SIJUI KAMA HOJA HIYO INA MSINGI AU LA,TIME WILL TELL
   
 9. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #9
  Sep 2, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kama ccm watawaza kuingiza nchi vitani ili kuahirisha uchaguzi ili chama kingine cha upinzani kisichukue dola, basi magamba watakuwa wamevunja rekodi ya kuwa chama kikongwe chenye viongozi wasiofikiria kesho bali matumbo yao hapa duniani! Hapo hapo watawaza kutengeneza deal nyingine za kimagumashi ili wauze silaha! Hapo hapo watazalisha EPA na kagoda nyingine.

  Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums
   
Loading...