Jamani kwani ni lazima! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani kwani ni lazima!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mamzalendo, May 31, 2011.

 1. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jamani kwani ni lazima mtu ukifanya harusi utoe kadi za michango kwanini mtu usifanye harusi unayomudu badala ya kusumbua watu na mikadi ya michango! tena kibaya zaidi eti mtu anakuwekea kiwango eti kiwango cha chini laki moja hivi hii kwanza ya kumuwekea mtu limit inatoka wapi? kwa sababu unaniomba na hujui mimi natengeneza kiasi gani au matatizo ya upande wangu!

  mi wanajamii nadhani mtu afanye kilichopo kwenye uwezo wake sio kuwa kero kwa wengine kisa michango na hata kama utahitaji michango basi iwe kutoka kwa familia yako tu. hii sio fashion jamani!

  au wenzangu mna maoni gani?nipo tayari kuwa challenged juu ya hili!
   
 2. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,463
  Likes Received: 3,727
  Trophy Points: 280
  swala la kuchangia sherehe sio jambo baya lakini sherehe za sasa zimekuwa mizigo kwa wachangiaji
  wahusika wanataka kufanya sherehe kama ya mtoto wa mfalme
  ukichangia sh 30,000 kwenye harusi upati kadi ya mwaliko
  tumeshindwa kuchangishana kwa mambo muhimu yanayogusa jamii kama elimu, magonjwa nk
  unakuta mtu anachangia harusi 1m ukienda kumwomba msaada wa kupata dawa utapata majibu 1000   
 3. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Afadhali umeona Black,inakera kwa kweli yaani hata mtoto akifaulu ndugu wakiambia watoe kdogo kdogo hawatoi lakini harusi anatafuta sa ina maana gani?inabidi tubadili mitizamo kdogo then hzo pesa zifanye mambo mengne,
   
 4. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Sijaoa lakni kwakweli michango inaharibu bajeti sana tu. Rafiki yangu alishangaa sana kusikia mtu akitaka kuoa tunachangishana kufanya sherehe kubwa. Kule kwao Zimbabwe hamna kitu kama icho. Unataka sherehe ya kifahari tafuta pesa mwenyewe andaa pati watu waje wanywe na kula waondoke zao.
   
 5. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Nafikiri kuchanga sio lazima na waweza tu kumwambia mhusika kuwa hutaweza kumchangia kwa sababu utakazozitoa.
  Tatizo watu nafanya michango ni upatu nae zamu yake ikifika atachangiwa kitu ambacho sio sahihi!
  Usichange na usipochangiwa elewa tu kuwa tunatofautiana.
  Hapa ninaandika kuna send off na Kitchen party 2, ya binamu na mtoto wa dada,
  Still kuna harusi ya mtoto wa mama mkubwa, Rafiki yangu nae ana harusi ya mdogo wake wa kuzaliwa naniomba mchango,
  Jamani, tunatafuta hela kwa ajili ya kuchangia watu sherehe?
  Sorry!
   
 6. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mie mwaka huu 2 nina watu kumi halafu kuna mtu wa kwanza kasema yeye minimum laki kamshahara kangu ndo hivyo,hivi ndio nini embu ona Da Pretty hao wote ni ndugu wa karibu so kama laki 2 2 hivi, tutaendeleaje?
   
 7. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mie kuna couple walinifurahsha waliomba wasaidiwe waanze biashara watu wakawahawaelewi,wakatangaza wanaoana watu wakatoa,siku ikafika wakaenda kanisani ibada imetoka 2 wakasema tunashukuru kwa kufika kwenu huu ndio mwisho wa siku,hao wakaenda honeymun sa hv wana mabiashara yao 2,kwani nini tendo kubwa katika harusi?
   
 8. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mimi nilishaacha kuchangia, na zamu yangu ikifika sitaomba mchango wa mtu. Nitakwenda church na mchezo kwishney.
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,087
  Trophy Points: 280
  Cha ajabu hyo michango inaishia kununua bia,pilau,kukodi magari ya kifahari na heinken,kumbi za gharama n.k...sasa jamani starehe za hvi za nini,nadhani tunauendekeza wenyewe huu uchafu,kama mtu anakupangia mpaka pesa hilo siyo ombi tena,hii ni "POLITE COMMAND",tupigane chini tuone kama mambo hayatabadilika
   
 10. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nafikiri nimejifunza kweli mi kwanzia sa hivi sichangii mtu tena na hii itamaanisha hata harusi za watu sitaenda ni heri kuliko kutoa huku nanung'unika, halafu eti mi nina swali kwani harusi na bites za ukweli tu si harusi kwani lazima machakula sa nyingine hata hayajaiva vizuri?
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
 12. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
 13. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ila pia na watu wenyewe ndo wanaohamasisha hii habari ya kuchangiana.usipomwambia mtu unaoa au kuolewa mkikutana anaanza lawama. i had a best wedding ever. just me na familia na close friends tu. na ilikua njema sana.no head ache za kijingajinga. na mtu akinihoji y sikumwambia. jibu ni simple.... nilitaka kutimiza agano langu na mpendwa wangu tu hayo mengine mapambo tu.

  afu angalia hata wenye harusi kwa kutamani kulisha matumbo meeeengi wanabaki na madeni hata mwaka mzima. yani maana ya ndoa hakuna, ishu ni umati kiasi gani ulikua ukumbini,vyakula vilikuaje zawadi kiasi gani.yaaani mashindano tu afu kesho yake unasikia mke kwao.

  watu wanapaswa wafanye kwa kadri ya uwezo wao. kusumbuana huku kila siku vikao na kadi mmmmmh.sijui tutafika wapi.
   
 14. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hongera sana ndio inavyotakiwa, if i get this chance to get married for real i will convince my boy for just a small but sweet party with just close family. haya mashindano wala hayalipi. big up sana.
   
Loading...