Jamani huyu ndugu yetu yupo wapi?

Kijana wa Ifoza

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2025
Posts
1,219
Reaction score
2,399

Picha: Watanzania kwa Upendo walitoa kikombe chenye ujumbe "NIOE TESHA"

Mnamo Oktoba 2025, kiongozi mzalendo Kapteni John Charles Tesha alijitambulisha na kutoa video iliyosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii. Alifanya hivyo wakati wataalamu wa CCM katika medani za sinema wakiwa hawajamaliza kutengeneza script ya sinema ya Oktoba 29.

Katika video hiyo, Kapteni Tesha alizungumzia masuala mengi mazito ya kitaifa, ikiwemo viongozi na matukio ya nyuma. Alipinga vikali matumizi ya nguvu dhidi ya raia, akaonya askari dhidi ya kuwafyatulia risasi wananchi, na kuulizia masuala mbalimbali ya kisiasa.

Hata hivyo, kabla ya Uchaguzi Mkuu, alipotea kabisa na hajasikika tena. Je, na yeye amekuwa Nchimbiji na Polepoleji? Swali linabaki: Kulikoni? Na je, nawauliza wana-JF, huko Barracks kuna wazalendo wengine kama huyu?

 
Ila ukikosoa pesa unadharaulika sana

Inamaana wanaume wengine hamuwaoni sio?
 
Ila ukikosoa pesa unadharaulika sana

Inamaana wanaume wengine hamuwaoni sio?
Hapa kuna majibu yako yaliyoboreshwa vizuri ili yawe na mtiririko mzuri na hoja zenye nguvu, huku font ikiwa imebaki katika mtindo wa Italics kama ulivyoomba:
Hujaeleweka una maana gani kiongozi! Kama unamaanisha hao waliotengeneza hivyo vikombe na mito hawana akili, unakosea sana. Hakuna anayesema duniani hakuna wanaume wengine, ila jamii inamuona Tesha kama mwanaume shujaa aliyesimama kishujaa kusema ukweli.
Kumbuka hata kina Mauzinde na Anko T nao ni wanaume pia, lakini kila mmoja anaheshimika kwa kile anachosimamia. Suala hapa halihusiani kabisa na kukosa pesa au dharau, bali ni heshima kwa ujasiri alioonyesha.
 
No sijasema waliyofanya hivyo hawana akili no,

Nawaalika tu ke kwenye mjadala.

Tesha namkubali sana.
Word
 
Mbona alikwisha olewa kule Mombasa, subiri atakapoachika.
 
Akina Kavulata hawajapita naye iulalo ulalo kama wengine tusiojua hatmà zao?
 
kwani alikua wap gentleman hiyo ndugu yenu?🐒
 
Kwasasa yupo Tanzania kaungana na familia yake upya

Baada ya kuomba msamaha kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Kaona ni ujinga kujificha na kuishi kwa kuomba
wenzie pesa !!

wkt mwenyewe nguvu anazo za kufanyakazi
Zaidi kakumbuka familia yake ndio kaona yaishe apate kuwa raia mwema!!!

yupo Tanzania kwasasa hataki tena arakati ushuzi!!!!
 
Kwasasa wana alakati wawili wa kiume wamesanda wamelejea Tanzania kwa kuomba msamaha

Bahati nzima Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hana matatizo yoyote na wenye kukumbuka nyumbani mwenyewe ni Mama pia Watoto wameona wamekosea kweli wanajutia kwanini wasilejee nyumbani

Kipindi cha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni Kipindi kizuri zaidi kwa wale wote wamekimbia Tanzania kwa midomo midomo yao japo wangeweza kuomba msamaha na kuondosha kiwingu mbele yao ,,

Babako mzazi anakufa wewe
unashindwa kuja kumzika nyumbani kwenu Tz !!!
watakufa na wengine bado utashindwa kuja yote yanini ¿¿¿¿¿¿
 
Ni ujinga kufanya arakati chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwasasa

Wangekuwa vichwa vyao sio maji
Wangeweza kumaliza mikwamoyao Tanzania chini ya Rais wasasa,
 
Yupo huko sehemu salama , Alipita mpaka wa Namanga ndio sababu ya watu wa Namanga kufanyiwa pangua pangua kwa unaoitwa “uzembe”

Issue ya oktoba ilikuwa deep wazee, nashangaa wanajitoa ufahamu kuhangaika na Lissu na CDM wakati wahusika wapo…..
 
Inaonekana wewe ni mafwele kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…