Jamani huu ni ushamba au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamani huu ni ushamba au?

Discussion in 'Matangazo madogo' started by rbsharia, Sep 21, 2011.

 1. rbsharia

  rbsharia Member

  #1
  Sep 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania wenzangu, inasikitisha sana mtu kuona au kuokota kitu cha mwenzako lakini unashindwa kukithamini au kukipeleka kwenye chombo cha usalama. Angalia tofauti;

  1. Kizazi cha zamani (Babu na Bibi zetu)
  Zamani enzi za babu na bibi zetu walikuwa wakiokota hata funguo moja walijaribu kuiwasilisha kwa polisi au kuiweka katika eneo la wazi karibu na alipoiokota ili kila mtu aweze kuiona hadi habari zinamfikia mmiliki wa funguo hiyo kulingana na alivyotangaza kupotelewa na funguo yake.
  2. Kizazi cha .COM
  Siku hizi kizazi cha .com au kizazi cha warembo na masharobaro. Mtu anapopoteza kitu, lazima kitaokotwa na hakitapelekwa kwenye sehemu ya usalama (mfano: radio, mitandao au polisi) bali kitahamishwa kutoka katika eneo kilipoangushwa na kupelekwa mahali ambapo muhusika wa kitu hicho ni vigumu kukipa, au hata akikipata basi hakifai tena kutokana na mikiki mikiki.
  Kwa mfano; 1. Utamuona mrembo au sharobaro ameokota funguo, badala ya kuitangaza ili apatikane mwenye funguo, eti bila kufikiria
  ataiongeza katika funguo zake.....!!!! We mrembo / Sharobaro, hiyo funguo itakusaidia nini kama sio kujiongezea mzigo?
  2. Mtu anaweza akaokota kadi ya bank (ATM CARD), badala ya kuitangaza ili atafutwe mmiliki wa hiyo kadi, eti utamuona
  anaitoboa na kuigeuza kibeba funguo (Key holder). Unataka mwenzako akale wapi kama kadi yake ukiiharibu?
  JE, tutawabadilishaje hawa wenye tabia kama hizi ili tuishi kama zamani?
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu kuwabadilisha kwani kishakua kizazi cha nyoka
   
 3. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hicho ndio kizazi cha kishariboro
   
 4. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  promote values. siku hizi ukiwa mwizi unonekana mjanja. ukimshangaa malaya wewe ndio unaonekana mshamba. Ukikataa rushwa unaambiw utakufa masikini.
  Kwanza watu waelewe nini kibaya na nini kizuri. Ujanja ni kuweza kuwa na amani na Mungu wako, jirani wako na nafsi yako mwenyewe. kitu chochote nje ya hapo ni ujinga mkubwa.
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hivi hadi leo hii watu huwa wanaokota vitu,mana nina muda sana hata sh 100 sijawahi okota jinsi hali ilivo mbaaaya
   
Loading...