Jamani hii ya Kamanda Kova imekaaje?

Kama ana heshima ampigie basi Dk. Slaa kama haujasikia another version of story, labda aseme to the late Kanumba was secret service na alikua na cheo kuliko yeye, otherwise babu kachemka mazima

Mkuu, kamanda kova ampigie saluti dr slaa wakati gani?
 
kova hajakosea.., polisi na jeshi, wote wanapaswa kum-salute marehemu YOYOTE..., awe na cheo asiwe na cheo.., ni heshima anayopewa marehemu..,

haku-salute kwa sbb ni kanumba, amesalute kwa sbb yule ni marehemu na anapewa heshima yake....,

kama hujui kanuni na nidhamu za kijeshi usibishe vitu usivovijua.., lakn ku-avoid kuchanganya watu wasiojua haya mambo ndio maana servicemen wengi wanaenda na civ clothes,

Ile ni nidhamu ya kijeshi kwa marehemu wetu si kwa sbb ni kanumba, nada!
 
Huyo mzee alikuwa anatafuta jinsi atakavyotoka kiaina. Kanumba alikuwa na title gani hadi kupigiwa saluti?

Kwa maoni yangu kamanda Kova hakuwa sahihi kuipigia salute maiti ya Kanumba.

Sababu salute ni salamu au heshima ya kijeshi kwa mtu aliyekuzidi cheo au mamlaka.

Kova anajua miko ya salute lakini nadhani alipitiwa tu.
Kama kitu haukifahamu kwa kina hakuna haja ya kubishana..... Waache wenye uelewa na jambo watoe ufafanuzi.

 
Mzee Luhala kaeleza vizuri lakini bado tusiokuwa wajeshi hatumwelewi.

Ndio maana wengine hata hawajui kwa nini tu maskini!
 
Huu ni ushenzi/ujinga wa kutojua mamlaka. Najiuliza, Kanumba alikuwa na mamlaka gani Tanzania? Hakuchangia chochote kwenye pato la taifa na hakuitangaza Tanzania kwenye sinema yeyote aliyetoa/kucheza halafu leo hii anapigiwa saluti kana kwamba yeye ni kiongozi wa nchi? Hapa sasa muone jinsi hii nchi ilivyo na viongozi feki. Haya ndiyo matokeo ya kuroga ili upate cheo wakati kazi huijui. Jamani, tutafika kweli?
 
Kwa uelewa wangu ambao si shaka nao heshima ya mwisho inayotolewa kwa mwili wa marehemu na skari jeshi,polisi,au magereza anapokuwa amaevaa unifomu na saluti ya kijeshi. Hii haitegemei kama marehemu wakati wa uhai wake alikuwa askari au kiongozi wa kiserikali, hii ndiyo protocali ya vyombo hivyo wakati wa msiba. so kamanda kova hakukosea na alifanya hivyo kama heshima yake kwa marehemu na sio kwa sababu ya uwepo wa viongozi.
 
Jaman watu hebu eleweni. Jeshini hakuna shikamoo, za asubuhi wala habari gan. Kule saluti tu. Kova hajakosea hata kdogo.
 
Jaman watu hebu eleweni. Jeshini hakuna shikamoo, za asubuhi wala habari gan. Kule saluti tu. Kova hajakosea hata kdogo.
 
hata wewe ujui maana ya salute, kova kakosea,unatia aibu kujifanya mwanajeshi
 
Kipara Kikubwa umechemka, haijalishi kama kuna uwepo wa Rais, Makamu, Waziri Mkuu au hata waziri kwani hata mimi na ujuzi wangu wa kawaida nafahamu ni sahihi kwa askari kutoa heshima ya saluti kwa maiti anapokuwa kwenye sare rasmi. Ufafanuzi wa Luhala ni sahihi na nimeshashuhudia mara nyingi hilo likitendeka si Tanzania tu bali hata nje ambapo bila ya uwepo wa viongozi wakuu wa nchi maafisa waliovalia sare walitenda hivyo kwa maiti ambaye ni raia. Kwa hapa nyumbani nimewaona JWTZ wakifanya hivyo na ni lazima nikiri kwamba nilikuwa sijawahi kumwona Polisi, magereza au uhamiaji wakifanya hivyo ingawa sikushangaa Kova alipofanya hivyo kwani nilidhani mafunzo wanayopata wote ni sawa sawa.
Kwa hiyo kama wewe ni askari au afisa rudi kafanye homework. kwa hiyo naunga hoja za wanaomsapoti Afande Kova.
 
Kwa maoni yangu kamanda Kova hakuwa sahihi kuipigia salute maiti ya Kanumba.

Sababu salute ni salamu au heshima ya kijeshi kwa mtu aliyekuzidi cheo au mamlaka.

Kova anajua miko ya salute lakini nadhani alipitiwa tu.

Mkuu mala ya kwanza nilidhani kama wewe kuwa amekosea,
lakini nimeuliza wataalamu wa mambo ya jeshi wanasema alikuwa sahihi kabisa,
kwa mwanajeshi akiwa amevaa kijeshi salamu yake kubwa ni salute,
Asingeweza kuinama wakati amevaa kijeshi na Salute inaonyesha heshima.
Na ndiyo salute hutolewa kwa uliyemzidi cheo lakini naye anarudisha kwa salute,
kwa hiyo mnapigiana salute mkuu!
 
JF kumbe wengi hamjui na hamtaki kuuliza mnaleta ubishi tuu, tafuteni data jamani!
 
Wewe ndi hujui protocol za kijeshi...kijeshi maiti yeyote inapigiwa salute...sasa wewe raia haya mambo huyajui bora ukae kimya...

Si ndio maana kasema hajui, sasa wewe unayejua umueleweshe sio kumwambie akae kimya.
 
Kama ana heshima ampigie basi Dk. Slaa kama haujasikia another version of story, labda aseme to the late Kanumba was secret service na alikua na cheo kuliko yeye, otherwise babu kachemka mazima
mkuu kila jamii duniani ina jinsi ya kufanya mambo yake pamoja na fikira. Kwa bahati mbaya wengi wetu hapa tz tulikuwa hatujajitambua upeo wetu wa kuangalia mambo lakini kwa hili tunaanza kupata picha kuwa sisi ni 'genius' kiasi gani

 
Well said and excellent comment. Tatizo hapa ni baadhi ya watu kuingilia fani wasiyoifahamu sawasawa.
 
Marehemu alivalishwa
sare yenye nyota fulani hivi,

itakuwa kova anaijua heshima/maana ya ile suti
ndo maana anapiga salute.

Naomba msaada kujua Kweli Salute ni nani anapigiwa kwani hapa naona anatoa salute wakati wa kumuaga Kanumba, I think this is not right, wanaojua please enlight me.View attachment 51467
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…