Ila paka wanafki unalijua Hilo? Mfano hai ni huu hapa, nilikuwa nikiishi na babu yangu, kuna paka nilimuokotaga jirani na nyumba ya wazungu, nikampeleka nyumbani, alikuwa ni mdogo sana nahisi alikuwa na siku mbili ama tatu tangu azaliwe, wengi hawakumtaka yule nyua sababu alikuwa analia sana, wakisema nimrudishe nilikomtoa, mi nikakomaa nikawa nampatia maziwa hata alipoweza kutembea vizuri na kula vyakula vingine,akakua, wakaanza mpenda, wakampakata na wakamuwekea minofu ya nyama, na mwisho paka akawa na sahani yake, muda wa kula ukiwekewa nyama mbili basi paka pia atapewa nyama mbili ama zaidi, kimbaumbau sasa akawa tukunyema, wanapishana na panya koridoni hata hastuki, akaanza upuuzi wa kunya ktk unga wa ugali na kuna siku alikunya ktk shati langu la shule, hapo nkatangaza kwamba huyo paka akiniona apotee mpaka nitapoondoka vinginevyo ntamuua, basi yule paka ikawa kama mimi ndo narudi na yeye yupo ndani atatafuta pa kuchomokea iwe dirishani ama mlangoni, na nitapoondoka ndipo atarudi, sasa kuna siku ikasemekana mimi nampiga paka kwa maana ninaporudi paka anakosa amani yaani akisikia sauti tuu mkojo unatoka, nikawaambia huyo paka ni mnafki sijawahi kumpiga ila nna plan za kumuua kwa kunya ktk shat langu..nakumbuka niliambiwa kama simpendi basi nihame kuliko kumuua so mimi nilihama nikamuacha paka home akitanua....kuna mtu alimuuwa baada ya mimi kusepa, nakumbuka walimpeleka hospital wakaambiwa kuwa alikula sumu, na alipata kipigo.....kwa hiyo mimi naamini paka anamjua mtu mwenye nia mbaya dhidi yake na unafki anao