GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Inasemekana kwamba Paka ndiyo Mnyama pekee ambaye anaweza kwa haraka sana kutambua ama roho mbaya ya Mtu au roho nzuri yake na kwamba huweza kukutambua kwa muda wa kati ya sekunde tatu hadi tano tu kukujua.
Ni kwamba kama ukiwa mmekaa Watu wawili na kuendelea kisha mara ghafla akatokea Paka na kwamba ukimwona tu huyo Paka anawatembelea ( kuwapapasa ) sana Wenzio pale tena bila wasiwasi huku Wewe akikuchunia jua ya kwamba tayari anakuwa ameshajua Kipaji cha Upendo cha wale wenzako na pia kukijua Kipaji chako cha Roho mbaya iliyokutukuka.
Hii kitu imekwenda mbali zaidi na kusemekana kwamba hata kwa Mzazi ambaye una Mtoto wako mdogo ( Toddler ) kama ukitaka tu kujua haraka jinsi tabia yake itakavyokuja kuwa kama akikuwa basi mchukue Paka kisha msogeze nae na ukiona yule Paka anaonyesha ushirikiano nae vizuri kila mara jua umezaa Mtoto mwema na kama ukiona kila ukijitahidi tu kumbeba Paka na kumweka na Mwanao huyo ama Paka analia au anataka kukimbia au pengine hata Kukung'ata jua ya kwamba umetuletea Tanzania Njemba yenye roho mbaya sana.
Je hili lina ukweli gani Wadau?
Karibuni mtiririke na mserereke.
Shikamoo Paka!