Jamani Hii Elimu Inaelekea wapi!???

Ugiligili

JF-Expert Member
Jun 20, 2014
3,023
4,053
Habari za jioni wakuu..
Nimehuzunishwa sana na hiki kinachoendelea kwenye baadhi ya Shule zetu za Serikali ambazo waTanzania wengi wenye kipato cha chini ndo tunawapeleka watoto wetu..

Kuna watoto watatu hapa..mkubwa drs la tano mwingine la tatu na wamwisho la pili.Wanasoma SHULE YA MSINGI NYARIGAMBA iliyopo MUSOMA MJINI MKOANI MARA
Tatizo lililopo ni kwamba leo nilikuwa nakagua maendeleo ya watoto hapa nyumbani cha kushangaza katika maongezi watoto waliniambia kwamba WALIMU wao huwa WANAWAPA DAGAA WACHAMBUE Hata kama wakiwa ktk MUDA WA VIPINDI DARASANI.Nilishangazwa zaidi waliposema huwa inafika kipindi wale wenzao wa drs la sita wanaletewa samaki watengeneze.Na hawa walimu wamezoea na ni zaidi ya miaka miwili wanafanya huu ujinga..

Jamani wazazi tuwaulize vizuri watoto wetu na tufuatilie maendeleo yao kwa ukaribu maana sometimes tunawalaumu watoto kwa perfomance mbaya kumbe makosa sio yao ila ni walimu wasio na weledi ndo wanashusha elimu yetu.
Hii inakera sana aisee mtoto anaenda shule yupo smart anarudi ananuka shombo ya samaki na dagaa.

Nimeamua kutaja na jina la shule ili hili swala lifanyiwe kazi.Na wakuu kama kuna shida kama hizi zinatokea kwa watoto wenu tupaze sauti tuzitaje hizi shule labda itasaidia wajirekebishe ili watoto wetu wapate elimu bora.Asanteni sana.
 
safi sana... tena ikiwezekana wapewe na mahindi wakasage... kama serikali hainijali unategemea mi ndo nijali wanafunzi..!
Mkuu mwisho wa siku hasara ni kwetu sisi wazazi/walezi..tutatengeneza kizazi cha wajinga kama tukikubaliana na hili swala..
 
Mzazi usipofuatilia maendeleo ya mwanao hasara ni kwako. Si kayumba wala private schools. Walimu wa siku hizi wamekosa moyo na hawaipendi kazi yao. Wengi wanafanya kwa sababu hawakuwa na mbadala wa kazi ya kujipatia kipato.
 
Haha nilisoma hapo miaka 20 iliyopita, hiyo kaz tuliifanya sana tena tulikuwa tunagombania, mwl akikuchagua unaona fahari sana
Nikahamia Mwisenge huko ndo basi tena, tulipanda sana maharage na mahindi kwenye mashamba ya walimu , huku majengo mapya,
Umenichekesha mkuu..ingawa inauma sana
 
Waligoma zamani kufundisha wewe ndo umelijua Leo????!!!!! Au unasubili waingie barabarani Kwa maandamano wapigwe virungu, hahaaa... Siku hizi watu wanagoma kidigital!! Ipigie kelele sirikali iwalipe stahiki zao.
 
Mkuu mwisho wa siku hasara ni kwetu sisi wazazi/walezi..tutatengeneza kizazi cha wajinga kama tukikubaliana na hili swala..
kizazi cha wajinga mbona kwenye siasa tayari kishatengenezwa.... umesahau mwanasiasa anatakiwa ajue kusoma na kuandika tu... hata akipata 0 fresh tu hatakaguliwa cheti..!
 
Habari za jioni wakuu..
Nimehuzunishwa sana na hiki kinachoendelea kwenye baadhi ya Shule zetu za Serikali ambazo waTanzania wengi wenye kipato cha chini ndo tunawapeleka watoto wetu..

Kuna watoto watatu hapa..mkubwa drs la tano mwingine la tatu na wamwisho la pili.Wanasoma SHULE YA MSINGI NYARIGAMBA iliyopo MUSOMA MJINI MKOANI MARA
Tatizo lililopo ni kwamba leo nilikuwa nakagua maendeleo ya watoto hapa nyumbani cha kushangaza katika maongezi watoto waliniambia kwamba WALIMU wao huwa WANAWAPA DAGAA WACHAMBUE Hata kama wakiwa ktk MUDA WA VIPINDI DARASANI.Nilishangazwa zaidi waliposema huwa inafika kipindi wale wenzao wa drs la sita wanaletewa samaki watengeneze.Na hawa walimu wamezoea na ni zaidi ya miaka miwili wanafanya huu ujinga..

Jamani wazazi tuwaulize vizuri watoto wetu na tufuatilie maendeleo yao kwa ukaribu maana sometimes tunawalaumu watoto kwa perfomance mbaya kumbe makosa sio yao ila ni walimu wasio na weledi ndo wanashusha elimu yetu.
Hii inakera sana aisee mtoto anaenda shule yupo smart anarudi ananuka shombo ya samaki na dagaa.

Nimeamua kutaja na jina la shule ili hili swala lifanyiwe kazi.Na wakuu kama kuna shida kama hizi zinatokea kwa watoto wenu tupaze sauti tuzitaje hizi shule labda itasaidia wajirekebishe ili watoto wetu wapate elimu bora.Asanteni sana.
Nilidhani lá maaana sana,

Bother wakati unasoma ulikwepa Stadi za Kazi,
Pole kwa hilo, kaanao uwaelimishe waambie Stadi Za Kazi hão wajomba zako
 
Mkuu mwisho wa siku hasara ni kwetu sisi wazazi/walezi..tutatengeneza kizazi cha wajinga kama tukikubaliana na hili swala..
Akiwa mjinga, mpeleke akateuliwe awe mkuu wa mkoa, hutapta hasara. Pale wenye sifa ni wale wenye sifuri
 
Nilidhani lá maaana sana,

Bother wakati unasoma ulikwepa Stadi za Kazi,
Pole kwa hilo, kaanao uwaelimishe waambie Stadi Za Kazi hão wajomba zako
Acha ujinga wewe.!! Yan km ndo mnatumia kivuli cha stadi za kazi kuwachambulisha dagaa na samaki watoto wadogo basi mna matatizo ya akili..
Haya niambie ni mtaala gani unasema mtoto achambulishwe dagaa na samaki kuanzia drs la pili mpk la tano!??? Na huo mtaala utumike kwenye baadhi ya shule tu!?? Acha kuleta upuuzi kwenye mambo ya msingi wewe!
 
Back
Top Bottom