Jamani hapa kosa likowapi?

Cyclone

Member
Nov 19, 2011
71
14
Unaamua kumuacha mpenzi wako wa sasa na kurudiana na mpenzi wako za Zamani, mme ombana misamaha na mmekubaliana kurudiana. Kwanini hivi? baada ya kuachana kwa muda mrefu mnagundua kuwa kama vile mlipangiwa kuwa pamoja so mnarudiana, unamueleza mpenzi wako wa sasa ukweli juu ya hili?

je kosa lako hapa likowapi ?kwani kama ukiendelea kuwa naye utakuwa ni wizi mtupu upendo umerudi kwa zamani.
NB: hakuna external factor yeyote iliyo pelekea maamuzi haya ila tu labda destine
 
Kosa lipo kwa 'destine'.

Kama umeshamwambia ukweli inabidi akubali tu hali halisi.
 
Ndo maana nasema sisi tusio na wanawake wakati mwingine tuna furaha!
 
kosa ni la kumpotezea muda mpenzi wako mpya. Kama ulikuwa bd wa mpenda wa zaman ungesubiri myasuruhishe
 
Hakuna kosa kwan umeamua kuwa mkweli,ni wanaume wachache sn wenye uungwana huu!
 
Kwaupande wangu kama tulishaachana na nimepata mpya naendelea nae huyo wazamani aendelea na mwengine, huyu mpya hana kosa kanipokea kwa mikono miwili vp nimuache kisa wazamani karudi au kaja omba samahani turudiane,hakuna cha destine wala nini ajipange mbele.....
 
Arabian.. hapo utakuwa hukumpenda wa kwanza ila kama ulimpenda aisee lazima utashidwa kuvumilia tu
 
Arabian.. hapo utakuwa hukumpenda wa kwanza ila kama ulimpenda aisee lazima utashidwa kuvumilia tu

Hapana hata kama nilimpenda kama basi ishakua basi, jee huyu mpya nilienae hana kosa na amenipokea kwa mikono miwili,amenipa mapenzi wakati yule wa mwanzo tulipo achana leo eti kisa wa zamani karudi ndio nimtose huyu nilonae hapana,kosa lake nn huyu nilokuanae? vp nisahau wema alonitendea au nna hakika gani kama hatonitema tena? kwaupande wangu atabaki zilipendwa,na hata mawasiliano nae staki....
 
Jamani, kuna wa zamani ambaye huwa hasahauliki, ije mvua lije jua.
Akikohoa tu unarudi mikono miwili
Kama umeshaoa au kuolewa waweza vunja ndoa.

Haya mambo hayana fomula, hakuna MAGAZIJUTO wala nini
 
Unaamua kumuacha mpenzi wako wa sasa na kurudiana na mpenzi wako za Zamani, mme ombana misamaha na mmekubaliana kurudiana. Kwanini hivi? baada ya kuachana kwa muda mrefu mnagundua kuwa kama vile mlipangiwa kuwa pamoja so mnarudiana, unamueleza mpenzi wako wa sasa ukweli juu ya hili?

je kosa lako hapa likowapi ?kwani kama ukiendelea kuwa naye utakuwa ni wizi mtupu upendo umerudi kwa zamani.
NB: hakuna external factor yeyote iliyo pelekea maamuzi haya ila tu labda destine

kosa ni kumweleza baada ya kutafuna tunda lake....................lakini kama hujaligusa hakuna shida................bado mlikuwa hamjaenda mbali naye.....................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom