Jamani eeh, ninaombeni msaada wa haraka

Kitombise

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
8,518
25,437
Nina mpenzi wangu ambaye nimedumu naye muda mrefu sana na nilikuwa na malengo ya kumuoa kati ya mwakani au mwaka unaofwata ila kuna tatizo limenitokea muda huu hapa na hilo tatizo ndo limenifanya niandike uzi huu mufa huu nikiwa na ghadhabu na huku nikiwa naomba ushauri pia.

Ishu yenyewe iko hivi:

Baada ya kuwa naye nikagundua kuwa bado ana mawasiliano na Ex boyfriend wake wake. Na nilipomuuliza akaniambia kuwa bado wanawasiliana ila walishaachana tokea kitambo na huyo jamaa kwanza kashaoa.

Akadai kuwa kama simuamuni basi anaweza pia akanikutanisha naye ilinidhibitishe.Mimi nkamwambia haina haja yakunikutanisha naye coz ninakuamini na hiyo siku tulivyokutana jamaa alikuwa ana simu ya tekno c8(hiyo ilikuwa ktk kumdadisi huyo jamaa) basi baada ya hapo maisha yakaendelea kama kawaida.

Kuna simu huyu mpenzi wangu akaniambia kuwa anatamani kuwa sana kutumia tekno c8 mimi nikamwambia kuwa nikiwa fresh basi nitakununulia.. huku yeye kwa wakati huo anatumia tekno s5.

Basi siku zikaenda weee,ila hivi juzi juzi tukiwa tumepanga kukutana basi demu akawa anakuja na simu yake ndogo ila nikimuuliza anasema iko kwenye charge wakati unakuta muda huo huo nimetoka kuchat naye whatsApp,
hilo mimi wala sikulitilia shaka.

Sasa wakati huu nmetoka kuonana naye hapa akaja na simu yake kubwa hivyo nkamuomba niingie mara moja LiveScore niangalia mechi za UEFA zinaanza muda gani. Mara heeeee! nashangaa anatumia Tecno c8 pale pale nkashtuka sana na kumwambia hii simu umeipata wapi na mbona hujaniambia kuwa unayo? Akasema alisahau kunijulisha.

Sasa nmevuta picha weee nimeona hapa huenda yule Ex wake ndo atakuwa amempa hivyo nmejawa na hasira hapaaa mpaka nataka kupasuka maana nikiunganisha matukio naona kabisa kama huenda hii simu atakuwa amehongwa na huyo Ex wake.

Wadau naombeni ushauri wa chapu chapu ili nichukue hatua ya haraka sana kwa huyu girlfriend wangu.

Sasa napiga kura wanaosema nimuache waseme MUACHE na waosema niendelee waseme USIMUACHE.

Ntahesabu kura zenu wadau na wataocomment kwa wingi ndo ushauri nitakaochukua huo huo.


Sorry kwa uandishi mbovu coz nimeandika hapa nikiwa na jazba balaaaa.
 
Mapenzi mapenzi mimi nakosa amani.

Kwanza relax, hebu fata hitaji la moyo wako
 
Kwan huyo dem wako anafanya kazi gan? Na je kipato chake hakimtoshi kujinunulia cm mpk nyie wanaume zake mmuhonge? Mfumo dume kero tup? Kama kuachana yeye ndo katangulia KUKUACHA cjui nikushaurije? MUOMBE MSAMAHA
 
Kwan huyo dem wako anafanya kazi gan? Na je kipato chake hakimtoshi kujinunulia cm mpk nyie wanaume zake mmuhonge? Mfumo dume kero tup? Kama kuachana yeye ndo katangulia KUKUACHA cjui nikushaurije? MUOMBE MSAMAHA
ñdo mana nmesema kuwa nmeandika kwa jazba mpk nkashinfwa kuorodhesha mambo mengne..
bado ni mwanafunzi hivyo hana kazi kwa sasa
 
Duh! Kumbe siku hizi mwanamke anaachwa kirahisi hivi kwa sababu ndogo tena tu eti kwa sababu kafanya 'jambo la maendeleo'? Dah, hapo nimeishiwa nguvu na sijui cha kukushauri ila maoni yangu ni kwamba wivu utakuponza udondoshe vitamu wengine wavifaidi...
 
Back
Top Bottom