Jamani biashara hii ya daladala ni pasua kichwa

Siku zote usicheke na Konda, dereva! Hao watu wakikuona laini laini tu umekwisha, kama mmekubaliana kwa siku ni sh 50000/=
Hakikisha inatimia. Kingine kwakuwa wao ndo wanashinda na gari, service ndogo ndogo na faini visiwe juu yako wewe, vinginevyo utafanya services na faini fake kila siku mwisho wa siku gari inakufa wanakuacha huna kitu.
Pamoja mkuu, nimekuelewa.
 
Nafatilia kwa makini maana na mimi nina mpango wa kuingia kwenye sekta ya usafirisha kwa upande wa daladala. Hope kukupitia uzi huu ntapata kitu
Hiyo biashara ni vizuri ukae mwenyewe ukonda, tafuta dereva mzuri upige nae kazi lakini kama unazo nyingi usidhubutu kumuweka ndugu yako kuwa dereva au konda, pia hakuna kucheka na dereva wala konda mlichopatana ndio kije hicho.
 
Hiyo biashara ni vizuri ukae mwenyewe ukonda,tafuta dereva mzuri upige nae kazi,lakini kama unazo nyingi husidhubutu kumuweka ndugu yako kuwa dereva au konda,pia hakuna kucheka na dereva wala konda mlichopatana ndio kije hicho.
Asante sana nduug maana nilikuwa namwandaa mdogo wangu ili akae mlango
 
Baada ya kutoka chuo kikuu, niliamua kufanya biashara ya daladala ili maisha yasonge, cha ajabu hii biashara ni pasua kichwa . Utasikia mara tochi , bao mara gari imehalibika nk

Binafsi napenda sana biashara ya usafirishaji , kama kuna mtu ana uzoefu nayo zaidi naomba anisadie.

Pili , kama kuna fursa zingine nzuri zaidi naomba tushirikishane jamani , naweza nikapiga hii chini nikawekeza kwingine.
Kama huwezi kusimamia hiyo daladala uza maana biashara ya daladala ni kuwa makini kwenye usimamizi. Mimi nina DCM limenishinda kwa ajili ya usmamizi, nakosa muda wa kusimamia kwa sababu ya shughuli zangu hiv sasa liko sokoni naliuza
 
Kama huwez kusimamia hiyo daladala uza maana biashara ya daladala ni kuwa makin kwenye usimamiamizi. Mimi nina DCM limenishinda kwa ajili ya usmamizi nakosa muda wa kusimamia kwa sababu ya shughuli zangu hiv sasa liko sokon naliuza

Mkuu kabla hujaliuza nipe usimamizi kwa mwezi mmoja tu. Thank me later
 
Kuna kipindi nilikomaa mwenyew hesabu ilikuwa haipungua 2,500,000 kwa mwez, toka nianze kukabidhi madereva hesabu ni kichefuchefu kila siku sababu haziishi hesabu hata milion haifiki kwa mwez na gari inazidi kuchakaa nikaamua kupaki
 
Kama huwez kusimamia hiyo daladala uza maana biashara ya daladala ni kuwa makin kwenye usimamiamizi. Mimi nina DCM limenishinda kwa ajili ya usmamizi nakosa muda wa kusimamia kwa sababu ya shughuli zangu hiv sasa liko sokon naliuza
ASEE TUWASILIANE TUFANYE BIASHARA YA HY DCM, NAITAKA. .....TAFADHALI KIONGOZI
 
Biashara hii yahitaji usimamizi mkubwa sana,kwanza kuwa na mkataba na Dereva means pia mwisho wa mwezi atakuwa na mshahara,mwache awe huru mwenyewe kutafuta konda wake ila wewe utadili na yeye tu,nunua vitu vyako kwaajili ya service na chagua siku maalum ya kufanya service,mfano mi hufanya Service jumapili ,hakuna gari yyt kufanya kazi jumapili ni siku ya service na yupo fundi maalum,service ndogo anahusika dereva,service kubwa zinakuhusu tajiri. Dereva kabla ya jumapili atakwambia kesho yake anaservice gani na gani,ataleta hesabu mliyokubaliana kwa siku mi hiyo siku ya service ndo huleta hesabu ya wiki nzima yaani siku 6. Kuwa na mkataba wa kutokuendesha nje ya root na iwapo atafanya hivyo kazi hana na litakalomkuta atawajibika,so means makosa yote ya kizembe ya barabarani sijui traffic kafanyaje anahusika yeye,labda itokee imekamatwa mfano bodi imechakaa,au viti vimeharibika na aliniambia sikutake action hapo nitawajibika mimi. Kuwa na muda maalumu wa kupaki gari,kama kupaki gari ni saa mbili usiku iwe hivyo siku zote labda itokee ana tenda maalum.

Mkataba wa kazi ndo kiongozi wako,itakuongoza wewe,itamuongoza dereva itamfanya kuwa mwaminifu kwa kazi yake na kuipenda na ataipenda gari,kuwa mtu mwenye msimamo na serious haswaa hasa kwenye swala la pesa na uzembe. Lakini pia kuwa friend kwao siku moja moja cheer up with them wanapofanya vizuri mpe bonas hata buku 10 sikiliza matatizo yao,solve them. Utaishi vyema sana yaani mimi nina madereva wengine huu ni mwaka 6 hata sijabadilisha na ninapoongeza gari wao wenyewe wanakuwa wa kwanza kunitafutia faithfully person,hesabu yangu kwa mwezi kama kawaida ile ile expected na Mungu akibarikia uharibifu mkubwa hujatokea kwenye gari basi ni bam bam. Kikubwa magari yanatakiwa uyapende uyafanyie service za ukweli usiwe mbahili utainjoi sana,mambo ya kubadilisha oil ziwe kama ilivyopangwa kwa kilometre zile zile,penda kunotis utofauti wowote unaouona kwenye gari jua umetokea kwasababu gani siyo unaona tatizo unalifumbia macho,na kama dereva yeye aliona anasikia kila siku hakusema atakuwa responsible kwa uzembe huo. Usikate tamaa pambana utatoka ni biashara nzuri hutajuta.
 
Umeeleza vizuri sana na kuondosha tamaa ya madereva kuna jamaa yangu yeye kamwachia dereva siku ya service akimaliza apige tu route atafute pesa kwa ajili yake na familia yake.

Hata kwenye hesabu wakati daladala nyingi wadosi wakipandisha hesabu toka kwenye sabini mpaka mia yeye alimwambia suka alaze 85 tu.

Kiukweli hajawahi kulalamika.
 
Yes lazima uwe na mbinu mbalimbali ambazo utamfanya dereva kuipenda kazi yake na kuithamini.
 
Back
Top Bottom