Habari za siku nyingi wadau?
Niende all the way kwenye mada. Mimi ni mfanyabiashara mdogo mdogo (machinga). Kiufupi kuna binti wa chuo nilikuwa namlipia kuanzia ada, hostel na kumsaidia kila kitu kwenye masomo yake, kuanzia mwaka wa kwanza mpaka sasa anakaribia kumaliza mwaka wa tatu.
Cha ajabu hivi karibuni amechange ghafla baada ya kuniomba laki 5 nikamuambia anivumilie kama wiki moja hivi, anadai eti nimepunguza mapenzi kwake eti simjali sana kama zamani, bora hata amkubalie yule mtu anayesoma nae chuo labda anaweza kuwa mtu sahihi kwake.
Anasema mimi niendelee na mchepuko wangu. Kiukweli sijawahi kulia kwa sababu ya mwanamke ila jana nimelia kwa mara ya kwanza, hasa nikifikiria gharama nilizotumia hapo awali, kwani nilikuwa zaidi ya mzazi wake.
Najuta kwanini nilimfahamu huyu mdada, naombeni ushauri wenu wadau nimfanyeje huyu mtu?