Jamaa yangu ananuka mdomo sana. Nitumie njia gani kumfikishia ujumbe?

Umnunulie dawa "ya mswaki" afu mwambie awe anatumia.
 
1. Mchunguze kama ana Cavities / ukoko kwenye meno juu ya fizi. Atumie Hydrogen Peroxide.
Siku hizi Kuna Whatsapp status andika ujumbe Hapo naa Picha ya Hydrogen Peroxide.
2. Kuna kunuka kinywa Kwa ajili ya njaa, harufu inatoka Tumboni. Ale Kwa wakati.

3. Kunuka kinywa toka kwenye oesophagus. Kusafisha Oesophagus Kwa kunywa Maji ya vuguvugu kitu Cha kwanza asubuhi kutazuia harufu ya mabaki ya chakula.

4. Damu kujaa kinywani kutokana na fizi kutumia husababisha harufu pia. Asukutue na maji chumvi Kila baada ya mlo.

Narudia Tena Tumia Wasap status au tafuta mtu arekodi kuhusu watu wanaonuka vinywa TIKTOK Kisha Share mara nyingi Hadi aipate.
 
Wengine tatizo halianzii hapo mdomoni, tatizo liko ndani zaidi, kwa hiyo unaweza kuta anaswaki lakini harufu ndio kwanza inajiandaa kutoka vizuri kama choo cha stendi.
 
Rafiki wa kweli
 
Huyo siyo mwanao z unajua maana ya neno mwanangu .. yaani mwana .. Wana ...
Usiwafanashe wanangu na wanao.

Mimi na mwanangu Tunaambizana ukweli .. mimi na wanangu tunaelekezana mambo ya msingi , mimi na wanangu kuna mda tunaact childish .. mimi na mwanangu before chochote chenye manufaa tunakaa chini tunajadili ...

Huyo siyo mwanao kama ni mwanao , mwambie yo dude ya mouth stinks like nyash .. nenda kasafishe .. mara tatu mara nne ..imeshindikana mwende hospitali itakuwa ni matatizo ya kinywa
 
You are so sweet, May God bless you!
 
Inategemea na nguvu yako ya ushawishi (kutongoza) kama unayo mwambie na umshawishi mtafute tiba. Kama huna maneno mazuri basi tumia mbinu ya jamaa hapo juu aliyeenda na jamaa yake hospitali.

Binafsi nimejaliwa kutoa masomo, mtu hata akijisikia vibaya kwa nilichomwambia ntakomaa nae hadi atatekeleza na atapona.
 
Kama unaweza kumsaidia tumia mbinu huu, mdangaye kuwa Tangawizi kama kangawizi ni dawa zaidi ya mzizi wa congo, awe anatafuna kila anapotaka kulala na anapoamka asubuhi, hapo utakuwa umemsaidia maana Tangawizi ukitafuna inakata harufu harafu inapambana na wadudu wanaozalisha harufu mbaya mdomoni pia hata wale wadudu wanaoharibu meno huwa wanakufa endapo utatafuna tangawizi mara kwa mara,
Pia Tangawizi huboost misuri ya uume, ki ukweli Tangawizi ni dawa ambayo inatibu magonjwa mengi hakika niamini
 
Kati ya sababu ya kunuka mdomo na kutoa harufu kali ya jasho ni pamoja na magonjwa ya ngozi pia, naomba yeye na wengine wenye matatizo hayo wafanye vipimo vya magonjwa ya ngozi kama fungus / mmba. Kama itabainika wana hilo tatizo watumie dawa za ngozi.
 
Vipi na wale wenye mgando mgando sijui ukoko wa njano na kijani ivi (sidhani kama nishawahi kusikia anatoa harufu mbaya kinywani mana nipo nae mikoa tofauti)

Anaweza tumia nn kutoa na kuwa na meno clear bila izo ukoko???
 
Mkuu mimi nadhani hii sio nzuri kwa sababu atahisi unakua unamsimanga. Kwangu njia bora nadhani ni kumwambia live katika namna ya kumsaidia au kuna jamaa kasema azuge kama anamsindikiza hospital then wakifika huko dokta anamaliza kila kitu.

Hiyo imekaa kiswahili sana na inawezekana haitamsaidia au asiione pia
 
Mwambie kwa kiingereza, watu wengine ata wakitukanwa kwa kiingereza wanafurahi
 
Hapa kila mtu alimnunulia dawa rafiki au alikuwa na rafiki mwenye harufu ya mdomoni, sijasoma bado mwenye personal experience


Anyways ni somo zuri pia, huenda baadhi yetu hapa tumeshajifunza kitu, actually nimesikilizia harufu mda huu, hivi unaweza "kujisikilizia"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…