Jamaa wanajenga afya... Naona wivu jamani.

na kwa mjamzito, eti mtoto atazaliwa bila nywele

au kama ni binti, ataolewa mbali na nyumbani.
Wanawake wakila vitamu watashindwa kuwalea watoto halafu kama ananyonyesha maziwa yanaweza kuharibika. By mababu zetu
 
sasa wale unawalaje?
Mwili mzima walikuwa kichwa
na vichwa vyao vilikuwa vigumu kama zege

Hata hao ni chakula kizuri tulikuwa tunawanasa kwa kuchomeka kinyasi ndani ya tundu halafu wanang'ata then tunawachoropoa
 
dar es salaam hamna kumbikumbi. ukitaka kula kumbikumbi nenda pale kwa sadala karibu na boma ng'ombe moshi.

hapo Bomang'ombe wanauzwa au ni wa dezo?
Miaka kadhaa nyuma nikiwa Azania kuna siku waliingia darasani kwa fujo, wacha nijinome kumbikumbi wabichi...
 
Kumbikumbi watamu bana,nakumbuka enzi hizo mvua zikinyesha tunaenda asubuhi kiwanjani kuwafukua,kazi inaisha saa tano asubuhi halafu baada ya hapo tunakarangiza -kula na ugali tena wa dona (si azamu) we utajing'ata...umenikumbusha mbaliiii Mphamvu.

Wapi Chumbo,Mwita,Joseph,Patrick (expert wa kumbikumbi wa kichuguuni),sadick n.k? Halafu enzi hizo hata kama kwenu ni masikini you dont feel that so much!

hata sisi ilikuwa ni wakati wa mvua mkuu, lakini sisi hula kumbikumbi kwa burudani, hatuli na ugali wala chochote.
Kuhusu umasikini ni kweli, since poverty is a comparison item. Hakuna matajiri, hakuna umasikini.
 
ndugu yangu mphavu huo ni mlo mzuri kwako wewe mboga saba, lakini kama ni chakula cha kila siku kwako basi wala usingesema tunafaidi. huku ukerewe kwenye mwaka 1990 na 1991 kulikuwa na njaa, tulikuwa tukila ugali kwa ndimu / limau au chumvi. na ugali wenyewe tumepata msaada wa kanisa katoliki. asante sana Padre Ferdinand Mwalimiu paroko wangu wa Parokia ya Nansia, siku nyingi sijakusikia.
 
ndugu yangu mphavu huo ni mlo mzuri kwako wewe mboga saba, lakini kama ni chakula cha kila siku kwako basi wala usingesema tunafaidi. huku ukerewe kwenye mwaka 1990 na 1991 kulikuwa na njaa, tulikuwa tukila ugali kwa ndimu / limau au chumvi. na ugali wenyewe tumepata msaada wa kanisa katoliki. asante sana Padre Ferdinand Mwalimiu paroko wangu wa Parokia ya Nansia, siku nyingi sijakusikia.

yeah.
Ndio maana nimesema kuwa anasacally wanaumia, ili nutritional wako juu.
FF na MS wakisikia kuwa kanisa limetoa chakula atasema ni hela za MoU, afu itakuwa taab bureh...
 
unamkumbuka fifi, na flinti miksa Kipara McRegan? Kwenye ile filamu ya masokwe, walifanya hivyo kula mchwa.

Aisee nimecheka sana nilipoikumbuka hii movie hasa Kipara McReagan, itabidi niitafute tena
 
I guess hawapendi, na kuna watu wanawasikitikia.
Ndio maana nikasema tuache anasa zote, tujadili viinilishe katika kumbikumbi na mbogamboga.
Am I right?

Mphamvu acha maskhara na njaa za watu, wenzio wanalia shida siyo starehe jamani. Unaweza ukala hao wadudu ukashiba?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom